Viongozi Wote Walio Karibu au Wana Uwezo wa Kumfikia Rais

Viongozi Wote Walio Karibu au Wana Uwezo wa Kumfikia Rais

Wanao wajibu wa kumweleza rais ukweli wanavyouona wao kwa msukumo wa uzalendo wao kwa nchi yao.

Maswala mazito, kama hili la Bandari yanapotokea nchini na kuwa na mwonekano wa kuwagawa wananchi katika makundi yanayovutanai, siyo mambo ya kunyamazia, hasa kwa viongozi wa ngazi za juu mbalimbali waliomo serikalini na ndani ya chama cha Mapinduzi.

Kwa bahati mbaya katika nchi yetu hatunayo mifano mingi ya aina ya watu wa namna hii, lakini tunaweza kumtaja Oscar Kambona, na pengine hata Abood Jumbe kama mifano husika.

Inaeleweka, siyo jambo sahihi kwa viongozi hawa kujitokeza hovyo hovyo mbele za wananchi na kuanza kuropoka hovyo kuhusu misimamo yao katika jambo linalojadiliwa.

Lakini kamwe, hapawezi kukosekana njia za kumfikia kiongozi wao mkuu na kujadili naye dukuduku zao kuhusu wanayoyaona wao katika jamii kuhusu mwelekeo wa jambo hilo linapoonekana kuleta mtafaruku ndani ya nchi.

Kwa hiyo, viongozi hawa, wanao wajibu mkubwa, kwanza kwa kiongozi wao, lakini hasa hasa kwa wananchi kuwa wawazi kabisa juu ya hali wanavyoiona wao, na kueleza msimamo wao juu ya swala husika.

Wakishajieleza kwa huyu kiongozi wao, na bado maoni yao yakawa hayatiliwi maanani, lakini dhamira zao zikiwa bado ni hasi juu ya jambo zima linavyofanyika; ni wajibu wa hawa viongozi kujitokeza mbele na kujieleza waonavyo wao. Huu ni wajibu wao kwa wananchi na kwa taifa lao.

Sasa mimi ninajiuliza baada ya kufikia hapa tulipofika na hii Bandari, huku serikali wakisema wananchi hawana elimu; na hao wanaotoa elimu wakizidi kuonekana kama vioja, je hawa viongozi wetu ambao dhamira zao zinawasuta juu ya jambo hili wao watafanya nini? Kunyamaza kimya ndilo suluhisho na salama kwao?

Kamwe siamini kuwa hakuna watu wa aina hiyo katika ngazi mbali mbali serikalini na ndani ya chama.

Watakaa kimya wakiwa na matumaini kwamba jambo lenyewe litalazimishwa kwa nguvu za dola na liwalo na liwe?

Inanibidi nitoe angalau mfano mmoja, hata kama sijui huyu mtu anasimamia wapi katika swala zima la Bandari..

Huyu "Profesa aliyeokotwa Jalalani" kwa namna alivyojipambanua wakati wa Magufuli, ni vigumu sana kuamini kwamba sasa hivi kabadilika na kuunga mkono hatua hizi zilizochukuliwa hadi kuwepo na makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu bandari zetu chini ya masharti yaliyomo ndani ya IGA.

Ni vigumu pia kuamini kwamba, yeye, kama mshauri wa Rais wa sasa, kama inavyofahamika, kwamba hakuwa na ushiriki, au ufahamu wowote juu ya jambo hili. Na kama hakuwa na ufahamu wowote hadi lilipojitokeza mbele za wananchi, hali hiyo yeye ataiona vipi, kama mshauri?

Huyu Profesa analo lipi tena la kupoteza katika maisha yake kwa hapo alipofikia, kiasi kwamba aogope hata kule kutamka tu lolote analoona ni kwa msukumo wa uzalendo kwa nchi yake! Bado anasubiri kuteuliwa kuwa waziri?

Nimetumia mfano wa Profesa Kabudi, lakini ipo mifano mingi sana ya viongozi hawa wanaoonekana kutoweka uzalendo wao mbele, kuitetea nchi yao dhidi ya kitu kingine chochote kwa ubinafsi wao pekee.

Nitawataja tu akina Majaliwa (Kassim); akina Lukuvi; Mawaziri mbalimbali, wabunge, n.k..

Huko kwenye chama nasikitika sina hata mmoja wa kumpa heshima ya kumtaja hapa.
Naona ni kama wote ni watumishi wa Mwenyekiti tu, wasiokuwa na utashi wowote juu ya jambo lolote.

Inasikitisha sana.
Don't be the first to say the Queen is naked!
Mfalme hapingwi Afrika!
 
Duh!

Kumbe? Haya nieleze hawa "wanaume" walikokwisha tufikisha. Tumesogelea karibu na Ulaya?

India ni ulaya, eti!

Hii 'argument' yako haina mashiko yoyote.
Acha ubishi Samia is an incompetent President!
 
na kama akiendelea kukaidi ushauri wao, ni muhimu wasaidizi hawa wajieleze kwa wananchi kulinda uzalendo kwa nchi yao.
Mkuu wamwambie nini na wao wanalinda ugali wao na matumbo yao? Sana sana wataogopa kupoteza vibarua vyao km ikionekana wana mawazo tofauti na yeye, wazungu wanasema 'never outshine your Master'
✍️
 
Acha ubishi Samia is an incompetent President!
Ona na wewe, unarukia tu jambo usilojua limeanzia wapi?
Umesoma wapi nilipoanadika kuwa Samia ni rais bora. Nionyeshe sasa hivi nilipoandika kwenya mada hii kuwa Samia ni rais "compitent".
Hizi bangi zinawaharibu vichwa vyenu kwelikweli.
 
Mkuu wamwambie nini na wao wanalinda ugali wao na matumbo yao? Sana sana wataogopa kupoteza vibarua vyao km ikionekana wana mawazo tofauti na yeye, wazungu wanasema 'never outshine your Master'
✍️
Nafahamu hili ndilo tatizo kubwa sana kwa hawa tunaowaita "viongozi" sifa ambayo hawaistahili kabisa.

Kuna mambo ambayo hawatakiwi kuwa na msimamo tofauti na ule uliofikiwa katika maamuza ya pamoja, kichama, au ndani ya serikali katika Baraza la Mawaziri.

Katika ngazi ya vikao hivyo huko kwenye chama au serkalini ndiko kunakotakiwa kuwa na mijadala moto moto sana ndani kwa ndani, hadi wanafikia maelewano ya pamoja, ambalo wote kwa ujumla wao wanakuwa pamoja kulitetea.

Lakini inavyoonekana nyakati hizi, hata vikao hivi havifanyi majadiliano ya aina hii. Mara nyingi ni uamzi tu aliokwishafanya mwenyekiti wao/rais na kuja kuwafikishia taarifa tu hawa wajumbe bila ya kushirikishwa na bila ya mjadala wa maana wa kufanya maamuzi juu ya jambo husika.

Huu mkataba wa Bandari ni mfano halisi wa haya ninayoeleza hapa, la sivyo kusingekuwepo na kelele nyingi kiasi hiki

Ni katika hali ya namna hii ndipo washauri wa kweli wa rais, wanaotumwa na uzalendo wa nchi yao wanapopaswa kumweleza kiongozi huyo misimamo yao, bila kujali hayo maslahi yao binafsi. Uzalendo una thawabu kubwa zaidi kuliko maslahi binafsi haya yanayowalaza akili hawa watu.
Watu hujitoa mhanga kufia nchi yao, kama vitani, bila kujali maslahi yao binafsi, itakuwa kucha kazi, ambayo pengine itapatikana nyingine nzuri zaidi na maisha kuendelea mbele?

Mbona Edwin Mtei aliacha Ugavana wa Benki, na maisha yakaendelea mbele!
 
" ... Wananchi hawana elimu, na wanaozidi kutoa hiyo elimu wakionekana vioja"

Hiyo caught hapo juu inaonesha vile tunachezewa na wajinga, wanaotudanganya hatuna tunalofahamu kuhusu ule mkataba wa hovyo, lakini kumbe, hao wanaotuambia hatufahamu kitu, wao ndio wajinga kabisa.

Hapo ndipo tunapoamua kwamba, hatuna sababu tena kuendelea kuwasikiliza hao wajinga, ambao baada ya kuona hatuelewi ujinga wao, wakaja na ujinga mwingine wa udini, nao tukaupuuza, sasa nao kama wanataka kuja na ujinga wa kumlaumu Nyerere kwa kila jambo, huu nao wakijaribu ndio utapuuzwa vibaya kabisa.

Vyema watambue tu, hili sasa sio taifa la wajinga walilozoea, hili ni taifa la watanganyika tofauti, werevu, wenye uwezo wa kuhoji, na kuhitaji majibu ya msingi sio vioja.
 
Back
Top Bottom