Viongozi wa Yanga nawapa pongezi kwa kufanya mambo kimyakimya bila kuwajibu wanaowazodoa

Viongozi wa Yanga nawapa pongezi kwa kufanya mambo kimyakimya bila kuwajibu wanaowazodoa

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Hii kitu nimeipenda sana, viongozi wa yanga wamepata shutuma za Kila aina wiki hizi tatu, timu ya yanga imechambuliwa na Kila mchambuzi na maneno yake, kocha kafukuzwa na wachambuzi.

Lawama za Kila aina zimerushwa kwa yanga baada ya kupoteza mechi 2 dhidi ya Azam na Tabora united, lakini hakuna kiongozi yoyote wa Yanga aliyetoka kauli yoyote juu ya hayo yote!

Wamekaa kimya wakiendelea kuyafanyia kazi yale yote yanayotakiwa kufanyiwa kazi,
Wanafanya mipango yao kiuweledi na sio kupayukapayuka ovyo.

Tunajua Kuna wachambuzi wako kwenye payroll ya klabu Fulani wanajaribu kuchokonoa kujua kinachoendelea ili waupate cha kuandika kwenye mitandao yao lakini wamepigwa Pini hawajui chochote wamebaki kuwa watabiri kama waganga wa kienyeji, Leo wanapost hiki kesho wanaposti kile awaeleweki!

Viongozi wameamua kunyamaza kufanya tathmini ya kina kujua ni wapi waliteleza na ni wapi warekebishe baada ya hapo Kuna kitu kinatengenezwa na watu watafunga Tena midomo waanze habari za gsm anaharibu ligi!

Wakati huu wako kimya wanakenua na meno yote 32 yanaonekana lakini wakianza kupoteana utaanza kusikia zile KELELE zinaibuka Tena za gsm anaharibu ligi!

Viongozi chapeni kazi nafikiri mmeona wanafiki wengi kipindi hiki, wanataka mpoteane wafurahie kwa maana iyo akuna habari za GSM anaharibu ligi bali ni wivu unawasumbua mkirudi kuanza ligi msicheke na kima iwe ni mwendo wa kata funua mpaka mwisho!
 
😆😆😆😆😆
Free mind Freee ignorance!!!!
 
Hii kitu nimeipenda sana, viongozi wa yanga wamepata shutuma za Kila aina wiki hizi tatu, timu ya yanga imechambuliwa na Kila mchambuzi na maneno yake, kocha kafukuzwa na wachambuzi, lawama za Kila aina zimerushwa kwa yanga baada ya kupoteza mechi 2 dhidi ya Azam na Tabora united, lakini akuna kiongozi yoyote wa yanga aliyetoka kauli yoyote juu ya ayo yote!

Wamekaa kimya wakiendelea kuyafanyia kazi yale yote yanayotakiwa kufanyiwa kazi,
Wanafanya mipango yao kiuweledi na sio kupayukapayuka ovyo, tunajua Kuna wachambuzi wako kwenye payroll ya klabu Fulani wanajaribu kuchokonoa kujua kinachoendelea ili waupate cha kuandika kwenye mitandao yao lakini wamepigwa Pini awajui chochote wamebaki kuwa watabiri kama waganga wa kienyeji, Leo wanapost hiki kesho wanaposti kile awaeleweki!

Viongozi wameamua kunyamaza kufanya tathmini ya kina kujua ni wapi waliteleza na ni wapi warekebishe baada ya hapo Kuna kitu kinatengenezwa na watu watafunga Tena midomo waanze habari za gsm anaharibu ligi!
Wakati huu wako kimya wanakenua na meno yote 32 yanaonekana lakini wakianza kupoteana utaanza kusikia zile KELELE zinaibuka Tena za gsm anaharibu ligi!

Viongozi chapeni kazi nafikiri mmeona wanafiki wengi kipindi hiki, wanataka mpoteane wafurahie kwa maana iyo akuna habari za gsm anaharibu ligi bali ni wivu unawasumbua mkirudi kuanza ligi msicheke na kima iwe ni mwendo wa kata funua mpaka mwisho!
Hatua zipi hizo zilizochukuliwa?
 
Tuthibitishie kwa vitendo yanga atashinda mechi zote 20 zilizobakia na simba atafungwa mechi zote 20 zilizobakia acha porojo.

Msimu uliopita kwenye mechi 10 za mwanzo ulikuwa umeshinda mechi 9 alama 27, na magoli 30 ukifungwa mechi 1 tu.

Hadi sasa hivi umecheza mechi 10,umefungwa 2,umeshinda 8,alama 24,magoli 14 ya kufunga,4 ya kufungwa halafu unacheza mpira mbovu unafunga magoli ya offside, halafu unajamba jamba tu hapa ooh tutashinda tutashinda,shinda tuone acha kujinyea nyea.

Kwa akili yako fupi unadhani simba hii ndo simba ile mbovu ya wazee ambao hawawezi kukimbia,kukaba,kushambulia,hawana ari,morari wapo kama mazombi tu.

Hii simba ni bora 3 times compared to the last season so usitegemee simba itadondosha alama kirahisi na ukijichanganya ukafirimbwa ukizidiwa alama 4 au 5 inaweza ikaisha ivo ivo.

Acha kuishi kwa mazoea kuti la mazoea ndiyo linalomuangushaga mgema.
 
Back
Top Bottom