Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Ngoja tumsikie Nduguyo na Muongo, wanaweza kusema tunapotoshwa na ni umeme wa kileo sio unaoharibu mazingira na utasababisha nchi kuwa kama hong kong.
hapa kutakuwa na hela ndefu ilipigwa. Kama serikali ilikopa $240m, kwa mtaji wa $320m serikali ingekuwa na 75% ya hisa. kutakuwa na zaidi ya $80m kwenye huo mkopo hazikuwekezwa Songas.
 
Hamna imani hata na Rais Samia ambaye kesho anaenda kuwa mwenyekiti wenu??
Kwa kweli mimi binafsi sina uhakika.

JPM nilikua na uhakika. Yeye alikua na uwezo wa kusema yes hata kama amekosea ama no hata kama amekosea.

Wazungu wanasema he got balls, he got the cojones.
 
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).

Hatujawahi kupata mrejesho kutoka kwa Bw. Kilagi kuhusu Songas, ila serikali inamiliki kupitia TANESCO na TPDC.

Mkataba wa kuuza wa umeme wa Songas na TANESCO unaisha ama unategemea kuisha mwaka 2024. Songas imekua na harakati za kutaka kuongezewa mkataba pale mkataba uliopo utakapofika mwisho na kulikua na ugumu kidogo kwani serikali inategemea kua na umeme wa bei rahisi wa maji kutoka JNHPP wa Megawati 2115. Songas wamekua wakitumia ushawishi mkubwa waongezewe mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO.

Mimi binafsi sioni haja ya kuendelea na hawa mabeberu kwani kwa hali ya sasa bado tunajitosheleza, tuna megawati 1600 ikiwemo Songas ya megawati 185 na maximum demand ni megawati 1200 kama alivyosema Rais juzi. Hivyo hata tukiwaondoa Songas sasa hivi bado tunaweza kukidhi mahitaji yetu ya juu kabisa na kusiwepo na shida ya umeme.

Juzi nilimsikiliza mkurugenzi wa TPDC akiongea TBC, alikiri kua bei ya gesi iko juu sana hapa TANZANIA, kwa maana kua TANESCO inauziwa umeme kwa bei ya juu sana na hawa kina Songas na bado inatakiwa kuuzia Watanzania.

Kuna kinyerezi 1, 2, kinyerezi 2 extension, kinyerezi 3, Ubungo 1, Ubungo 2 zote za gesi na kuna mpango wa kujenga hadi kinyerezi 5 ya megawati 600, sasa Songas ya nini tena?

Ni wakati sasa Watanzania tujifunze, haya makampuni ya umeme hapa Tanzania ya binafsi yatatufirisi. Kulikua na Agreko, Symbion, IPTL, Songas na sijui itakuja ipi nyingine.

Ngoja tuone kama mama atawatolea nje hawa jamaa. Mwendazake alikua ametoa nje kabisa hiyo deal ya extension.

Mbona Magufuli hajawahi kusema kitu! Au wapigaji ni hao watangulizi wake wa CCM . Pesa ilienda kwenye kampuni au walikuwa njiani
 
Trust the process
"Viongozi wakuu wa kampuni ya Songas"..., ndio akina nani hao?

Hasa hao watatu waliopo kwenye picha, ni akina nani hao?

Haya mambo tuanze kuwa tunayafanya kwa uelewa, tusiwe tunalalamika tu kijumlajumla bila kujua tunacholalamikia!
 
Najiuliza swali gumu; kwa sasa yupo mtu serikalini mwenye ubavu wa kusema NO baada ya JPM kutangulia mbele za haki?

Vv
Magufuli alisimamia huu mkataba tangu ameingia ikulu songas wanaiuzia umeme TANESCO mpaka amekufa ameacha hivohivo mbona mnajifanya hamnazo?
 
Leo ubalozi wa Marekani umetoa taarifa kua viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme wa gesi ya Songas imekutana na Balozi wa Marekani na kufanya mazungumzo kuhusu nishati ya Tanzania.

Historia ya Songas Tanzania inajulikana ilivyojawa na utata na nakumbuka mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Kilagi alipoingia madarakani alisema anafuatilia umiliki wa kampuni ya Songas kwani umejawa na utata, wabunge huko nyuma wameizungumzia sana Songas. Kwa haraka ni kua mtaji uliotumika kuanzisha Songas ni Dollar Million 320, serikali ya Tanzania ikakopa Dollar Milioni 240 kuwekeza lakini ajabu yeye ndie mmiliki mdogo(minority shareholder).

Hatujawahi kupata mrejesho kutoka kwa Bw. Kilagi kuhusu Songas, ila serikali inamiliki kupitia TANESCO na TPDC.

Mkataba wa kuuza wa umeme wa Songas na TANESCO unaisha ama unategemea kuisha mwaka 2024. Songas imekua na harakati za kutaka kuongezewa mkataba pale mkataba uliopo utakapofika mwisho na kulikua na ugumu kidogo kwani serikali inategemea kua na umeme wa bei rahisi wa maji kutoka JNHPP wa Megawati 2115. Songas wamekua wakitumia ushawishi mkubwa waongezewe mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO.

Mimi binafsi sioni haja ya kuendelea na hawa mabeberu kwani kwa hali ya sasa bado tunajitosheleza, tuna megawati 1600 ikiwemo Songas ya megawati 185 na maximum demand ni megawati 1200 kama alivyosema Rais juzi. Hivyo hata tukiwaondoa Songas sasa hivi bado tunaweza kukidhi mahitaji yetu ya juu kabisa na kusiwepo na shida ya umeme.

Juzi nilimsikiliza mkurugenzi wa TPDC akiongea TBC, alikiri kua bei ya gesi iko juu sana hapa TANZANIA, kwa maana kua TANESCO inauziwa umeme kwa bei ya juu sana na hawa kina Songas na bado inatakiwa kuuzia Watanzania.

Kuna kinyerezi 1, 2, kinyerezi 2 extension, kinyerezi 3, Ubungo 1, Ubungo 2 zote za gesi na kuna mpango wa kujenga hadi kinyerezi 5 ya megawati 600, sasa Songas ya nini tena?

Ni wakati sasa Watanzania tujifunze, haya makampuni ya umeme hapa Tanzania ya binafsi yatatufirisi. Kulikua na Agreko, Symbion, IPTL, Songas na sijui itakuja ipi nyingine.

Ngoja tuone kama mama atawatolea nje hawa jamaa. Mwendazake alikua ametoa nje kabisa hiyo deal ya extension.

Awamu ya pili imeanza
 
Kwa taarifa ni kwamba Songas walianza toka mwaka 2019 mazungumzo ya kutaka waongezewe mkataba na kuahidi kua mkataba mpya watapunguza bei ya umeme wanaoiuzia Tanesco lakini mwendazake alikua amekataa hilo wazo la kuongeza mkataba.

Walikua wanatumia ushawishi wa hali ya juu sana kuongezewa mkataba ila hawakua na uhakika maana mwenzake alikua meshagoma.

Nadhani baada ya JPM kufariki jamaa walishangilia maana sina hakika kama watakataliwa. Tusubiri tuone.

Mikataba ya take or pay ukishaingia mkataba, utumie hicho mlichokubaliana ama usitumie unalipa.

Mashirika yetu haya yanatengeneza hasara kwa sababu ya wanasiasa wasio waaminifu. TANESCO imetwishwa madeni, ATCL imetwishwa madeni, TTCL imetwishwa madeni na yote yanatokana na mikataba mibovu.
Waziri ana PHD kwenye Mining Law
 
"Viongozi wakuu wa kampuni ya Songas"..., ndio akina nani hao?

Hasa hao watatu waliopo kwenye picha, ni akina nani hao?

Haya mambo tuanze kuwa tunayafanya kwa uelewa, tusiwe tunalalamika tu kijumlajumla bila kujua tunacholalamikia!
Hiyo picha ipo wapi

  • Nigel Whittaker
    Managing Director
  • Anael Samuel
    Managing Director
  • Sebastian Kastuli
    Chief Financial Officer and Officer
  • Agatha Keenja
    Personnel Manager
 
Na ndio kisa cha marekani kununa kwani walikua wanadai makampuni yao yanafanyiwa figisu kumbe wanalazimisha kutupora.

Haya jamaa hawana utu kabisa yaani, nchi yetu ndio kwanza tunajitutumua tufike mahali wao wanalazimisha kutuuzia umeme wa mabei makubwa.

Shame on USA.
 
Mashirika na makampuni yote ya umma yaorodheshwe kwenye soko letu la hisa ili wananchi na taasisi binafsi wanunue hisa. Serikali kumiliki hisa za makampuni na mashirika ya umma kwa asilimia mia, kunatoa mwanya kwa viongozi kufanya maamuzi bila shinikizo na kutengeneza ufisadi.
 
Sana, sawa na zile ziara za Kikwete kumtembelea Magufuli Ikulu mwanzoni mwa utawala wa awamu ya 5. Sijui alikuwa anajaribu kushawishi nini!
Tukitaka kuwajua wote wanaohujumu taifa letu tutawajua.

Na mwanzo wa vita ni kutambua adui ni nani.

Na mbinu ya kwanza kivita ni kuwafichua, kila mtu ajue.

Uwezo tunao, na Nia tunayo.
 
Magufuli alisimamia huu mkataba tangu ameingia ikulu songas wanaiuzia umeme TANESCO mpaka amekufa ameacha hivohivo mbona mnajifanya hamnazo?
Kama utakumbuka ishu ya IPTL, magufuli alikuta mkataba wa IPTL, hakuona busara kuuvunja ule mkataba kwani muda wake wa kuisha ulikua umebakiza miezi kadhaa, muda ulipoisha akawanyima IPTL leseni, IPTL ikafa kifo cha mende. Hakuna kuvunja mkataba na hakuna gharama zozote za kuvunja mkataba.

Songas pia idea ni hiyo, kuuvunja ule mkataba utaleta shida nyingi na bado Songas ilikua inategemewa kwani miradi kama Kinyerezi imekamilika sio miaka mingi iliyopita, nadhani kuanzia 2017.

Leseni ya Songas inaisha muda wake 2024, mwaka huo huo tutakua na umeme wa Megawati 2115 kutoka JNHPP, hivyo tutakua na sababu zote za kuwanyima leseni Songas na hakuna wa kutudai.

Hiyo ndio akili.
 
Mashirika na makampuni yote ya umma yaorodheshwe kwenye soko letu la hisa ili wananchi na taasisi binafsi wanunue hisa. Serikali kumiliki hisa za makampuni na mashirika ya umma kwa asilimia mia, kunatoa mwanya kwa viongozi kufanya maamuzi bila shinikizo na kutengeneza ufisadi.
Lifanyie kazi hili wazo lieleweke vizuri mkuu, naona kuna matumaini katika wazo lako.

Tusichotaka kamwe, ni hawa viongozi kuendelea kutuhujumu.
 
Back
Top Bottom