Viongozi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas wakutana na Balozi wa Marekani

Ngoja tumsikie Nduguyo na Muongo, wanaweza kusema tunapotoshwa na ni umeme wa kileo sio unaoharibu mazingira na utasababisha nchi kuwa kama hong kong.
hapa kutakuwa na hela ndefu ilipigwa. Kama serikali ilikopa $240m, kwa mtaji wa $320m serikali ingekuwa na 75% ya hisa. kutakuwa na zaidi ya $80m kwenye huo mkopo hazikuwekezwa Songas.
 
Hamna imani hata na Rais Samia ambaye kesho anaenda kuwa mwenyekiti wenu??
Kwa kweli mimi binafsi sina uhakika.

JPM nilikua na uhakika. Yeye alikua na uwezo wa kusema yes hata kama amekosea ama no hata kama amekosea.

Wazungu wanasema he got balls, he got the cojones.
 

Mbona Magufuli hajawahi kusema kitu! Au wapigaji ni hao watangulizi wake wa CCM . Pesa ilienda kwenye kampuni au walikuwa njiani
 
Trust the process
"Viongozi wakuu wa kampuni ya Songas"..., ndio akina nani hao?

Hasa hao watatu waliopo kwenye picha, ni akina nani hao?

Haya mambo tuanze kuwa tunayafanya kwa uelewa, tusiwe tunalalamika tu kijumlajumla bila kujua tunacholalamikia!
 
Najiuliza swali gumu; kwa sasa yupo mtu serikalini mwenye ubavu wa kusema NO baada ya JPM kutangulia mbele za haki?

Vv
Magufuli alisimamia huu mkataba tangu ameingia ikulu songas wanaiuzia umeme TANESCO mpaka amekufa ameacha hivohivo mbona mnajifanya hamnazo?
 
Awamu ya pili imeanza
 
Waziri ana PHD kwenye Mining Law
 
"Viongozi wakuu wa kampuni ya Songas"..., ndio akina nani hao?

Hasa hao watatu waliopo kwenye picha, ni akina nani hao?

Haya mambo tuanze kuwa tunayafanya kwa uelewa, tusiwe tunalalamika tu kijumlajumla bila kujua tunacholalamikia!
Hiyo picha ipo wapi


  • Nigel Whittaker
    Managing Director
  • Anael Samuel
    Managing Director
  • Sebastian Kastuli
    Chief Financial Officer and Officer
  • Agatha Keenja
    Personnel Manager
 
Na ndio kisa cha marekani kununa kwani walikua wanadai makampuni yao yanafanyiwa figisu kumbe wanalazimisha kutupora.

Haya jamaa hawana utu kabisa yaani, nchi yetu ndio kwanza tunajitutumua tufike mahali wao wanalazimisha kutuuzia umeme wa mabei makubwa.

Shame on USA.
 
Mashirika na makampuni yote ya umma yaorodheshwe kwenye soko letu la hisa ili wananchi na taasisi binafsi wanunue hisa. Serikali kumiliki hisa za makampuni na mashirika ya umma kwa asilimia mia, kunatoa mwanya kwa viongozi kufanya maamuzi bila shinikizo na kutengeneza ufisadi.
 
Sana, sawa na zile ziara za Kikwete kumtembelea Magufuli Ikulu mwanzoni mwa utawala wa awamu ya 5. Sijui alikuwa anajaribu kushawishi nini!
Tukitaka kuwajua wote wanaohujumu taifa letu tutawajua.

Na mwanzo wa vita ni kutambua adui ni nani.

Na mbinu ya kwanza kivita ni kuwafichua, kila mtu ajue.

Uwezo tunao, na Nia tunayo.
 
Magufuli alisimamia huu mkataba tangu ameingia ikulu songas wanaiuzia umeme TANESCO mpaka amekufa ameacha hivohivo mbona mnajifanya hamnazo?
Kama utakumbuka ishu ya IPTL, magufuli alikuta mkataba wa IPTL, hakuona busara kuuvunja ule mkataba kwani muda wake wa kuisha ulikua umebakiza miezi kadhaa, muda ulipoisha akawanyima IPTL leseni, IPTL ikafa kifo cha mende. Hakuna kuvunja mkataba na hakuna gharama zozote za kuvunja mkataba.

Songas pia idea ni hiyo, kuuvunja ule mkataba utaleta shida nyingi na bado Songas ilikua inategemewa kwani miradi kama Kinyerezi imekamilika sio miaka mingi iliyopita, nadhani kuanzia 2017.

Leseni ya Songas inaisha muda wake 2024, mwaka huo huo tutakua na umeme wa Megawati 2115 kutoka JNHPP, hivyo tutakua na sababu zote za kuwanyima leseni Songas na hakuna wa kutudai.

Hiyo ndio akili.
 
Lifanyie kazi hili wazo lieleweke vizuri mkuu, naona kuna matumaini katika wazo lako.

Tusichotaka kamwe, ni hawa viongozi kuendelea kutuhujumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…