Viongozi ndiyo wanaokwamisha mchakato wa mabadiliko, FCC yatoa taarifa leo. Mashabiki na wanachama wa Simba mtadanganywa hadi lini?

Mhindi usiwafokee mbumbumbu
 
Sidhani hata kama na wewe unaelewa tatizo liko wapi.
Tatizo lililopo Mo ni mzamini kwa sasa maana bado hajawekeza pale simba kile kiasi kilichopo kwenye mkataba ili awe mmiliki halali wa 49%.
Mkanganyiko unapokuja ni kua kama uwekezaji bado je yeye anawezaje kuwa mwenyekiti wa bodi?
 
Mo Barba
 
Barua ya FCC imejitosheleza kuwa MO ni muhuni.
Mawazo na ushauri kwa Mudi afate maelekezo ya FCC.
 
Sijakataa mkuu lakn kumbuka n huyuhuyu MO ndiye aliyesema kuwa mchakato umekamilika kwa 97% je alimaanisha nn? Unajua wengi tunaangalia matokeo ya Leo ya timu yetu kuwa inashinda vikombe vya ndan lakn hatuangalii future ya timu kujiendesha bila kutegemea hawa maponjoro

Yanga enzi za YUSUFU MANJI ilinshinda kila kitu cha ndani na wakjisahaulisha kuwa hawana shida Leo wenyewe mnaona nn kinawakuta

FCC wapo pale kwa ajil ya kuweka mambo sawa kila upande utimize wajbu wake

Kama mchakato bado he mo anahudumu simba kam nani na anamamlaka yap hadi achague Co mpya wakat mchakato bado ?

Sasa tuchague moja je tunataka furaha yamuda mfupi kama yanga kwa manji au tukomae na FCC ili mchakato uende mbele ili tufurah milele?

Hamis kigwangala alisema haya mwenyekiti upande wa wanachama SUED NKWABI aliyasema haya kuwa IPO. Siku ukweli utajulikana na ndio huu umejulikana wazi
 
Mo-pesa ,Mo- maarifa,Mo-mafa ikio,lakini wanaoumia sanaaa ni timu wananchi,hawapendi na haitatokea kupenda mafanikio ya Mo +[emoji881][emoji460], pilipili isiyoila inakuwashia Nini [emoji196][emoji196][emoji196]?
Sisi mwananchi wenye Akili tulishajua hapa kuna janja janja wanafanyiwa mbumbumbu
 
Mo Simba Arena, Mo Simba foundation, Mo energy, Barbra jamaa ndo anapata sana kuliko simba
Simba pia inanufaika,pesa ya usajili, mishahara ya wachezaji,huduma za kambi nk., waacheni fitna.
 
Haya alishayaona Dr Kigwa,akatoa ushauri kuwa kanjibhai aweke mzigo mezani kabla ya ajira ya house girl wake kwenye timu.. Dr alitukanwa matusi balaa
Tatizo aliomba bodaboda
 
Kanjibay mjanja mjanja sana yaani ukisoma hapo no.6 utagundua kiasi kilichopo kwenye mkataba sio hiyo billion 20 inayotajwa mitandaoni.
Nakubaliana na wewe kbsa, hapo huwenda kiasi kinachotajwa majukwaani ni kikubwa kuliko kilichopo kwenye mkataba
 
Wadaawa ndo kina nani mkuu?
Simba hao........nadhani ni kiswahili ambacho hakijazoeleka Sana kutumika,nadhani ni neno wanaolitumia kwenye mishe zao na litakuwa limetafsiriwa toka lugha ya malkia,soon tutalielewa vema
 
Kanjibay mjanja mjanja sana yaani ukisoma hapo no.6 utagundua kiasi kilichopo kwenye mkataba sio hiyo billion 20 inayotajwa mitandaoni.
Mkuu unahisi mkataba una kuasi cha 50b au?
 
Angalao wewe unapoint zinazofikirisha. Natamn uendelee kutoa kutoa uchambuzi zaidi tunaweza kupata point zaidi
 
Swali nzuri sana. Viongozi wa Simba waje watupe majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…