Kwanza mimi nilishangaa serikali hii ilishindwa hata kumpa nafasi Rasmi kwenye ratiba aliyekuwa waziri wake Mkuu yaani Ndugu Sumaye nafasi ya kuongea machache juu ya Marehemu raisi Mkapa, naona kama ni uchoyo fulani wa baadhi ya watu kuhodhi msiba wa marehemu.
Hata wastaafu nao hawakuwekwa rasmi kwenye ratiba ili kumzungumzia mwenzao, uchoyo wa namna gani huu. Eti ni mpaka Magufuli alipojisikia ndo akawastukiza!
Nakumbuka mwaka 1999 kwenye kifo cha Mwalimu, pale uwanja wa Taifa mzee Mwinyi aliwekwa kwenye ratiba ya kumzungumzia mwalimu, mstaafu mwenzie. Lakini cha ajabu safari hii Ratiba yote ilikuwa centred juu ya Magufuli tu!