SoC03 Viongozi wetu wanafanya kazi kwa weledi uliotukuka, tatizo ni sisi!

Stories of Change - 2023 Competition

Black Opal

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2023
Posts
233
Reaction score
298
Nawashangaa wanaopiga kelele; viongozi wetu wabadhirifu, wala rushwa, wanaingia mikataba isiyo ya maana kama enzi za ukoloni za kubadilisha dhahabu na vipande vya jiwe na kadhalika, tunawalaumu bure tu, kuwatwisha msalaba usiowahusu. Hivyo ndivyo walivyokuwa toka wakiwa wanaomba ridhaa ya kuongoza kwetu, na hivyo ndivyo wanavyoendelea kuwa mpaka sasa, cha ajabu ni nini hapo? Kipi hatukukijua hapo kabla mpaka tuanze kushangaa sasa wakati wakiwa wanatenda?

Wawakilishi ambao baadae wanakuja kuchakuguliwa kuwa wakuu katika viota nchini mbalimbali pamoja na Kiranja Mkuu wanatoka miongoni mwetu, tunakua nao na kuishi nao mitaani mpaka kufikia kushika nyadhifa mbalimbali, tunajua kama ni wezi, wala rushwa wakubwa wasio na maana, wasioweza kulinda hata kipande cha mkate, eti leo tunawapa funguo walinde almasi yetu! Mbali na kujua yote hayo kwanini tunarudia tena na tena makosa haya? Yaani tunajua huyu mtu ni mla nyama za watu halafu kila uchwao tunampa watoto wetu atulelee tukitegemea watakakuwa salama, wewe ulisikia wapi?

Tena msinijie na jibu la “Hakuna mbadala wake”, kama tunaona kati ya waliokuwepo hakuna mwenye uwezo, kwanini tupitishe wabovu wakati tuna uwezo wa kusimamisha chaguzi ili waletwe wagombea wenye uwezo ndio mchakato uanze? Sisi ndio serikali na sisi ndio tunachagua wenye kushika vijiti kukimbia badala yetu, sisi tukisema wakimbiaji wa sasa hamna kitu, mapafu yao hayawezi kufanikisha hata kupiga hatua tano, hatuna timu ya kuipeleka kwenye shindano kuu ni nani mwingine wa kusema hapana?

Inashangaza sana, kipindi cha kutia vema kwenye vile vikaratasi sandukuni ni sisi ambao tunapokea michuzi kwa ahadi ya kuwapa kura mabaradhuli hao, lakini pia ni sisi sisi ambao tunapokea vibunda kuhakikisha tunafumbia macho wasiofaa wapate kula chakula tunachokitafuta kwa jasho wakati tunajua dhahiri kesho watoto wetu wakilia njaa hakutakuwa na wakutusaidia.

Ni sisi tunaogeuza shingo pembeni wakati wenzetu wa upande wa pili wakifanyiwa figusu ili wasiweze kusimamia haki za wagombea wao na wa kwetu aonekane amepita ‘bila kupingwa’, lakini pia ni sisi tunaozibwa midomo na vipisi vya makaratasi kutangaza uongo na ukweli kuuweka kando. Ikifika muda wa kutenda wanafanya kama tunavyowajua, wala hakuna jipya, tena safari hii wakiwa wameungana, nguvu zimeongezeka, yule anampigia panga huyu, na huyu akihakikisha hakuna panapovuja tupate la kutufaidisha.

Kinachostaajabisha zaidi ni kwamba, hawa hawa tuliowapa vijiti kwa moyo mkunjufu tukiona wameleta mambo yaanza kutuchoma eti tunaanza kupiga kelele, na hiki ndio tunachofanya pekee, KUPIGA KELELE. Na kelele hizi hazina lengo la kuleta mabadiliko au kuwawajibisha viongozi hao, ni kutembea tu upepo, kulivalia njuga kama vile tunamaanisha, tukishachoka tunalibwaga tukisubiria lingine. Tumewaamini, tunawapenda, hawawezi kufanya baya, ni kwa maslahi yetu, hao tunaendelea kutembea kama vile mwiba uliotuchoma mguuni hautuumizi na wala damu haitoki!

Hili ndio imekuwa mtindo wetu uliozoeleka, wataleta kitu kibovu wakujua fika tutapiga kelele tu ya kuvalia jambo kishabiki na tukichoka tutaliacha tusubirie jingine. Jambo hili pia limetengeza mwenendo wa kupitisha mambo maovu, ambapo wakitaka tu jambo lao lipite wanaachia ‘connection’ kama vijana wa mjini wanayosema, wanakuwa wamemaliza kazi, wanachota hela huku sisi tunabishana mkono ule ni wake au wa baunsa! Hatujiongezi kujua zaidi ya tulichosikia na wala hatutaki kujua tunaumia vipi, kuonekana tunapiga kelele ni muhimu zaidi kuliko hasa kujua mzizi wa tatizo ni nini na vipi tunang’oa mzizi huo ili tusije kuwa na matunda yenye sumu.

Hii inafanya hata wale wachache wanaofanya utafiti na uchambuzi wa kina mpaka mambo yakaeleweka wakazidiwa na sisi wapumbavu, hata wakijaribu kutuosha tongotongo zilizoziba macho na kutuweka kwenye mwangaza wanaonekana wabaya, waso na maana wanaotakia mabaya nchi yetu! Wakipaza sauti kutuelimisha na majina tunawapachika; “Vimbelembele”, “Wanafiki waso Wazalendo,” “Wanafanyia kazi Mabeberu”, na kubwa zaidi ni hili “Wamelambishwa Asali!” Mbaya zaidi ni wale waliotupa vipande vya kanga na miche ya sabuni wakitia neno, bendera sie haooo, tunafata upepo wenye harufu iliyooza kwa nderemo na vifijo, meli yetu wenyewe tunaitoboa kuruhusu maji yaingie, tunazama huku tunajiona!

Tabu kwa wachache hawa wanaoweka maisha yao hatarini kila siku kwa ajili yetu sisi wajinga tuliofunga macho haziishii hapo; mbali na wenye vijiti kuwawekea kauzibe mambo yao yaharibike, jeshi letu nalo linaenda kuongeza msumari wa moto kwenye kidonda! Tunashindwa kuwategemea tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha, lakini hata nyinyi pia mlioapa kutulinda kwa jasho na damu, nanyi vipande vya dhahabu vinawapumbaza mnakuwa kama misukule walotolewa akili kutenda kama hawana vichwa!

Tutapumilia wapi, nani atatukomboa kama nanyi mnachafua mikono yenu na damu kupoteza hata hawa wachache wanaopigana kila leo kwa imani kuwa tutazinduka kwenye usingizi huu mzito tuliolala? Mlitakiwa kuwashika mkono, gizani kutuondoa, lakini ni kinyume chake, kesi ya mwizi unampelekea jambazi ukitegema kuku wako bandani sasa wataanza kuongezeka, matokeo yake wanapikwa, unaishia kupewa mchuzi ukiambiwa nyama na mifupa zimevuja kwenye tundu! Tumekwisha!

Waandishi wa Habari nao wamekuwa kundi jingine linalochangia kutuangamiza badala ya kutuokoa. Kwa pesa ndogo tu na kujali matumbo yao wamekuwa wapotoshaji wakubwa wa mambo yanayotokea nchini, wanasahau kwamba leo wanafurahi na pengine mifuko yao inatuna lakini kesho mtoto wake na ndugu zake watalipia dhambi zao.

Ikiwa umempa fundi kazi akushonee nguo au akutengenezee kabati halafu fundi yule akala hela na kazi ikarudi mbovu, utampa tena akufanyie kazi nyingine? Kwanza utafanya vurumai arudishe hela nusu na utakuwa kiongozi wa kuwaambia wengine wasiende kwa fundi yule mbovu! Sasa inakuaje hufanyi kitu chochote mafundi hawa wanapoharibu nchi yetu na unaendelea tena na tena kuwapa kazi nyingine? Kwanini hupati uchungu kwa hawa wanaoharibu Tanzania hii moja tuliyonayo? Tunasubiri pakuche ndio tutafute shuka?

Tuwajibike, mafundi hawa tunaowapa kazi kuanzia fundi mkuu mpaka mfagizi wa ofisi tunawamudu, wakiharibu kazi ya kwanza hakuna haja ya kuwapa ya pili na ya tatu, kwanza hakuna haja ya kusubiri mpaka kazi iishe wakati uona nusu ya alichofanya ni sawa na sifuri wakati una machaguo mengi ya fundi wazuri wanaoweza kukamilisha kazi hiyo kwa weledi.

Kama ambavyo tunawasimamia kidete mafundi wetu ndivyo hivyo tusimame imara kwa viongozi tuliowapa dhamana kutuongoza, tuache kuwa makasuku, tuwe wa kwanza kukemea rushwa, kuchagua viongozi wenye sifa, kuhakikisha kuna uwazi kila hatua kwenye miradi inayofanyika, kusimama imara kwenye sheria mbovu zinazokandamiza uhuru wetu na kukwamisha maendeleo, lakini pia tuwalinde wale wachache wanaotoa maisha yao kupigania haki, tujufunze, tusikilize na tuungane kuisimamia na kuijenga Tanzania yetu isibaki tu kuwa ndoto tunayoota. Inawezekana, ikiwa tu utawajibika.
 
Upvote 5
Wazee chuma cha pili hicho, karibuni kwa mjadala na maoni
 
Nawashangaa wanaopiga kelele; vingozi wetu wabadhirifu, wala rushwa, wanaingia mikataba isiyo ya maana kama enzi za ukoloni za kubadilisha dhahabu na vipande vya jiwe na kadhalika, tunawalaumu bure tu, kuwatwisha msalaba usiowahusu. Hivyo ndivyo walivyokuwa toka wakiwa wanaomba ridhaa ya kuongoza kwetu, na hivyo ndivyo wanavyoendelea kuwa mpaka sasa, cha ajabu ni nini hapo? Kipi hatukukijua hapo kabla mpaka tuanze kushangaa sasa wakati wakiwa wanatenda?

Kama ambavyo tunawasimamia kidete mafundi wetu ndivyo hivyo tusimame imara kwa viongozi tuliowapa dhamana kutuongoza, tuache kuwa makasuku, tuwe wa kwanza kukemea rushwa, kuchagua viongozi wenye sifa, kuhakikisha kuna uwazi kila hatua kwenye miradi inayofanyika, kusimama imara kwenye sheria mbovu zinazokandamiza uhuru wetu na kukwamisha maendeleo, lakini pia tuwalinde wale wachache wanaotoa maisha yao kupigania haki, tujufunze, tusikilize na tuungane kuisimamia na kuijenga Tanzania yetu isibaki tu kuwa ndoto tunayoota. Inawezekana, ikiwa tu utawajib wanaiba kura na kujipatia madaraka, wala hakuna anaye wapa kura zetu, karibu kupiga kura yako pia hapa SoC03 - Umuhimu wa kamera za ulinzi (cctv camera) katika vyombo vya usafiri wa umma na vituo vyake hapa nchini
 
Nawashangaa wanaopiga kelele; viongozi wetu wabadhirifu, wala rushwa, wanaingia mikataba isiyo ya maana kama enzi za ukoloni za kubadilisha dhahabu na vipande vya jiwe na kadhalika, tunawalaumu bure tu, kuwatwisha msalaba usiowahusu. Hivyo ndivyo walivyokuwa toka wakiwa wanaomba ridhaa ya kuongoza kwetu, na hivyo ndivyo wanavyoendelea kuwa mpaka sasa, cha ajabu ni nini hapo? Kipi hatukukijua hapo kabla mpaka tuanze kushangaa sasa wakati wakiwa wanatenda?

Wawakilishi ambao baadae wanakuja kuchakuguliwa kuwa wakuu katika viota nchini mbalimbali pamoja na Kiranja Mkuu wanatoka miongoni mwetu, tunakua nao na kuishi nao mitaani mpaka kufikia kushika nyadhifa mbalimbali, tunajua kama ni wezi, wala rushwa wakubwa wasio na maana, wasioweza kulinda hata kipande cha mkate, eti leo tunawapa funguo walinde almasi yetu! Mbali na kujua yote hayo kwanini tunarudia tena na tena makosa haya? Yaani tunajua huyu mtu ni mla nyama za watu halafu kila uchwao tunampa watoto wetu atulelee tukitegemea watakakuwa salama, wewe ulisikia wapi?

Tena msinijie na jibu la “Hakuna mbadala wake”, kama tunaona kati ya waliokuwepo hakuna mwenye uwezo, kwanini tupitishe wabovu wakati tuna uwezo wa kusimamisha chaguzi ili waletwe wagombea wenye uwezo ndio mchakato uanze? Sisi ndio serikali na sisi ndio tunachagua wenye kushika vijiti kukimbia badala yetu, sisi tukisema wakimbiaji wa sasa hamna kitu, mapafu yao hayawezi kufanikisha hata kupiga hatua tano, hatuna timu ya kuipeleka kwenye shindano kuu ni nani mwingine wa kusema hapana?

Inashangaza sana, kipindi cha kutia vema kwenye vile vikaratasi sandukuni ni sisi ambao tunapokea michuzi kwa ahadi ya kuwapa kura mabaradhuli hao, lakini pia ni sisi sisi ambao tunapokea vibunda kuhakikisha tunafumbia macho wasiofaa wapate kula chakula tunachokitafuta kwa jasho wakati tunajua dhahiri kesho watoto wetu wakilia njaa hakutakuwa na wakutusaidia.

Ni sisi tunaogeuza shingo pembeni wakati wenzetu wa upande wa pili wakifanyiwa figusu ili wasiweze kusimamia haki za wagombea wao na wa kwetu aonekane amepita ‘bila kupingwa’, lakini pia ni sisi tunaozibwa midomo na vipisi vya makaratasi kutangaza uongo na ukweli kuuweka kando. Ikifika muda wa kutenda wanafanya kama tunavyowajua, wala hakuna jipya, tena safari hii wakiwa wameungana, nguvu zimeongezeka, yule anampigia panga huyu, na huyu akihakikisha hakuna panapovuja tupate la kutufaidisha.

Kinachostaajabisha zaidi ni kwamba, hawa hawa tuliowapa vijiti kwa moyo mkunjufu tukiona wameleta mambo yaanza kutuchoma eti tunaanza kupiga kelele, na hiki ndio tunachofanya pekee, KUPIGA KELELE. Na kelele hizi hazina lengo la kuleta mabadiliko au kuwawajibisha viongozi hao, ni kutembea tu upepo, kulivalia njuga kama vile tunamaanisha, tukishachoka tunalibwaga tukisubiria lingine. Tumewaamini, tunawapenda, hawawezi kufanya baya, ni kwa maslahi yetu, hao tunaendelea kutembea kama vile mwiba uliotuchoma mguuni hautuumizi na wala damu haitoki!

Hili ndio imekuwa mtindo wetu uliozoeleka, wataleta kitu kibovu wakujua fika tutapiga kelele tu ya kuvalia jambo kishabiki na tukichoka tutaliacha tusubirie jingine. Jambo hili pia limetengeza mwenendo wa kupitisha mambo maovu, ambapo wakitaka tu jambo lao lipite wanaachia ‘connection’ kama vijana wa mjini wanayosema, wanakuwa wamemaliza kazi, wanachota hela huku sisi tunabishana mkono ule ni wake au wa baunsa! Hatujiongezi kujua zaidi ya tulichosikia na wala hatutaki kujua tunaumia vipi, kuonekana tunapiga kelele ni muhimu zaidi kuliko hasa kujua mzizi wa tatizo ni nini na vipi tunang’oa mzizi huo ili tusije kuwa na matunda yenye sumu.

Hii inafanya hata wale wachache wanaofanya utafiti na uchambuzi wa kina mpaka mambo yakaeleweka wakazidiwa na sisi wapumbavu, hata wakijaribu kutuosha tongotongo zilizoziba macho na kutuweka kwenye mwangaza wanaonekana wabaya, waso na maana wanaotakia mabaya nchi yetu! Wakipaza sauti kutuelimisha na majina tunawapachika; “Vimbelembele”, “Wanafiki waso Wazalendo,” “Wanafanyia kazi Mabeberu”, na kubwa zaidi ni hili “Wamelambishwa Asali!” Mbaya zaidi ni wale waliotupa vipande vya kanga na miche ya sabuni wakitia neno, bendera sie haooo, tunafata upepo wenye harufu iliyooza kwa nderemo na vifijo, meli yetu wenyewe tunaitoboa kuruhusu maji yaingie, tunazama huku tunajiona!

Tabu kwa wachache hawa wanaoweka maisha yao hatarini kila siku kwa ajili yetu sisi wajinga tuliofunga macho haziishii hapo; mbali na wenye vijiti kuwawekea kauzibe mambo yao yaharibike, jeshi letu nalo linaenda kuongeza msumari wa moto kwenye kidonda! Tunashindwa kuwategemea tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha, lakini hata nyinyi pia mlioapa kutulinda kwa jasho na damu, nanyi vipande vya dhahabu vinawapumbaza mnakuwa kama misukule walotolewa akili kutenda kama hawana vichwa!

Tutapumilia wapi, nani atatukomboa kama nanyi mnachafua mikono yenu na damu kupoteza hata hawa wachache wanaopigana kila leo kwa imani kuwa tutazinduka kwenye usingizi huu mzito tuliolala? Mlitakiwa kuwashika mkono, gizani kutuondoa, lakini ni kinyume chake, kesi ya mwizi unampelekea jambazi ukitegema kuku wako bandani sasa wataanza kuongezeka, matokeo yake wanapikwa, unaishia kupewa mchuzi ukiambiwa nyama na mifupa zimevuja kwenye tundu! Tumekwisha!

Waandishi wa Habari nao wamekuwa kundi jingine linalochangia kutuangamiza badala ya kutuokoa. Kwa pesa ndogo tu na kujali matumbo yao wamekuwa wapotoshaji wakubwa wa mambo yanayotokea nchini, wanasahau kwamba leo wanafurahi na pengine mifuko yao inatuna lakini kesho mtoto wake na ndugu zake watalipia dhambi zao.

Ikiwa umempa fundi kazi akushonee nguo au akutengenezee kabati halafu fundi yule akala hela na kazi ikarudi mbovu, utampa tena akufanyie kazi nyingine? Kwanza utafanya vurumai arudishe hela nusu na utakuwa kiongozi wa kuwaambia wengine wasiende kwa fundi yule mbovu! Sasa inakuaje hufanyi kitu chochote mafundi hawa wanapoharibu nchi yetu na unaendelea tena na tena kuwapa kazi nyingine? Kwanini hupati uchungu kwa hawa wanaoharibu Tanzania hii moja tuliyonayo? Tunasubiri pakuche ndio tutafute shuka?

Tuwajibike, mafundi hawa tunaowapa kazi kuanzia fundi mkuu mpaka mfagizi wa ofisi tunawamudu, wakiharibu kazi ya kwanza hakuna haja ya kuwapa ya pili na ya tatu, kwanza hakuna haja ya kusubiri mpaka kazi iishe wakati uona nusu ya alichofanya ni sawa na sifuri wakati una machaguo mengi ya fundi wazuri wanaoweza kukamilisha kazi hiyo kwa weledi.

Kama ambavyo tunawasimamia kidete mafundi wetu ndivyo hivyo tusimame imara kwa viongozi tuliowapa dhamana kutuongoza, tuache kuwa makasuku, tuwe wa kwanza kukemea rushwa, kuchagua viongozi wenye sifa, kuhakikisha kuna uwazi kila hatua kwenye miradi inayofanyika, kusimama imara kwenye sheria mbovu zinazokandamiza uhuru wetu na kukwamisha maendeleo, lakini pia tuwalinde wale wachache wanaotoa maisha yao kupigania haki, tujufunze, tusikilize na tuungane kuisimamia na kuijenga Tanzania yetu isibaki tu kuwa ndoto tunayoota. Inawezekana, ikiwa tu utawajibika.
"Never underestimate the power of fools in a large number. They can elect one of their own to rule"
 
Back
Top Bottom