Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Viongozi wetu, tena wa CCM na Serikali, wameiharibu kabisa Masaki na Oysterbay, kutokana na kuharibu Mipango Miji.
Taratibu, Masaki na Oysterbay zinageuka kuwa Upanga , kumbi za Disco, makunywaji na Mtaa wa Uhuru, badala ya makazi ya viongozo waandamizi wa serikali.
Leo viongozi wenzao chipukizi wamerithi kero za malelele katika makazi yao. Kumbi za disco , bar na biashara ziko kila mahali.
Waliosababisha yote hayo ni viongozi binafsi wa chama na serikali, kwa tamaa zao.
Viongozi wengi bado wana mentality ya kule walikotoka na matamanio yao ni utajiri wa haraka haraka.
Matokeo tunayaona hata kabla ya kizazi chao kutoweka.
Heko Meya Songoro kwa kuliweka wazi.