Ninafuatilia kwenye runinga tukio la kuuaga mwili wa aliyekuwa mtumishi wa serikali na mwanadiplomasia mbobezi ndg Bernard Membe.
Ninawiwa kuwaasa viongozi wetu wa serikali, bunge na mahakama mliopewa dhamana ya kulitumikia taifa letu, kulitazama jeneza la aliyekuwa kiongozi kama ninyi mlivyo na kujitafakari matendo yenu na mwisho wa maisha yenu hapa duniani. Wengi wenu mmekuwa hamuwatendei haki watanzania,n Kwa namna mnavyoikiuka waziwazi katiba ya nchi ambayo mliapa kuilinda.
Hakuna haki ktk mahakama,kutotimiza wajibu wenu kuwaletea wananchi nafuu ktk maisha,kulindana kwenye ufisadi,polisi kutotenda haki kwa wananchi. Ni mengi yakusikitisha na kuhuzunisha yanayoendelea ktk mihimili ya nchi hii. Itoshe kusema tu kitafakarini kifo kupitia msiba wa Membe, na muangalie mienendo yenu ktk kulitumikia nchi na wananchi. Hukumu ya haki ipo mbele yenu na kifo ni muda wowote.