Hasara ambazo zingetokea iwapo CHADEMA haingeteua wabunge wa viti maalumu ni pamoja na hizi:
- CCM, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake TANU, kingeendelea kuwa chama pekee (essentially) ndani ya bunge. Madhara yake makubwa ni kwamba hakungekuwepo mtu kama Mdee wa kuzungumzia ukweli ni upi na uwongo ni upi huku akiwa na kinga ya bunge.
- CHADEMA kingekosa mahali pa kuzungumza huku kikiwa na kinga ya bunge. Watanzania hawana uhuru wa kutoa maoni yao nje ya bunge. Unamkumbuka yule kijana aliyesema “Rais kitu gani bwana?” na hilo likatosha ahukumiwe kifungo cha miezi sita? Ndani ya bunge kuna kinga, mbunge anaweza kusema, bungeni, bila kukamatwa na polisi. Sana sana anaweza kukandamizwa na Ndungai, lakini siyo kukamatwa polisi.
- Wabunge walioteuliwa wangekosa fedha za mshahara wa mbunge. Huo umasikini ungewanyima nguvu kuendelea kupigana. Ubunge ni aina ya ajira pia.
- CHADEMA kingeshindwa kusikika na hivyo kufifia. Kipindi hiki cha vyama kutofanya mikutano mbali na sehemu za wabunge na kipindi cha uchaguzi, chama kisichokuwa na wabunge lazima kififie sana.
Ni sahihi kwa CHADEMA kuteua wabunge kina mama. Hawangefanikisha lolote kwa kukaa tu nje. They will now fight from inside.
Wale ambao lengo ni kushambulia CHADEMA, wamepata pa kujishikiza kwenye jambo hili, na siyo kwamba wana principles. Principles gani wakati watu wenyewe ni wale wale wa Lumumba?
It's okay CHADEMA, Mdee na wenzako mkafanye kweli ndani ya mjengo. Anzeni kwa kupigia kelele katiba muflisi tuliyo nayo.