Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa azitaka wizara, idara na taasisi za serikali kuhakikisha zinapitisha viongozi wake katika mafunzo yanayoandaliwa na kutolewa na Taasisi ya UONGOZI. Waziri Mchengerwa aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo mapema hivi leo.
“Taasisi zote hapa nchini ambazo zina watumishi wa umma wajipange, watenge bajeti zao kuhakikisha kwamba wanapita kwenye taasisi hii ili tuweze kupikana zaidi. Na wale ambao tunaamini wanaweza kutusaidia, tuwatumie.
Tunao Wakuu wa Mikoa ambao wana uzoefu zaidi, waiteni na kuwatumia ili kuendelea kutoa elimu. Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni vijana na pengine wanadhani wao wakishateuliwa ndiyo wameshamaliza, kwamba hakuna mamlaka ya kuwachunguza na kuwafuatilia, ni lazima tuzingatie sana,” alisema Waziri huyo.
Aidha, Waziri Mchengerwa alitoa msisitizo kuhusu suala la utendaji kazi kwa wizara, idara na taasisi zote za serikali; ikiwemo kuhakikisha kwamba stahiki za watumishi wa umma zinapatikana kwa wakati na kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha kwamba watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu waweze kuthibitishwa katika nafasi hizo endapo wana sifa zinazostahili, na kuhakikisha maadili na taratibu za utumishi wa umma zinazingatiwa ili kuleta ufanisi katika kazi na huduma zitolewazo kwa wananchi.