Viongozi wa Juu wa CHADEMA kuongea na Wanahabari Novemba 25, 2020 Makao Makuu ya Chama, Kinondoni

swala siyo matamko tu, tunataka na hatua za kisheria dhidi ya tume, kama kweli uteuzi huo ni wa kughushi. Haiwekani nchi kuwa na taasisi kubwa kama na muhimu kuwa ya kughushi, hii inanipa mashaka kama ni kweli chadema hawakuandika barua kwenda Nec, uongozi wote uliotokana na matokeo yaliyotangazwa na tume ni ya kughushi na siyo kwa uhalali.
 
Hasara ambazo zingetokea iwapo CHADEMA haingeteua wabunge wa viti maalumu ni pamoja na hizi:
  • CCM, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake TANU, kingeendelea kuwa chama pekee (essentially) ndani ya bunge. Madhara yake makubwa ni kwamba hakungekuwepo mtu kama Mdee wa kuzungumzia ukweli ni upi na uwongo ni upi huku akiwa na kinga ya bunge.
  • CHADEMA kingekosa mahali pa kuzungumza huku kikiwa na kinga ya bunge. Watanzania hawana uhuru wa kutoa maoni yao nje ya bunge. Unamkumbuka yule kijana aliyesema “Rais kitu gani bwana?” na hilo likatosha ahukumiwe kifungo cha miezi sita? Ndani ya bunge kuna kinga, mbunge anaweza kusema, bungeni, bila kukamatwa na polisi. Sana sana anaweza kukandamizwa na Ndungai, lakini siyo kukamatwa polisi.
  • Wabunge walioteuliwa wangekosa fedha za mshahara wa mbunge. Huo umasikini ungewanyima nguvu kuendelea kupigana. Ubunge ni aina ya ajira pia.
  • CHADEMA kingeshindwa kusikika na hivyo kufifia. Kipindi hiki cha vyama kutofanya mikutano mbali na sehemu za wabunge na kipindi cha uchaguzi, chama kisichokuwa na wabunge lazima kififie sana.
Ni sahihi kwa CHADEMA kuteua wabunge kina mama. Hawangefanikisha lolote kwa kukaa tu nje. They will now fight from inside.

Wale ambao lengo ni kushambulia CHADEMA, wamepata pa kujishikiza kwenye jambo hili, na siyo kwamba wana principles. Principles gani wakati watu wenyewe ni wale wale wa Lumumba?

It's okay CHADEMA, Mdee na wenzako mkafanye kweli ndani ya mjengo. Anzeni kwa kupigia kelele katiba muflisi tuliyo nayo.
 
Ndugu zangu Watanzania, Jana Tanzania kwa mara nyingine tena tumeshtushwa Sana kushuhudia tukio la ghafla Sana ambalo hatukulitarajia kuwa lingetokea na hususani kwa wakati kama huu ambao bado wapo kwenye tafakuri kwa kilichotokea Oktoba 28 !!! Tukiwa bado kabisa hatuamini kilichotokea Oktoba hiyo 28 , Jana Watanzania tumebaki vinywa wazi pale tuliposhuhudia Waliokuwa Wanawake Makomandoo ambao Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ), kilikuwa kinawategemea Sana Katika kufikia Mabadiliko ya kweli kwenye Taifa hili, wakiapishwa na kuwa rasmi Wabunge!

Je, CHADEMA kwa Msingi huo, mnamaanisha kwamba Uchaguzi haukuwa na dosara na hivyo mnakubaliana moja kwa moja na Tume ya Uchaguzi ilitenda haki !? Sasa Malalamiko yenu mliyoyapeleka Umoja wa Mataifa na sasa tunataarifiwa kwamba tayari Kesi imefunguliwa katika Mahakama ya ICC The Huage, Je, Malalamiko yenu ni nini sasa !? Mbowe jitokeze ulipo haraka uzungumze na Watanzania kuhusiana na hili tukio lililotokea Jana hapo Dodoma!
 
Akijitokeza nistue.
 
Polepole na Mashinji wanasemaje?
 
Mbowe ni master plan atawamaliza hao malaya wa kisiasa
 
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji1787][emoji2][emoji1][emoji28]
 
Mkuu unamanisha wanachama wa chadema ni Malaya Hadi wanunulike?
 
Swala hapa ni uhalali wa wao kuwepo
Swala hapa ni uhalali wa kisheria kwa wao kuteuliwa na time siyo madhara kwa chadema
 
Watuache tuendelee kuijenga nchi yetu bwana. Wanataka kutwambia nini? Watu wamegana sehemu za kukimbilia. Kuna wengine wamekimbilia kenya, wengine ulaya na wengine Bungeni.
 
hakutakuwa na jipya,uchaguzi umekwisha,bunge limetimia
 
mbona kwa Membe hamkutulia mkajipanga??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…