Viongozi wa machinga Dar wakumbana na vurugu wakiwapanga wenzao

Viongozi wa machinga Dar wakumbana na vurugu wakiwapanga wenzao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Viongozi wa Machinga Dar es Salaam walijitolea kuwapaga wamachinga wenzao wa Msimbazi, Kariakoo ili kutii amri ya Serikali ya kutofanya biashara maeneo yasiyo rasmi.

Baadhi ya machinga wameonesha upinzani kiasi cha kuzua vurugu ambapo polisi walilazimika kuingilia kati ili kuwaokoa viongozi hao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewapongeza viongozi wa machinga kujitolea kufanya zoezi hilo la kuwapanga wenzao.

Zaidi, soma;

“Leo Jumanne kumetokea tafrani katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo wakati Viongozi wa Wamachinga katika jitihada za kuunga mkono Serikali kuwapanga vizuri Wamachinga walifanya wenyewe oparesheni ya kuwatoa Watu walioziba njia za wapita kwa miguu”

“Nawapongeza sana Viongozi wa Wamachinga Dar es salaam kwa kazi nzuri waliyoifanya leo na niwaambie pamoja na changamoto iliyojitokeza baadhi yao wachache kuwapinga, wameonesha ni Viongozi wakomavu ambao wanaelewa nia nzuri ya Serikali”-Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla.

Hao machinga inatakiwa wafahamu tu kwa sasa serikali haiwezi kurudi nyuma tena , kwani wanafanya vitimbi vingi kutafuta huruma kuwa wanaonewa, ili zoezi lisitishwe, usije shangaa wakaanda hata bonge ya tukio la kutisha ili tu kutafuta huruma!!ZAMU HII AFE KIPA, AFE BEKI, LAZIMA TU GOLI LIINGIEEE!!mlivumiliwa sana na kujiona ndio wenye haki za kufanya mlitakalo kwenye mitaa.
 
kwa mfano na wewe uamke asubuhi ukute tu umefukuzwa kazi
 
Kama kuna mgogoro kati ya machinga na viongozi wao inaonesha hilo agizo la mkuu wa mkoa halikukubaliwa na wote, mwanzo mgumu, naamini baada ya muda machinga wataizoea hii hali mpya iliyowakuta na kuacha maisha yaendelee.
Sio rahic kukubali watu woteeee
 
“Leo Jumanne kumetokea tafrani katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo wakati Viongozi wa Wamachinga katika jitihada za kuunga mkono Serikali kuwapanga vizuri Wamachinga walifanya wenyewe oparesheni ya kuwatoa Watu walioziba njia za wapita kwa miguu”

“Nawapongeza sana Viongozi wa Wamachinga Dar es salaam kwa kazi nzuri waliyoifanya leo na niwaambie pamoja na changamoto iliyojitokeza baadhi yao wachache kuwapinga, wameonesha ni Viongozi wakomavu ambao wanaelewa nia nzuri ya Serikali”-Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla.
View attachment 1979812
Hata kwenye familia hamuwezi kukubaliana wote kwenye jambo!

Hakuna kurudi nyuma lazima wapangwe na wawe kwenye utaratibu ili baadae wawe walipa kodi!

Hatuwezi kuishi bila utaratibu
 
Tatizo la wamachinga matokeo ya siasa chafu za maccm yenyewe. Nakumbuka yule jini aliwahi kuwakemea wakuu wa mikoa waliokuwa na nia ya kuwaondoa maeneo yasiyo rasmi (enzi hizo walikuwa wachache).

Maccm yale yale yamegeuka na sasa yanatatua tatizo walilolitengeneza wao wenyewe
 
Back
Top Bottom