Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Sahihi kabisa. Kitakachoamua kama hii mechi itakuja kuchezwa ama la ni baada ya hizi timu mbili kucheza mechi kadhaa zinazofuata za ligi na ama kupoteza au kushinda mechi hizo. Hapo ndiyo utashangaa Simba ama Yanga anarudi kulazimisha na kudai hii mechi ifanyike maana ndiyo inaweza kufufua matumaini yao ya bingwa.
Ila mmoja akipoteza pwenti za kutosha katika mechi hizi kiasi cha kwamba mechi hii ya derby haiwezi kuleta utofauti, basi jua mechi haitakuja kuchezwa tena.
Hilo la mechi kutokuchezwa kabisa sidhani, itashangaza likitokea.
Kutegemeana na kukamilika kwa uchunguzi wa hayo matukio yaliyoletwa na afisa usalama wa michezo ambayo hayajawekwa wazi, ni either:
1. Mechi kurudiwa
2. Simba kunyang'anywa point 3 na faini au vyote
3. Yanga kunyang'anywa point 3 na faini au vyote
Kinyume na hapo bodi ya ligi itakuwa imejiacha utupu mno.