A
Anonymous
Guest
Mimi ni mfanyabiashara ambaye nimefanikiwa sana lakini wapo baadhi ya ndugu zangu ambao ni watumishi wa umma katika taasisi mbalimbali.
Malalamiko ya ndugu zangu kuhusu namna ambayo viongozi wao wa taasisi wanavyowafanyia yanafanana karibu kila taasisi.
Viongozi wanafanyia kazi habari za umbeya na unaweza kuta mtu anakuchukia kwa habari za kusikia kabla hata hajakuhoji. Na mbaya zaidi ni kwamba katika taasisi mbalimbali huo unaoitwa uchawa umeshamiri kupita kiasi.
Wafanyakazi wanatafuta kiki kwa viongozi na mara tu wanapojua kwamba kiongozi wao anapenda habari za udaku basi wao wanazipeleka hata kama si za kweli ili kufaidika na kile wanachokita.
KItendo cha kufanyia kazi habari za umbeya kinadhihirisha wazi kwamba viongozi wengi wa taasisi hawahitaji kuwa kwenye nafasi walizo nazo. Kitendo cha kulishwa maneno na kuyakubali inathibitisha wazi kwamba kiongozi husika hana akili ya kuweza kufikiri yeye mwenyewe.
Je, tunaweza kuwa na maendeleo kwenye taasisi zetu kwa kuwa na watu ambao hata akili ya kufikiri mambo madogo hawana?
Tunaomba kamati za uteuzi ziwe macho kwenye swala hili kwa sababu trend ya sasa hivi ya dunia inahitaji watu makini kwenye kila eneo la ujenzi wa serikali. Nchi haiwezi kuendelea kwa majungu na umbeya katika taasisi zetu