Viongozi wanaofaa na wasiofaa kuwa Marais mbeleni

Mtu yeyote anayefikiri kwamba Gwajima anafaa kuongoza watu ni mtu mwenye akili ndogo sana.
 
Polepole tangu akiwa kwenye tume ya mabadiliko ya katiba alikuwa na dhamira ya dhati ya mabadiliko,na ndio maana akaenda ccm ili akakitekeleze akiwa ndani ya system.
Ukiwa nje ya system ni ngumu kuyafanya yale alokusudia,na anaonekana mtu mwenye mikakati mizuri na URAISI unamfaa
 
Liambie Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na huyu Samia, uchaguzi uitishwe fasta, Majaliwa apambane na Lissu. Kidume apewe kombe.
 
Nape Nnauye - Ana kinyongo, kila anachofanya anahitaji malipo... (HAFAI).

January Makamba - Anajiona bora kuliko wengine, mpenda sifa, urafiki kwake ni bora kuliko maslahi ya uma, haonekani kuwa mzalendo! - (HAFAI).

Zitto Kabwe - Fisadi anayetumia akili, mafisadi humtumia kwenye deals zao na wasipomtumia ndo hujitokeza na kujifanya anatetea Watanzania, huyu anaweza uza nchi kisirisiri bila watu kustuka. -(HAFAI).

Heri James, Ally Happy, Jaffo- Hawa wote hutanguliza sifa kwenye utendaji wao na si uzalendo. -(HAWAFAI).

Bashiru Ally Kakurwa - Mzalendo, mchapakazi, anayetanguliza maslahi ya uma kwenye kazi zake. Habagui watu kwa vyama vyao wala dini na ndo maana alibariki wapinzani kupewa vyeo na serikali.
Sio mnafiki ndo maana alimchana live Magufuli kuwa hawezi ongezewa muda.
Hana kinyongo na anaheshimu mamlaka ya juu yake siku zote. -(ANAFAA).

Tundu Lisu - Wakili msomi na jasiri. Haogopi chochote zaidi ya sheria na siku zote amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunapata katiba mpya. Mtetezi wa wanyonge na amewahi fanya hivyo huko mara kwa wanyonge waliokuwa wakinyanyaswa. - (ANAFAA)

Prof Adolf Mkenda - Huyu ni mchapakazi, mwenye msimamo na asiye na mihemko. -( ANAFAA).
 
Umejitahidi ila kwa Lissu hapana atatuuza kwa Amsterdam,halafu anashobokea wazungu hawezi kulinda Mali za nchi,Ana kinyongo kisichoisha mfano kuisema vibaya maiti ya Mwendazake hata kabla ya kuzikwa.

Hajafanya kitu chochote jimboni kwake Cha kuonyesha anaweza.

Uanaharakati tu anaweza,nchi haihitaji mwanaharakati mwingine maana huyu aliyepo ni mwanaharakati kila siku 50/50.
 
Na siku ikitokea hicho KILIO,basi wa kulaumiwa ni nyinyi wapinzani kwa kushindwa kwenu kuandaa watu makini kwa zaidi ya miongo miwili.
Mnazidi kudumaa siku hadi siku.
Naomba tu niweke kumbukumbu sawa kwa faida ya baadae. Mkuu mimi siyo mpinzani. Ni Mtanzania tu Mzalendo na mpenda haki.

Sina kadi ya chama chochote! Ingawa siwezi kukataa, nina tamani sana kuona siku moja Tanzania ikitawaliwa na watu tofauti kabisa na wale ccm ambao kiukweli binafsi nimewachoka! Tangu uhuru 1961, ni TANU na mtoto wake CCM pekee!! Inachosha aisee.
 
Mimi ninaye comment sina chama lakini naamini huu upinzani hasa wa chadema ni genge la wahuni
 
Yaani hata Gwajima na polepole eti nao wanafaa. Hawa hawafai hata kuwa mabalozi wa nyumba kumi wala viranja mashuleni. Hopeless and useless no comparison so to speak.
 
Haihitaji akili nyingi kumbaini LISU hafai,hoja zake nyingi zimejikita kwenye utegemezi au kuwaona wazungu ndio msaada pekee kwa taifa letu(HAFAI)

Ila mkuu umenifurahisha ulivyowachambua hao wengine,yaani umegonga mulemule
 
Mimi ninaye comment sina chama lakini naamini huu upinzani hasa wa chadema ni genge la wahuni
Hivi mtu kama MBATIA anapataje kugombea nafasi ya uraisi? Si ndo huyu alisema eti baada ya wiki mbili korona itaipiga sana tanzania! wapinzani walichojaliwa ni kuliombea taifa mabaya tu basi
 
Yaani hata Gwajima na polepole eti nao wanafaa. Hawa hawafai hata kuwa mabalozi wa nyumba kumi wala viranja mashuleni. Hopeless and useless no comparison so to speak.
Wanayoyafanya na kupigania kwa taifa hili huyajui mkuu,we huyawezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…