Pre GE2025 Viongozi wanasema ni haki yenu kikatiba kujiandikisha kupiga kura hao hao wanasema kuandama ni uchochezi na uvunjifu wa amani!

Pre GE2025 Viongozi wanasema ni haki yenu kikatiba kujiandikisha kupiga kura hao hao wanasema kuandama ni uchochezi na uvunjifu wa amani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,132
Reaction score
5,508
Kuna wimbi kubwa sana la watanzania ambao wameupuuza huu uchaguzi wa serikali za mitaa na Mimi nikiwepo. Niwapongeze kwa kuchukua maamuzi yao kikatiba na kibinafsi kufanya maamuzi bila bugudha. Hii ndiyo sehemu pekee mtanzania anayo maamuzi binafsi bila mtutu wa polisi, vitisho vya viongozi wala kutekwa. Katiba imempa mwananchi uwanda mpana sana katika kufanya maamuzi yahusuyo mustakabali wa nchi yake lakini viongozi huwaamulia wanancho ni sehemu gani haswa wanapasea kuwa active na sehemu gani wanapasea kuvunga, hii sio sawa

Wananchi tunajua imma tujiandishe au tusijiandishe kupitia nukuu za viongozi wa CCM na polisi tukifanya hivyo ni kupoteza muda na rasilimali nguvu.

Wananchi tumeamua kuwaachia mfanye mnachokiona kinafaa lakini msitupangie kuhusu kujiandikisha. Tutafanya tunachojisikia uchaguzi sio muhimu kwetu na hautatuletea ugali mezani
 
Mtu anapiga kura yake, anakua na mashaka kama haki haitotendeka anataka kukaa chini ya mti asubiri aone matokeo anakatazwa
Bado safari ndefu
 
Mtu anapiga kura yake, anakua na mashaka kama haki haitotendeka anataka kukaa chini ya mti asubiri aone matokeo anakatazwa
Bado safari ndefu
Hii ndo nafasi ya kugoma haswa na najua wanajua hatuwapendi ila wadilazimishe kubadili taswira waishi waishivyo nasi kwa namna yety
 
Back
Top Bottom