Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Kwa kweli sijui, lakini inawezekana, maana na visomo vyao nje ya nchi , na interaction yao ina saidia kupata hizi kazi
Watanzania wenzetu wanatu blackmail mkuu.

Siku zote walikuwa wapi?
 
sasa kama mkataba unaelekea kuisha, balozi ama ubalozi wa marekani nchini utawasaidiaje?

Au ndio ataweza kushauri na kushawishi* serikali yetu dhidi ya hili dili?

anyway, kwa kuwa sijui kilichojiri kwa undani, ngoja niendelee kutega sikio zaidi...

* - ushawishi wa marekani ni hatari sana
 
Magufuri tutakukumbuka daima!
Katika hili tukio Mungu wetu hakuona shida za watanzania?
Kazi ya Mungu haina makosa
 
Hivi mitambo ya ﹰSymbion aliyo kazindua ﹰﹰJK ﹰna ﹰObama uku wakipiga danadana mpira ilikuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuri tutakukumbuka daima!
Kwa nini hukuzikwa naye? Idadi ya wapumbavu kama wewe labda ingepungua Tanzania. Magufuli atakumbukwa kama anavyokumbukwa Adolf Hitler na si kwa mema bali kwa uovu wake dhidi ya Watanzania.
Katika hili tukio Mungu wetu hakuona shida za watanzania?
Eti Mungu wenu hakuona! Huyo ni mungu feki. Kwa Mungu wa kweli hii ni kufuru na kwa hii kauli, mbona shetani lazima atakuwa anashangilia? Mungu wa kweli aliona mateso waliyopitia Watanzania na akatuokoa na yule muovu.
Kazi ya Mungu haina makosa
Hapa tunakubaliana kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Mwanga ukipiga hodi giza hutokomea bila kuaga na kwa miaka mitano taifa la Tanzania lilikuwa kwenye giza totoro lakini Mungu akafanya kweli kwa kutuletea mwanga!
 
Mama alishasema yeye na Mwendazake ni kitu kimoja. Kwa hiyo mawazo ya aliyemtangulia yanashabihiana na yake kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwa nini watu wana mashaka? Wanataka Mama aseme nini sasa?
Ndio, amesema sote tumesikia mkuu. Tunasubiri kuona. Kusikia tumesikia, imebaki kuona, au sio?
 
Ni kweli halieleweki kwa wengi lakini lipo kwenye mfumo, utekelezaji wake umeshindikana kwa awamu zote pamoja na kuwepo kwenye mipango na kuwahi kujadiliwa bungeni sababu kuu ikiwa kuwa inagusa maslahi ya watu wachache. Anahitajika mtu mwingine mwenye utashi na uthubutu wa kuhakikisha kuwa kinachoamuliwa huko Bungeni kinatekelezwa.

Mali za nchi hii ni zetu sote. Serikiali inamiliki hisa za makampuni na mashirika ya umma kwa asilimia mia, viongozi tuliowachagua ndio wasimamizi wa hizi mali na kwa mamlaka tuliyowapa wanaweza kuamua kuyaendesha kwa kuegemea pale yalipo maslahi yao. Sehemu pekee ya mwananchi wa kawaida kuweza kuhoji juu ya mwenendo wa hizi mali ni kushiriki moja kwa moja kwenye umiliki wa hizi mali kupitia soko la hisa.
Katika wabunge wote waliomo bungeni (hata wale ambao walipata ubunge wa chee), hakuna wanaoweza kulisemea hili jambo likaeleweka kwa watu wengi?
Akina Zitto (at least yule niliyemjua zamani); pamoja na kwamba hayumo Bungeni hawezi akalisemea watu wakamsikiliza na pengine kumuunga mkono?

Njia yoyote inayotafuta wigo wa kuyakingia uhujumu haya mashirika inafaa kuungwa mkono.

Tafadhali mkuu GwaB, kwa nini usilitafakari vizuri wazo hili halafu ulianzishie mada hapa watu tulijadili kwa kina?
 
..tatizo mkataba unaisha 2024.

..na 2025 ccm inahitaji fedha za kampeni za uchaguzi mkuu.

..hapo ni lazima waweke rehani rasilimali za watanzania.

..tusubiri tuone itakuwaje.

cc tindo
Una hoja mkuu.

Nakuelewa. Unaweza kua sahihi kabisa kwa mtazamo wako.

Kwa CCM inapokua kwenye chaguzi ama kuchagua kupotea kwenye siasa na kupoteza uongozi ama kuuza rasilimali za Taifa watachagua kuuza rasilimali za Taifa.
 
Katika wabunge wote waliomo bungeni (hata wale ambao walipata ubunge wa chee), hakuna wanaoweza kulisemea hili jambo likaeleweka kwa watu wengi?
Akina Zitto (at least yule niliyemjua zamani); pamoja na kwamba hayumo Bungeni hawezi akalisemea watu wakamsikiliza na pengine kumuunga mkono?

Njia yoyote inayotafuta wigo wa kuyakingia uhujumu haya mashirika inafaa kuungwa mkono.

Tafadhali mkuu GwaB, kwa nini usilitafakari vizuri wazo hili halafu ulianzishie mada hapa watu tulijadili kwa kina?
Nitaanzisha uzi wake muda si mrefu ili lijadiliwe humu.

Pamoja na kuanzisha mada nagundua kuwa wapo wengi tu wasiolielewa hili na viongozi wetu wanaolijua hawaweki msukumo kwa kuwa hakuna anaedai.

Nawashauri ndugu zangu wanaokerwa na hali hii waanze kujielimisha kuhusu utendaji wa soko letu la hisa. Hii itawafungua macho watu wengi na kuongeza wigo wa usimamizi wa mali zetu za umma.
 
Hivi mitambo ya ﹰSymbion aliyo kazindua ﹰﹰJK ﹰna ﹰObama uku wakipiga danadana mpira ilikuwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
sijui kiundani sana ila Obama alijua ataweza kuleta ushawishi wa hali ya juu east africa (si nyumbani). alipokuja na kutembelea nchi hizi mbili jirani na kusepa, nadhani alisikitishwa sana na utendaji wa viongozi wao. na zile ripoti za takukuru zilivyo leak ndio akaona bure kabisa!

namshangaa na nakumuangalia sana jamaa na familia yake wanavyo hangaika! kosa alilofanya generali mmoja miaka fulani iliyopita huku 'wakijua' ni kazalendo wakati ni ka 'snitch' ka hali ya juu (na huku Mossad angefaa) nadhani walijuta sana!
 
Obama ahitimisha ziara yake nchini Tanzania, azindua mradi mkubwa wa umeme

Imechapishwa: 02/07/2013 - 16:37

Rais wa Marekani Barck Obama amehitimisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania, kama sehemu ya ziara yake ya siku saba Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika Kusini na hatimaye Tanzania.

MATANGAZO YA KIBIASHARA

Katika ziara yake nchini Tanzania Barack Obama alipata nafasi ya kuzungumza na mwenyeji wake kwenye mazungumzo ya faragha ikulu jijini Dar es Salaam jana na kisha kuzungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari ambao walipata nafasi ya kumuuliza maswali kabla ya kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ya Tanzania majira ya jioni.

Aidha mapema hii leo kabla ya kuelekea katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko Ubungo jijini Dar es Salaam, rais Obama na mtangulizi wake Gorge W Bush walifika kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kuweka mashada ya maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya watu waliouwawa katika shambulizi la kigaidi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998.

Ifuatayo ni Ripoti maalum iliyoandaliwa na Victor Robert Wile ambaye alikuwa akifuatilia ziara ya rais huyo wa Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hoja mkuu.

Nakuelewa. Unaweza kua sahihi kabisa kwa mtazamo wako.

Kwa CCM inapokua kwenye chaguzi ama kuchagua kupotea kwenye siasa na kupoteza uongozi ama kuuza rasilimali za Taifa watachagua kuuza rasilimali za Taifa.

..kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe.

..lakini mimi nadhani ccm wana uchu uliopitiliza wa madaraka.

..pia sidhani kama wana uchungu na nchi hii, wako kwa manufaa ya chama chao zaidi.

..tunapofika kipindi cha uchaguzi wanachofanya ccm siyo kampeni bali ni kufuru ya kisiasa na usaliti kwa watanzania.

..chukulia mfano kampeni za 2020. Hivi kulikuwa na ulazima wa wasanii wote nchi nzima kuipigia kampeni ccm?

..au vyombo vyote vikuu vya habari kutangaza kampeni za ccm huku vyama vingine vikiwa gizani?

..au kuwatumikisha viongozi wa dini kwa namna ya kinafiki ambayo inawapunguzia heshima zao?

..au kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mahakama, kisiasa.

..sidhani kama kuna wakati wowote ktk uhai wake ccm imekuwa ktk tishio kiasi cha kulazimika kuuza utu wao, kuchukua fedha chafu, au kuweka rehani rasilimali za nchi.
 
sidhani kama kuna wakati wowote ktk uhai wake ccm imekuwa ktk tishio kiasi cha kulazimika kuuza utu wao, kuchukua fedha chafu, au kuweka rehani rasilimali za nchi.
Na haya ndiyo yanayoiondolea CCM heshima, kama chama kilichoasisiwa kusimamia maslahi ya nchi na wananchi wake wote.
 
Najiuliza swali gumu; kwa sasa yupo mtu serikalini mwenye ubavu wa kusema NO baada ya JPM kutangulia mbele za haki?

Vv
Kwenye mambo magumu kama haya yanayolikabili Taifa hili,hapa ndipo ninapoukumbuka umuhimu wa hayati JPM.
Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom