Viongozi wa Yanga mwacheni Azizi Ki aende tu

Viongozi wa Yanga mwacheni Azizi Ki aende tu

Naunga mkono hoja. Ni kweli ni mchezaji mzuri ila kwa ligi yetu mshahara wa USD 20,000 na signing Fee ya USD 500,000 ni kutengeza mpasuko wa Fei Toto.
 
Wamlete Chama ambae hana bei kali anaweza kukaribia Aziz ki kipindi wanajipanga
Hoja yako kuu ilikuwa nzuri kasoro hapa.
Hapa umeshauri kama mamluki vile!!
Yanga siyo Juve hatutaki kusajiri wazee, exception ipo kwa wazawa mfano wa Mkude na Abubhakar SureBoy.
 
Nawashauri viongozi wa Yanga, msiwe na pressure kutoka Kwa mashabiki wasiojua mpira mkaingia kwenye mtego wa kumpa Aziz ki pesa ndefu takriban 1.3 billion, mtakuwa mmejichanganya.

Azizi ki Kwa Sasa ana miaka 29 kwenye mpira umri huo jua limezama, unaweza kumbakiza kumbe ndo amefika kwenye peak/ kilele cha career yake.

Nawasihi Yanga muwe na msimamo wa kiwango cha mshahara na utamaduni wenu.

Ukimwongeza Azizi pesa ya usajili na mshahara wa million 80 Kwa mwezi, kila mchezaji akimaliza mkataba atataka alipwe kama Aziz, Ambapo itakuwa gharama kuendesha team.

Africa Kuna vipaji vingi zaidi ya Aziz na vinataka pesa ndefu.

Hakuna mchezaji asiyeizwa au kuachwa akiingia tofauti na uchumi wa club.

Man u walimuuza Ronaldo, Barcelona walimuuza Mesi, arsenal walimuuza Henry na van persie n.k na Bado team zilikomaa na utamaduni wao wakafanya vyema.

Ukimwongeza Azizi ki mkataba wa pacome, yao, mdathir, aucho, max, bacca, job illkiisha watataka mabilion kama ya Aziz.

Wasalam
Mkuu wewe si kuna mahali nimekusoma ukisema Aziz Ki yupo Yanga na hizo tetesi kuwa anaondoka ni za uongo?
 
Chama tena? Mpira wa Gamondi kila mtu ni mkabaji, mpira wa Gamondi kila mtu anatakiwa awe mwana riadha. Kama viongozi watafosi kumsajili Chama basi wajue kuwa wanamsajilia Gamondi mchezaji wa kumuweka benchi. Chama kwasasa kabakiza akili tu mpira ila umri ndio unaomkataa kwasasa hivyo kuna vitu vingi hawezi kufanya kwasasa. Nadhani uongozi wa Yanga warudi tena kiwandani wakachukue mashine nyingine. Kile kiwanda kinazalisha vifaa kila msimu, anatoka mtu anakuja mtu, Asec ni chuo cha kuzalisha mafundi wa mpira Africa.
Sijasikia vzri hpo kuhusu Chama
 
Bado nasimamia msimamo wangu Chama ni mzee hawezi kuwa mbadala wa Aziz Ki Ila anaweza kuwa nyongeza au squad player wakati wenye namba zao wakiwa nje kwa majeruhi au adhabu za kadi za njano na nyekundu.
 
Tukiwa bado tunamuhitaji na hajatuboa hawezi kwenda timu yeyote ile mpira maokoto mzee baba
 
Hoja yako kuu ilikuwa nzuri kasoro hapa.
Hapa umeshauri kama mamluki vile!!
Yanga siyo Juve hatutaki kusajiri wazee, exception ipo kwa wazawa mfano wa Mkude na Abubhakar SureBoy.
Kiko wapi?
 
Du kuna watu Wana macho ya mbali. 🤣🤣. Nasikia ameingia MJINI Kwa pupa clubing, mashangazi 😄😄😄
 
Kiko wapi?
Kama ulimaanisha kusajiliwa Chama naona muda umesimama na Mimi.
Chama mzee na anafaa kuwa nyingeza squad player.
Kama ulimaanisha kuhusu Aziz Ki Mimi nilimuunga mkono ngara23 kwa kusema hoja yake kuu ilikuwa nzuri na ndicho kinachotokea Sasa Aziz hafanyi vema.
 
Back
Top Bottom