Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Kwa hasira kali!
Kwa pamoja wananchi na wapenda soka wa Tanzania wamesikitishwa na suala zima la kughairishwa kwa mechi ya watani wa jadi baina ya Yanga na Simba.
Viongozi wa bodi ya ligi na TFF wameonesha udhaifu mkubwa wa kusimamia hili sakata. Mbaya zaidi walitoa taarifa mapema kuwa mechi itakuwepo na hivi mchana wametoa tena taarifa kuwa mechi haitakuwepo leo hii.
Bodi ya Ligi na TFF watuambie wanalipa vipi hasara ambazo mashabiki waliotoka mikoani wamegharamika kuzitumia kufika jijini Dar-es-salaam kuitazama hii mechi?
Bodi ya Ligi na TFF wameonesha wazi kuwa hawana nguvu yoyote ya usimamizi wa hii ligi kuu ya NBC. Hivyo wajiuzulu ili kupisha watu wenye weledi wa kuiongoza hii ligi.
Bodi ya Ligi na TFF imeonesha wazi kuwa inapelekeshwa na hizi timu mbili kubwa nchini Tanzania yaani Simba na Yanga.
Hivi TFF na Bodi ya Ligi walishindwa nini kupeleka maafisa wao uwanja wa Taifa ili kufanikisha timu ya Simba iweze kuingia uwanjani na kufanya mazoezi hapo jana?
Lawama zote wa hili sakata tunazipeleka kwa TFF na Bodi ya Ligi...Hivi nini kimezuia hii mechi isichezwe hapo kesho ili kuwaepushia hasara zaidi mashabiki waliosafiri kutoka kila kona ya nchi na nje ya nchi?
Viongozi wa TFF na Bodi ya Ligi wanatakiwa wajiuzulu haraka sana