Ungesaidia kutoa taarifa basi, kwamba mke mmoja anaitwa fulani, na mwingine fulani, na mwingine fulani. Muundo wa utendaji ulivyo ni kwamba Paroko anapata taarifa kutoka kwa kiongozi wa jumuiya anayotoka muumini. Kama hakupata hizo taarifa hawezi kuhisi. Unatakiwa useme wazi kwamba kiongozi wa jumuiya ya Komba alikuwa ana uhakika wa kuwapo kwa wake wengi ila hakumpa taarifa Paroko, au useme wazi Paroko alipewa taarifa hizo lakini akazipuuzia. Na wewe kama ulikuwa na taarifa hizo ukakaa kimya, lawama zinapaswa kuja kwako