Vipengele vya Katiba unavyodhani haviko sawa na mapendekezo yako

Vipengele vya Katiba unavyodhani haviko sawa na mapendekezo yako

Kuwepo na kipengele cha kuhakikisha Wakuu wa nchi wastaafu wanadhibitiwa kisheria. Ili wale waliopungukiwa hikma na busara wanapo jaribu kutaka kwa mlango wa uwani kupenyeza agenda zao wakwame. Hii itasaidia hata wasaidizi wa Rais aliye madarakani wajiamini katika kutenda kazi kwao. Sio hii ya sasa ambayo inawafanya wachanganyikiwe ima wamsikilize aliye madarakani au wawafurahishe wastaafu wasije wakapenyezewa fitina tonge likaingia mchanga.
 
Madaraka ya rais ni makubwa iwepo check and balance rais awajibishwe kwa kutofuata katiba, jinai, Wizi na ufisadi hata akiwa madarakani.

Kazi za mahakama ziachwe zifanywe na mahakama kama kupatikana kwa Majaji, jaji mkuu, mwanasheria mkuu wa serikali!

Kuondoa utitili wa vyeo kama

Mkuu wa wilaya

Mkuu wa mkoa

Wabaki wakurugenzi

Wabaki wabunge

Wabaki madiwani na meya ndiye awe bosi wa wilaya na achaguliwe na wananchi

Wabunge wagombee wawili yaani mwanamke na mwanaume na lisiwe jimbo iwe kwa kila wilaya

Waziri mkuu na mawaziri wasiwe wabunge wawe wasomi na wapitishwe na bunge na mahakama kwa kufanyiwa vetting na kuangaliwa juu ya record zao za uko nyuma.

Sera ya Elimu iwekwe kwenye katiba hata aje kichaa gani watanzania waweze kusoma bure elimu ya msingi na sekondani na elimu yote i-base kwenye technical education.

Afya tuwe na Sera ya bima kwa watu wote iwe ni lazima kwa kila mtu utengenezwe mfumo wa kila raia kuwa na bima ya bei nafuu na tuwatambue masikini wote wanaoishi chini ya dollar moja kwa siku bima wapewe bure ndani ya katiba.

Ni hayo tu wengine watasema mengine!!
Umemaliza ongezea hapo atakaegunduluja kafisadi anyongwe jumatatu pale kwa mkapa iwe siku maalum na vyombo vya habari virushe live
 
iingizwe Adhabu ya kifo kwa wala rushwa na Mafisadi.
Adhabu ya kifo ni kinyume na haki za binadamu. Lengo la adhabu ni "deterrence", yaani kumfanya mkosaji ajutie kosa na asirudie.

Ukishamuua lengo la adhabu linapotea kwa kuwa anakuwa hayupo tena kwa kujifunza
 
Adhabu ya kifo ni kinyume na haki za binadamu. Lengo la adhabu ni "deterrence", yaani kumfanya mkosaji ajutie kosa na asirudie.

Ukishamuua lengo la adhabu linapotea kwa kuwa anakuwa hayupo tena kwa kujifunza
Itakuwa fundisho kwa atakayeshuhudia na atafanya akijua lazima aende na maji hio adhabu ni sawa kabisa tena irushwe live pale uwanja wa Uhuru CCM waaache kutuchezea
 
Kiweke kipengele kinacho taja dira ya uchumi ya Taifa ambayo itakuwa inapitishwa na Bunge kila baada ya miaka 25. Vile vile kuwe na kipengele kinachomzuia Rais kutekeleza dira/ miradi yake binafsi au dira ya chama chake.

Hii itazuia mambo kama haya ambayo Mwendazake ameyafanya kujenga Airport kijinini kwake au alivyoacha kuendeleza mradi wa gesi ya Mtwara na kwenda kukata miti ya Selous Game reserve kwa ajili ya umeme wa 2100 megawatt
 
Mahakama, bunge na tume ya uchaguzi zijitegemee.

Kiandaliwe chombo Cha kuchagua Jaji mkuu, mkurugenzi wa time ya uchaguzi na jinsi ya kupata spika ikiwezekana atoke nje ya vyama vyenye wabunge ndani ya bunge.

Rais asiteuwe wakuu was mihimili inayojitegemea.
 
MI NAOMBA TANZANIA IUNDWE UPYA KUWA MOJA. KATIBA MOJA, RAIS MMOJA, BUNGE MOJA NA MAHAKAMA MOJA. CHINI YAKE NI MAJIMBO. KIFUP KUSIWEPO BARA NA VISIWAN AU TANGANYIKA NA ZANZIBAR
 
Kwa kadri joto la kudai katiba mpya linavyozidi ndivyo ninavyojiuliza maswali mengi sana.

Maswali haya yanatokana na kwamba tulishuhudia jirani zetu Kenya walitunga katiba mpya kwa mbwembwe nyingi sana, kwa kuaminishwa kwamba wamepata muarobaini wa demokrasia.

Hata hivyo muda mfupi baadae walianza kuilalamikia hiyo katiba mpya kiasi cha kuibuka upya kwa vuguvugu linalodai mabadiliko mengine ya katiba ambayo hata raisi yuko upande wa walalamikaji.

Kwa uelewa wangu wa kawaida, kwa nchi zetu za kiafrika katiba nzuri ni ile inayompendelea mhusika kwenye maslahi yake.

Tuache kuzolewa na upepo wa wanasiasa naomba tutoe maoni huru kabla ya kuvaa jezi ya chama chochote ni kipengele kipi na kipi unadhani hakipaswi kuwepo kwenye katiba na kwa sababu zipi?

Mkuu umehitaji maoni huru bila kuvaa jezi wakati wewe umesheheni maoni lukuki ukiwa umevaa jezi.

Ya Kenya umeyapotosha kwa maslahi ya jezi ulilovaa.

Kwa kuyatambua mapungufu hayo ya dhahiri, itoshe sasa kukupa baadhi ya mapungufu ya wazi ya katiba iliyopo, ambayo yanaweka umuhimu na dharura ya katiba mpya hasa kwa mtanzania yule wa kawaida:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Kwa katiba hii polisi wanaweza mshikilia mtu kwa kumbambikizia kesi hata kwa miaka kadhaa. Mhanga akaja kuachiliwa bila ya wahusika kuwajibika kwa lolote. Hili likihalalishwa na katiba hii.
9. Nk.Nk.

Yako mengi ila umevaa jezi mkuu yaani hata kuandikia ni ukakasi mtupu!

Hata hivyo, kwenye mazingira haya hudhani kuwa mwananchi wa kawaida anaihitaji zaidi katiba mpya kuliko hata hao wanasiasa?

Kwamba, hudhani kuwa anayedhani hahitaji katiba mpya ni kwa sababu tu ya ujinga wake au kukosa elimu au kuwa na uelewa mdogo tu?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Katiba itamke wazi kwamba hayupo aliye juu ya sheria, raia wote wako sawa mbele ya sheria......rais akiiba kuku ashtakiwe sawa na kijana wa uswazi aliyekwiba kuku. Hizo kinga walizowekeana hadi kina ndugai ziondolewe, tutambue kwamba aliye juu ya sheria ni Mungu Mwenyezi pekee. Ikiwa Mungu anaweza kuapa kwa jina lake kuu na asiende kinyume na kiapo chake, itakuwa binadamu bhanaa............

Kingine, endapo rais amefariki au ameshindwa kufanya majukumu yake, jaji mkuu akaimu nafasi kwa kipindi kisichozidi miezi sita na uchaguzi mwingine ufanyike......
 
Umeambkwa vipengele gani umekimbilia u-DC. U DC ni kipengele? Pumbavu!!!

Anapewa vipengele vya nini aliyeomba maoni huru bila kuvaa jezi wakati yeye kasheheni maoni lukuki yasiyo huru, huku dhahiri akiwa katupia jezi ya kijani kama mburumundu tu?!
 
Wewe ni mzima au umekimbia matibabu? Mbona unatukana watu hovyo wakati mleta mada kimsingi kataka maoni.
Mtoa mada kaulizia "vipengele". Huyo niliyemjibu Kuna kipengele kakionesha? Pumbavu!
 
Rangi ya katiba iwe kijani au njano kama timu ya wananchi
 
Kwa kadri joto la kudai katiba mpya linavyozidi ndivyo ninavyojiuliza maswali mengi sana.

Maswali haya yanatokana na kwamba tulishuhudia jirani zetu Kenya walitunga katiba mpya kwa mbwembwe nyingi sana, kwa kuaminishwa kwamba wamepata muarobaini wa demokrasia.

Hata hivyo muda mfupi baadae walianza kuilalamikia hiyo katiba mpya kiasi cha kuibuka upya kwa vuguvugu linalodai mabadiliko mengine ya katiba ambayo hata raisi yuko upande wa walalamikaji.

Kwa uelewa wangu wa kawaida, kwa nchi zetu za kiafrika katiba nzuri ni ile inayompendelea mhusika kwenye maslahi yake.

Tuache kuzolewa na upepo wa wanasiasa naomba tutoe maoni huru kabla ya kuvaa jezi ya chama chochote ni kipengele kipi na kipi unadhani hakipaswi kuwepo kwenye katiba na kwa sababu zipi?

Ile Rasimu ya warioba ilikuwa KONKI sana...Waipitishe ile tu.
 
Back
Top Bottom