Viongozi wote wa Yanga na mdhamini GSM waondoke. Manji rudi utuokoe, mmetutia aibu

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Tumefungwa tena na kutolewa katika mashindano ya ligi ya mabingwa ya Afrika baada ya kufungwa tena 1 bila hivyo matokeo kuwa Rivers United 2 Yanga 0.

Viongozi wote wa Yanga inabidi wajiuzulu na mdhamini GSM aende zake,wanachama na wapenzi tumwombe shujaa wetu MANJI ARUDI KUTUDHAMINI.

Sababu kuu 2 zilizonifanya kuwataka viongozi na kamati ya utendaji kujiuzulu.

1)Tumeingia kwenye mashindano haya kupitia mtani wetu Simba SC.Tumeshindwa kwenye ligi na sasa tumeshindwa kwenye mashindano makubwa Africa champions league.

2)Kumpokea HAJI MANARA AMBAE HATA BABAKE MZAZI ALIMKATAA KUJIUNGA NA YANGA.HUYU KAJA KUTIBUA NA MUDA SI MREFU ATARUDI NYUMBANI KWAKE SIMBA.WAINGEREZA WANASEMA MISSION ACCOMPLISHED.Maana yake kazi aliyopewa na Mo sports club,samahani Simba SC Ameitimiza.

Mpira ni Biashara,Mpira ni SIASA.Ndio maana Rais wa Liberia George Weah alichaguliwa kuwa Rais wa Nchi ya Liberia.Huyu muda wote wa maisha yake alikuwa anacheza mpira,akaingia kwenye siasa akaukwaa urais.

NAHITIMISHA KWA KUWAAMBIA VIONGOZI WA YOUNG AFRICANS SC (YANGA),KAMATI YA UTENDAJI NA MDHAMINI MKUU GSM KUONDOKA.

Yanga ijengwe upya.Manji rudi nyumbani utuokoe.
 
Hiyo hoja yako namba 1 haina mashiko! Maana Yanga ilifika mpaka fainali kwenye Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo tayari ilikuwa na sifa ya kushiriki mashindano ya Kimataifa mwaka huu kutokana na kanuni za TFF.

Bado Yanga ilishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu! Nako ilibebwa na Simba? Yaani unajinasibu kuwa shabiki wa Yanga lakini una mawazo kama ya wale mbumbumbu wa Moo!!
 
Mm ni mwana yanga lini tuliwahi kufanya vema kwenye mashindano ya nje ya nchi

USSR
 
Hivi mnamsakama Manara kwani yeye ndiyo anacheza uwanjani? Tofautisha KAZI ya mhamasishaji na mchezaji.
 
Mawazo ya kipuuzi hayo!!huyo manara anahusika nini na uchezaji mpira wa timu?timu gani kila mwaka mnasajiri karibu timu nzima harafu utegemee miujiza ya haraka?kwa sasa timu sio mbaya , tatizo la Tz, tunapenda sana kuzikuza timu zetu wakati mpira bado sana!!wa kushindana na timu bora afrika, hata simba mwaka huu robo fainali hatafika.tutambiane humu humu ndani tu.
 
Hiyo hoja yako namba 1 haina mashiko! Maana Yanga ilifika mpaka fainali kwenye Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo tayari ilikuwa na sifa ya kushiriki mashindano ya Kimataifa mwaka huu kutokana na kanuni za TFF...
Hamna shabiki wa Yanga pale
 
Yanga ilikosa muda tu wa maandalizi na kosa jingine kubwa walipofanya makosa ya kuchelewa itc za baadhi ya wachezaji,na imani kama tukitulia timu wala sio mbaya
 
Hiyo hoja yako namba 1 haina mashiko! Maana Yanga ilifika mpaka fainali kwenye Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo tayari ilikuwa na sifa ya kushiriki mashindano ya Kimataifa mwaka huu kutokana na kanuni za TFF...
Yeah imebebwa kama si Simba wangeshiriki Kombe la Shirikisho kama Azam na Biashara na si Champions ligi mpaka mkajinasibu #TheReturnOfChampions
 
Mawazo ya kipuuzi hayo!!huyo manara anahusika nini na uchezaji mpira wa timu?timu gani kila mwaka mnasajiri karibu timu nzima harafu utegemee miujiza ya haraka?kwa sasa timu sio mbaya , tatizo la Tz, tunapenda sana kuzikuza timu zetu wakati mpira bado sana!!wa kushindana na timu bora afrika, hata simba mwaka huu robo fainali hatafika.tutambiane humu humu ndani tu.
Kwenye swala la vunja jenga vunja jenga ni wakina nani wanaohusika kama sio GSM na Msola? Mpira una misingi yake lakini tokea waingie GSM na vihela vyao wanachojua ni kuvunja mabenchi ya ufundi na wachezaji wapya kusajili kila msimu. Tukatae tukubali GSM na Msola wameshindwa kuleta mafanikio tokea wahusike kwenye timu
 
Hiyo hoja yako namba 1 haina mashiko! Maana Yanga ilifika mpaka fainali kwenye Kombe la Shirikisho la Azam, hivyo tayari ilikuwa na sifa ya kushiriki mashindano ya Kimataifa mwaka huu kutokana na kanuni za TFF.

Bado Yanga ilishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu! Nako ilibebwa na Simba? Yaani unajinasibu kuwa shabiki wa Yanga lakini una mawazo kama ya wale mbumbumbu wa Moo!!
Mkuu usipate shida, hakuna mwana Yanga wa namna hii
 
Tumefungwa tena na kutolewa katika mashindano ya ligi ya mabingwa ya Afrika baada ya kufungwa tena 1 bila hivyo matokeo kuwa Rivers United 2 Yanga 0.

Viongozi wote wa Yanga inabidi wajiuzulu na mdhamini GSM aende zake,wanachama na wapenzi tumwombe shujaa wetu MANJI ARUDI KUTUDHAMINI.

Sababu kuu 2 zilizonifanya kuwataka viongozi na kamati ya utendaji kujiuzulu.

1)Tumeingia kwenye mashindano haya kupitia mtani wetu Simba SC.Tumeshindwa kwenye ligi na sasa tumeshindwa kwenye mashindano makubwa Africa champions league.

2)Kumpokea HAJI MANARA AMBAE HATA BABAKE MZAZI ALIMKATAA KUJIUNGA NA YANGA.HUYU KAJA KUTIBUA NA MUDA SI MREFU ATARUDI NYUMBANI KWAKE SIMBA.WAINGEREZA WANASEMA MISSION ACCOMPLISHED.Maana yake kazi aliyopewa na Mo sports club,samahani Simba SC Ameitimiza.

Mpira ni Biashara,Mpira ni SIASA.Ndio maana Rais wa Liberia George Weah alichaguliwa kuwa Rais wa Nchi ya Liberia.Huyu muda wote wa maisha yake alikuwa anacheza mpira,akaingia kwenye siasa akaukwaa urais.

NAHITIMISHA KWA KUWAAMBIA VIONGOZI WA YOUNG AFRICANS SC (YANGA),KAMATI YA UTENDAJI NA MDHAMINI MKUU GSM KUONDOKA.

Yanga ijengwe upya.Manji rudi nyumbani utuokoe.
Utopolo never give up tafuteni chemistry kwanza
 
Back
Top Bottom