Wengi wanaompinga MO sio kwamba wana uchungu na Simbasc ni watu wanao ona wivu na watengeneza fitna, ni kawaida ya ngozi nyeusi!!! Maana ukiwasikiliza wapingaji wengi hawana mawazo mbadala zaidi ya kejeli na matusi kwa muekezaji!!
Kauli zao ni "Simbasc inaibiwa" muhindi ni mjanja anafaidika sana, hawasemi anafaidika nini na kwa kiwango gani?!!! Akili za wamatumbi "waswahili" ni shida. Kwa akili tu kabla ya kuja kwa bw. MO simbasc ilikuwa kama kikundi cha tu cha watu kisichokuwa na vision wala mission ya kueleweka, uyu muhindi amejaribu angalau kufanya kitu kinachoonekana.
Kama tunaitaji kukosoa ni ruksa tukosoe uku tukionyesha njia sahihi za kupita na sio makelele tu kama tupo kwenye vijiwe vya walevi!! Tumeona simbasc imebadilika inalipa mishahara kwa wakati, inasajili wachezaji wazuri angalau kwa ukanda huu, ina wataalamu wa benchi la ufundi na imetoa ajira kwa vijana wengine kwenye engo tofauti za kiofisi!! Yote hayo uwezi kusikia wakosoaji walau wakipongeza!!
Mimi ninachoona MO Dewji anajaribu kutengeneza taasisi yenye brand ya kueleweka ili baadae aje atengeneze faida ambayo watagawana yeye na wanahisa wenzake ambao watakuwa wanamiliki share!! Kitu ambacho ndio lengo la mfanyabiashara yeyote yule, kitu ambacho sio kibaya hata kidogo, ila kwa sasa mtu akisema anafaidi sijui anapata zaidi ni uongo mkubwa na mtu wa dizaini iyo hajui biashara!! Biashara ya mpira kwenye nchi maskini kama hii ambayo haina miundombinu ya mpira wala mazingira rafiki ya uwekezaji wa mpira ni ngumu kufanikiwa!!! Ndio maana wafadhili wengi wa vilabu vya Simba and Yanga wa zamani waliishia kufilisika tu!! Washabiki wa nchi hii wanajaa mechi moja wakikutana watani!! Hata mapato yanayopatikana hapo ukichunguza asilimia kubwa yanaenda kwenye taasisi za serikali, na timu zinabaki na chini ya asilimia 30 tu. Sasa hapo ni mwehu tu anaweza kusema kuna faida!!
Kuhusu biashara ya jezi nayo ni utata mtupu washabiki wengi wanavaa jezi feki, ambazo mapato yake yanaishia kwa wanjanja wa kikinga hapo kariakoo!! Hakuna udhibiti na serikali ipo kimya!!!
Nafikili kuliko kumkosoa MO kwa kumuita majina mabaya na kumtuhumu ebu tumpe ushirikiano wa mawazo ili walau tuone tutafika wapi!! Maana kiukweli hizi timu kubwa zikisimama vizuri zitainua soka la nchi hii kwa asilimia kubwa.