Viongozi wakifika kesho wataongea tu,lakini kwa sasa hakuna ufumbuzi kwa hii vita

Viongozi wakifika kesho wataongea tu,lakini kwa sasa hakuna ufumbuzi kwa hii vita

..mpaka wa Drc na nchi za Rwanda na Uganda ufungwe, na kati yao kuwe na demilitarized zone.
Umeandika kitu cha maana sana.
Dawa ya jipu ni kulitumbua tu.
Mpaka ufungwe, askari wa SADC waweke zone katikati hapo. Mchawi akiibuka apigwe hapo hapo.
 
Hoja muafaka kabisa. Banyamulenge waondolewe mpakani mwa Rwanda wapelekwe sehemu nyingine ndani ya Congo
Nyerere, wakimbizi wa sehemu hizo waliwekwa Kambi ya Mishamo, na wengine Katumba. Walivyo pewa uraia wamejikuta wapo Rukwa wengine Tabora n.k na kuna wakati alitaka kuwa peleka Mtwara, maana wakikaa hapo mpakani , Mchana wanakuwa wakimbizi wanakuja Bongo , jioni Wana rudi nchini mwao kama wapiganaji.
 
Binafsi naona suluhisho la hii vita ni
1. DRC akubali kukaa na waasi mega moja. Waasi woote maana kuna zaidi ya vikundi 100 vya waasi ...Hawa m23 ni most popular tu. Hii itasaidia kujua panapovuja. Kagame atakosa support.

2. DRC ikubali kuwapinga FDLR....watangaze kuwafukuza nchini kwao...Kagame atakosa sababu ya kwenda Congo.

3. Congo ijenge ukuta kuzizunguka Rwanda na Uganda....na kiwekwe kikosi katikati ya Rwanda na Congo

Rwanda ni jeuri....ana ego...kumbukeni pia Rwanda na Uganda ndiyo Marais Senior EAC na SADC wanajua mbinu zote....na kutakuwa na ile dharau ya hawa wanajua nini.....

Tshekedi humble yourself to save your country. Ongea na hao waCongomani ujue wanahitaji nini? La sivyo utaendelea kumpa upenyo Rwanda wa kutumia huo mwanya kukupiga.

Binafsi.

Lakini hapo kwenye point no.1.Nadhani ni kudhibiti chanzo cha nguvu ya hivyo vikundi. kuna mtu ambaye yuko nyuma yao anaye finance hizo harakati.huyo ndiyo mhimu kudhibitiwa.Maana hata unajiuliza silaha zinaingiaje nchini DRC.Huyo anaye finance hivyo vikundi ndiyo msemaji mwenyewe.hao wenyewe ukiwauliza hawana cha maana kwenye ufumbuzi.Halafu pia jeshi la DRC limechafuka kwa idadi kubwa ya mamluki.Kwa hiyo taarifa zinavuja mapema
 
Tusiweke matumaini makubwa kuhusu summit meeting ya kesho.

Jambo moja tunaweza kuridhika ni kwamba kwa kusikiliza ripoti nyingi tunaweza kuona kwamba wapo viongozi wa Jeshi la Kongo ambao sio waaminifu kwa nchi yao.

Tutapata suluhu labda katika huu mgogoro lakini siyo katika Mkutano wa kesho.

Wanajadiliana hawa wataalamu experts in so- called International Relations.
Ndio hao hao experts waliotuletea Ukrainian War na Syrian War na Gaza War.

Nashindwa kuelewa.
Kama Banyamulenge ni raia wa North Kivu kwa nini watake kuiteka Kongo yote?

Hii ni attempt to hypnotize the whole country.

Soma Pia: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo
Viongozi wameshindwa kufanya zoom meeting!
Hadi wafike Dar ili Barabara zifungwe na kuongeza gharama za nchi zao!
Trump punguza misaada!
 
Namna pekee ni kuwaonyesha wamejumuishwa kwa serikali hata kama nchi ni maskini.

Tusisahau pia Makampuni makubwa na nchi kubwa zimetumia huu mgogoro kama njia ya kujineemesha....vikundi zaidi ya 100 nani anavifadhili? Vyote vinafandhiliwa na Rwanda? Staking kuliamini hili
Hivyo vikundi vinaibuka tu vyenyewe wala hakuna anayevifadhiri, ni kama ilivyokuwa somalia, vita nayo ni biashara kama biashara nyingine yaani kama ilivyo siasa bila hela/mtaji hautoboi.
 
Lakini hapo kwenye point no.1.Nadhani ni kudhibiti chanzo cha nguvu ya hivyo vikundi. kuna mtu ambaye yuko nyuma yao anaye finance hizo harakati.huyo ndiyo mhimu kudhibitiwa.Maana hata unajiuliza silaha zinaingiaje nchini DRC.Huyo anaye finance hivyo vikundi ndiyo msemaji mwenyewe.hao wenyewe ukiwauliza hawana cha maana kwenye ufumbuzi.Halafu pia jeshi la DRC limechafuka kwa idadi kubwa ya mamluki.Kwa hiyo taarifa zinavuja mapema
Banyamulenge walikuwepo toka wakati WA Mabuto, lakini hawakuwa na nguvu kama sasa baada ya Kagame aliye aanzia Updf, na sasa RPF , kuanzisha hivyo vikundi vya M23 na AdF
 
Binafsi naona suluhisho la hii vita ni
1. DRC akubali kukaa na waasi mega moja. Waasi woote maana kuna zaidi ya vikundi 100 vya waasi ...Hawa m23 ni most popular tu. Hii itasaidia kujua panapovuja. Kagame atakosa support.

2. DRC ikubali kuwapinga FDLR....watangaze kuwafukuza nchini kwao...Kagame atakosa sababu ya kwenda Congo.

3. Congo ijenge ukuta kuzizunguka Rwanda na Uganda....na kiwekwe kikosi katikati ya Rwanda na Congo

Rwanda ni jeuri....ana ego...kumbukeni pia Rwanda na Uganda ndiyo Marais Senior EAC na SADC wanajua mbinu zote....na kutakuwa na ile dharau ya hawa wanajua nini.....

Tshekedi humble yourself to save your country. Ongea na hao waCongomani ujue wanahitaji nini? La sivyo utaendelea kumpa upenyo Rwanda wa kutumia huo mwanya kukupiga.

Binafsi.
Hao m23 watakuwa wanasikiliza kagame anasema Nini na sio maamuzi ya kikao
 
..DRC hawajapewa nafasi ya kuongoza na kujenga nchi yao.

..pia ujiulize mbona mipaka ya Drc na nchi kama South Sudan, Zambia, Angola, na Tanzania, haina matatizo?
Mipaka hiyo ulioitaja haina matatizo na DRC kwasababu haiwabagui makabila yanayoishi mipakani kuwa sio raia wa nchi zao!
Kwanza kabisa DRC lazima iwatambue M23 kama raia halali wa Congo na kuwaunganisha katika serikali ya DRC!!
Hayo yakifanyika Rwanda haitakuwa na sababu ya kuwasaidia ndugu zao huko DRC kwasababu hawatakuwa wanateswa na kutengwa na serikali yao!
As long as M23 wanabaguliwa na Kinsasha vita Hivi havitakoma😂😂
 
Congo igawanywe tu iweze kutawalika vizuri
 
Unaweza kuvi orodhesha hivyo vikundi. Na kwanini ADF iwe Congo na sio Uganda , na kupewa Jina la waislamu WA itikadi Kali , pili kwa nini Rwanda itumie kisingizio cha FDRL , wakati wao wenyewe asili Yao ilikuwa kutoka updf. Na zaidi ya hapo wao RPF ni zao la kutotekeleza mkataba wa Amani wa Arusha. Ambao. Ungewawezesha kuishi kwa pamoja na hao FDRL. Na sasa hao RPF wamepata Madaraka , wamewafungia vioo wa Hutu Ndani ya Rwanda na nje ya Rwanda . Na kutumia kisingizio hicho kuingia DRC Kwa kisingizio cha FDRL na hao Banyamulenge . Kwa hiyo Nia Yao ni kuwamaliza "wahutu" kadiri inavyowezekana , na kujiimarisha zaidi Kwa kuwa tumia Banyamulenge na kuchukua Ardhi ya Kongo Kivu ya kaskazini na baadae kuiingia Burundi na kuwa maliza au kuwa punguza Wahutu Burundi. Ndio wajichukulie Kivu ya kusini.

Ikibidi Sana hao Banyamulenge wahamishwe upande wa pili wa mpaka na wasi kae mpakani na Rwanda au Burundi. Na idaddi Yao hihesabiwe na vizazi vyao vianze kuwa vinaandikishwa huko.
Seriously niorodheshe vikundi Mia moja.....hao wanaoitwa Mai Mai wenyewe wanamgawanyiko wa makundi.

Angalia baadhi hapa chini. DRC ukiamka ukataka kuanzisha kakindi chako unaanzisha tu.
 
Attachments

  • Screenshot_20250208_065746_Chrome.jpg
    Screenshot_20250208_065746_Chrome.jpg
    153.9 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250208_065739_Chrome.jpg
    Screenshot_20250208_065739_Chrome.jpg
    126.3 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250208_065733_Chrome.jpg
    Screenshot_20250208_065733_Chrome.jpg
    134.4 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250208_065715_Chrome.jpg
    Screenshot_20250208_065715_Chrome.jpg
    153 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250208_065704_Chrome.jpg
    Screenshot_20250208_065704_Chrome.jpg
    100.6 KB · Views: 1
Tusiweke matumaini makubwa kuhusu summit meeting ya kesho.

Jambo moja tunaweza kuridhika ni kwamba kwa kusikiliza ripoti nyingi tunaweza kuona kwamba wapo viongozi wa Jeshi la Kongo ambao sio waaminifu kwa nchi yao.

Tutapata suluhu labda katika huu mgogoro lakini siyo katika Mkutano wa kesho.

Wanajadiliana hawa wataalamu experts in so- called International Relations.
Ndio hao hao experts waliotuletea Ukrainian War na Syrian War na Gaza War.

Nashindwa kuelewa.
Kama Banyamulenge ni raia wa North Kivu kwa nini watake kuiteka Kongo yote?

Hii ni attempt to hypnotize the whole country.

Soma Pia: Rais Samia kuwa mwenyeji wa mkutano wa marais wa nchi za SADC na EAC kujadili Mgogoro wa DR Congo
Issue ni kuwa west backers hawataki influence ya China kwenye rasilimali za Kongo period.Tshisekedi hakulijua hilo mapema.Hakuna cha banyamulenge sijui issue ya tutsis n hutus walaaa.Issue ni cobalt and other vital minerals available in eastern Congo.Hii ni vita ya superpowers na wanaoumia na watakaoendelea kuumia ni Congolese.Mkutano wa leo ni kujaribu kumlainisha Tshisekedi abadili upande chap kama anataka at least Kivu ipoe lakini kuhusu issue na mipango yake ya kujaribu kuleta umilki wa rasilimali za nchi kwa Serikali ya Kongo hilo asahau.Wote hao wanasiasa watakaokutana nae leo wao walishakubali big corporations za magharibi zichote rasilimali za nchi zao vyovyote zitakavyo.Tshisekedi hawez kuwazuia m23(backing by Rwanda backing by the west) hata kama nchi zooote za SADC na EA zitapeleka majeshi yao yoooote huko KIVU hawatafua dafu.Ni ukweli mchungu lakini ndio UKWELI HUO
 
Congo igawanywe tu iweze kutawalika vizuri
Sidhani kama suala ni Congo yenyewe.....Kipindi cha Mobutu Congo haikuwa na amani 100 lakini haikuwa hivi. Suala lilianza pale ilipopokea wakimbizi wa Kimbari.
 
Seriously niorodheshe vikundi Mia moja.....hao wanaoitwa Mai Mai wenyewe wanamgawanyiko wa makundi.

Angalia baadhi hapa chini. DRC ukiamka ukataka kuanzisha kakindi chako unaanzisha tu.
Lakini hatuvisiki kubugudhi wananchi, zaidi ya hivi viwili vya nji jirani, na ndio maana haya matatizo tunaona ni ya kupikwa
 
Lakini hatuvisiki kubugudhi wananchi, zaidi ya hivi viwili vya nji jirani, na ndio maana haya matatizo tunaona ni ya kupikwa
Vina bughudhi sema haupati habari....
 
Ile vita haijakaribia kuisha. Bado inaendelea.
Kwa hiyo ushauri wangu kwa combatants ni kwamba,in order to minimize collateral damage,yaani ili kupunguza madhara kwa raia,watumie risasi badala ya kutumia multiple rocket launchers.
Nilikuwa naitazama Ile multiple rocket launcher. Nimehesabu 39 shells.
This is my macabre advice for them.
They should hunt the enemy with rifles.
Kwa sababu already the ICC is becoming restless.
 
Back
Top Bottom