Vipaji 20 bora vya muda wote kwenye muziki wa Tanzania

Barnabas, Mboso wana vipaji vikubwa sana ila hawana mafanikio makubwa
 
HAWA HUWAJUI ??
*HEMEDI MANETI
*EDDY SHEGI
*HAMZA KALALA
*NIKO ZENGEKALA
*MWIMAMILA
*MORRIS NYUNYUSA
*NGURUMO
*JERRY NASHON
*BALISIDYA
*****N.K
 
Kitendo Cha Diamond platnamz kukosekana kwenye top ten ni dharau kubwa sana kwa watu wa mziki. twenty years+ msanii hajawahi kuchuja Wala kupoteza kwenye mziki unachukulia ni jambo dogo?? Punguzeni chuki mnapofanya tafiti zenu.
 
Kwako wewe sasa ila siyo Bora kwa watu wote
 
Ramadhan Masanja “Banza Stone” alikuwa mbele ya muda

Mwenyezi ampunguzie adhabu ya kaburi na amlaze mahala pema peponi
 
Kwa hicho kizazi cha kisasa mimi ningewaondoa wote, na kuwaingiza Cosmas Chidumule, Marehemu mzee Juma mlisho, Ngolimba wa Ngolimba Shabani Dede, Max Wiliam Bushoke. Na wengine wengi.
I second you ... Na Bushoke sijui kwa nin watu wanamchukulia Poa. Isee Bushoke ni Maana halisi ya Kipaji cha Mziki hapa Tanzania, Ni mzuri kuanzia Utunzi mpaka kuimba. Banana Zoro pia nisingemuweka Mbali
 
Kumtaja bi kidude ambaye career yake yote anaimba cover za msanii mwengine na kumuacha OG aliyetunga hizo nyimbo na kuziimba Siti binti Saad?

Siti pengine ndio msanii bora zaidi kutokea ukanda wetu, nyimbo zake hadi leo zinakua covered na Ali exist zaidi ya miaka 100 iliopita.
 
Ushubwada huo!
Sasa kwa wewe, mtoto wa kizazi cha Nandi huwezi kuelewa hapo, maana kwako hata mziki wa Dudubaya, Ray c, Daz nunda, East Coast, Dataz, Mandojo & Domokaya na wengine wa kizazi hicho ni hadithi, Hapo zaidi na kizazi Cha Cool Jemes (James Dandu) Sugu AkA Jangwe.
.
 
Sasa kwa nini uwaondoe wasanii wa kizazi hiki?
Kwamba vipaji vya kuimba walikuwanavyo watu wa zamani tu na watu wa siku hizi hawana vipaji hivyo au?
 
Bado: Patrick Balisidya, john kijiko, muhidin maalim ngurumo, cosmas chidumule, nico zengekala,
 
Ingependeza uweke top 20 ya mwanamuziki wa Tanzania na top 20 ya wasanii wa Tanzania.

Ili kuondoa double standard
 
Anyway mawazo yako yaheshimiwe
 
Sasa kwa nini uwaondoe wasanii wa kizazi hiki?
Kwamba vipaji vya kuimba walikuwa nao watu wa zamani tu na watu wa siku hizi wana vipaji hivyo au?
Sababu hawajafikia ubora wa Waimbaji wa zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…