Viongozi wa wizara na taasisi za Wizara ya Mambo ya Ndani mkeka wenu unakuja kama siyo leo usiku basi wiki hii

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Malalamiko mengi yamepelekwa kwa Waziri wa Mambo ya ndani na viongozi wake. Maeneo yanayolalamikiwa zaidi ni
1. Utekaji
2. Wananchi kunyimwa dhamana na kushikiliwa kinyume cha sheria
3. Viongozi wa chama cha mapinduzi kusafirisha wahamiaji haramu kwa mashangingi bila kuchukuliwa hatua
4. Vitambulisho vya NIDA kutotolewa kwa wakati na kukosekana kwa online application ya kuomba vitambulisho husika au kupata ujumbe wa sms kwamba kitambulisho kimetoka
5. Kupotea kwa watoto na mauaji ikiwemo ubakaji
6. Rushwa ya barabarani inayoombwa na trafic

Hata mambo yamechafua taswira ya nchi yetu. Naamini kuna jambo linakwenda kutokea katika wizara hiyo Muda siyo mrefu
 
Kila mtu amesha anza kujiona mtabiri ili apate credit wakati wote tunaona upepo unapo elekea
 
Wambura ni mhalifu namba moja, eidha awajibike AMA awajibishwe
 
Labda una id mbili lakini kama ni hii moja basi imani yangu ni haba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…