Vipengele vya Katiba unavyodhani haviko sawa na mapendekezo yako

Vipengele vya Katiba unavyodhani haviko sawa na mapendekezo yako

je haya yote yamo katika ile rasimu ya warioba?
ninachojua kiasi ni kwamba katiba mpya itakuja kuendelea pale mchakato ulipoishia

Hayo tano mkuu bila kuusahau mhogo mchungu: serikali 3 au 1.
 
MI NAOMBA TANZANIA IUNDWE UPYA KUWA MOJA. KATIBA MOJA, RAIS MMOJA, BUNGE MOJA NA MAHAKAMA MOJA. CHINI YAKE NI MAJIMBO. KIFUP KUSIWEPO BARA NA VISIWAN AU TANGANYIKA NA ZANZIBAR
We wazanzibar watakupiga dua Sasa hivi,
 
Kuwepo kwa Statesman (Hili litakua ni kundi la wataalamu mbalimbali ambao hawafungamani na chama chochote cha siasa watakaoishauri serikali ktk masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii)

Sent from my vivo 1820 using JamiiForums mobile app
 
We wazanzibar watakupiga dua Sasa hivi,
ni kwa faida ya wote naamin. wakiendelea kushupaza shingo bas tuache vyote. kuna watu hawatambui umuhim wa mtu mpaka awe marehem. sasa bara wao wanamiliki ardhi sisi kwao hapana. kama vile tunalazmisha ndoa. zanzibar ipo tanganyika haipo(ingawa binafs hata neno tanganyika silipend). wana wabunge huku sisi kwao hatuna. wana katiba yao sisi hatuna. wana rais wao sisi hatuna. kila kitu tunawapanulia tuuu.
UNDUGU WETU UMESHAKOMAA INATOSHA TUWE NCHI MOJA, YENYE SERKALI MOJA. sana sana bara watasaidia kuambukiza kupenda haki na ustaarab.
 
Mkuu binafsi naunga mkono mawazo YAKO ,ila wazanzibar kuwambia tuifute Zanzibar Kama AMBAVYO ilifanyika kwa TANGANYIKA ili tue kitu kimoja ,Jiandae na makombora ya dua, hawawezi kukubali, serikali tatu ndo inaweza tutoa tulipo , tuludishiwe TANGANYIKA ,then pawepo serikali ya Muungano,
 
Rasimu ya Warioba bado ingali ina mapungufu kibao hasa kwenye uteuzi wa majaji na tume ya uchaguzi.

Wabobezi ktk maswala ya sheria waliostaafu ndio waunde tume maalumu ya kuwafanyia watu wanaotakiwa kuwa majaji "Vetting" na rais apelekewe orodha ya wale waliofaulu kwenye mchujo kwa ajili ya kuapishwa.

Tume huru ya uchaguzi iundwe na wananchi wasomi (wasio na uegemezi kwa chama chochote cha siasa) moja kwa moja kwa kuunda kamati za uchaguzi kutoka kwenye ngazi za vijiji/mitaa/kata/wilaya na hao hao wajumbe ndio wachague tume huru ya uchaguzi ya taifa bila kuingiliwa na mtu au kikundi chochote kile katika shughuli hiyo na kisha wawajibike chini ya sheria.
 
Muungano upitiwe upya , twende na serikali tatu, Tanganyika iludi, wa Sasa hapana, Tanganyika imemezwa
Hapo kwenye muundo wa serikali ndipo penye ugumu wa katiba. Tukifika hapo nu bora kupaacha kwanza kiporo(deffered). Hata hivyo rasimu ya Warioba lazima ipitiwe sambamba na rasimu ya Sita ili kuona mapungufu na tofauti zilizopo na practically inakuwaje.
 
Yote KWA yote mkuu muungano twautaka ila uwe fair pande zote bila kujali ni njia gani zitumike kuweka USAWA ,vinginevyo mawazo yako pia yanajenga mkuu
 
Tume ya uchaguzi iwe ni taasisi inayohusisha watu wenye taaruma hiyo na waajiriwe kama wafanyakazi wengine wa umma mfano hakimu, dakitari mwalimu n.k na isiwe tume yenye watendaji wanaochaguliwa na rais au na kiongozi yeyote anayetokana na chama.
Kwenye kuajiliwa hapa nakupinga,kwa hiyo waajiliwe maafisa wa tume watakao sambazwa nchi nzima wakati majukumu yao makubwa yako kila baada ya miaka mitano na inapotokea kufanyika uchaguzi mdogo ambao nao mi emergence.Je huo mshahara na masilahi ya kuwalipa wote hao vinatoka wapi? Huo si ndo uhujumu uchumi namba moja?
 
Kwa kadri joto la kudai katiba mpya linavyozidi ndivyo ninavyojiuliza maswali mengi sana.

Maswali haya yanatokana na kwamba tulishuhudia jirani zetu Kenya walitunga katiba mpya kwa mbwembwe nyingi sana, kwa kuaminishwa kwamba wamepata muarobaini wa demokrasia.

Hata hivyo muda mfupi baadae walianza kuilalamikia hiyo katiba mpya kiasi cha kuibuka upya kwa vuguvugu linalodai mabadiliko mengine ya katiba ambayo hata raisi yuko upande wa walalamikaji.

Kwa uelewa wangu wa kawaida, kwa nchi zetu za kiafrika katiba nzuri ni ile inayompendelea mhusika kwenye maslahi yake.

Tuache kuzolewa na upepo wa wanasiasa naomba tutoe maoni huru kabla ya kuvaa jezi ya chama chochote ni kipengele kipi na kipi unadhani hakipaswi kuwepo kwenye katiba na kwa sababu zipi?
'Succession plan and leadership transition' hatuna
 
CDM nao wapewe kuongoza nchi maana wanalalamika sana
 
Kiweke kipengele kinacho taja dira ya uchumi ya Taifa ambayo itakuwa inapitishwa na Bunge kila baada ya miaka 25. Vile vile kuwe na kipengele kinachomzuia Rais kutekeleza dira/ miradi yake binafsi au dira ya chama chake.

Hii itazuia mambo kama haya ambayo Mwendazake ameyafanya kujenga Airport kijinini kwake au alivyoacha kuendeleza mradi wa gesi ya Mtwara na kwenda kukata miti ya Selous Game reserve kwa ajili ya umeme wa 2100 megawatt
Mkuu umeme wa gas ni ghali sana kuliko umeme wa maji hasa in terms of service.Fungua akili yako na jiruhusu kutafakari na kuelewa.
 
CCM Ife TU ndio wanaleta umaskini wajinga Hawa ..jitu Kama Polepole anachunga mbuzi Kinondoni Leo ndio anaamua maamuzi ya watu 60m ...katiba sio hiari ni lazima kwa jasho na damu
 
Madaraka ya rais ni makubwa iwepo check and balance rais awajibishwe kwa kutofuata katiba, jinai, Wizi na ufisadi hata akiwa madarakani.

Kazi za mahakama ziachwe zifanywe na mahakama kama kupatikana kwa Majaji, jaji mkuu, mwanasheria mkuu wa serikali!

Kuondoa utitili wa vyeo kama

Mkuu wa wilaya

Mkuu wa mkoa

Wabaki wakurugenzi

Wabaki wabunge

Wabaki madiwani na meya ndiye awe bosi wa wilaya na achaguliwe na wananchi

Wabunge wagombee wawili yaani mwanamke na mwanaume na lisiwe jimbo iwe kwa kila wilaya

Muda wa kuwa mbunge au waziri uwe mwisho miaka 10

Waziri mkuu na mawaziri wasiwe wabunge wawe wasomi na wapitishwe na bunge na mahakama kwa kufanyiwa vetting na kuangaliwa juu ya record zao za uko nyuma.

Sera ya Elimu iwekwe kwenye katiba hata aje kichaa gani watanzania waweze kusoma bure elimu ya msingi na sekondani na elimu yote i-base kwenye technical education.

Afya tuwe na Sera ya bima kwa watu wote iwe ni lazima kwa kila mtu utengenezwe mfumo wa kila raia kuwa na bima ya bei nafuu na tuwatambue masikini wote wanaoishi chini ya dollar moja kwa siku bima wapewe bure ndani ya katiba.

Ni hayo tu wengine watasema mengine!!

Kwa mbali nimeichungulia katiba ya Marekani kupitia mapendekezo yako. La kuondoa wakuu wa wilaya, mikoa, das ni la muhimu sana. Nafasi hizo sio hata za kiutendaji lakini zina nguvu kubwa!! Mbunge awe wa wilaya na kama wilaya ina idadi kubwa ya watu - kuwe hata na wabunge wawili au hata watatu kadiri ya idadi ya wananchi. Madiwani wa kata zote za wilaya wawe wachague kati yao meya ambaye ndio atakuwa kuongozi wa kusimamia mkurungenzi ambaye awe ni mwomba kazi hiyo sasa wawa na walinzi wanavoomba sasa!!

Zaidi sana ili kukomesha wizi wa kura kitaifa - tume ya uchaguzi iwe na kikomo katika jimbo tu. Iwe hakuna tume ya taifa ya uchaguzi isipokuwa kukusanya tally ya kura za rais tu!!

Jimbo likusanye aina za kadhaa za kodi kwa ajili ya maendeleo ya elimu, barabara, afya nk katika eneo lake. Haiwezekani wilaya kama kinondoni inakusanya pesa na kuzipeleka kilolo huku ina matatizo lukuki. Tuanze kujali maeneo tunayoishi kuhakikisha yana huduma tunazohihitaji!! Kozi kwa mambo ya kitaifa zitakusanywa na serikali ya kitaifa.

Tunashindwa hata kuiga mambo yanayowezekana kwenye mataifa mengine??? China haikuendelea kwa kuvumbua bali kwa kuiga na kuweka discipline katika utendaji!! Nalo hilo linatushinda??
 
Kwanza Katiba iwe na kipengele cha kujilinda kutokana baadhi ya viongozi wenye tabia kuikiuka waziwazi.

Pili Katiba iweke wazi adhabu kwa viongozi hasa rais anapoingilia shughuli za mihimili mingine ya Bunge na Mahakama.
Katiba iseme kwamba rais anaweza kushitakiwa akiwa madarakani au baada kumaliza uongozi wake iwapo ataingilia shughuli za bunge kama rais au kama kiongozi wa chama chenye idadi kubwa ya wabunge.

Katiba iwekwe vipengele vingi vya kupinga mabadiliko yake yoyote ya ghafla.
Mabadiliko ya Katiba yapitie mchakato mrefu.
Hili ni lazima ili kuwakomesha watu wenye nia za kurefusha vipindi vya utawala.
Kabla ya mabadiliko ya Katiba, tume iitishe kura ya maoni upande wa Zanzibar ili kuamua aina ya Muungano.
Mengine yachukuliwe kwenye rasimu ya Tume ya Warioba.
 
640px-PoliticalSystemGermany.png
 
Mkuu umeme wa gas ni ghali sana kuliko umeme wa maji hasa in terms of service.Fungua akili yako na jiruhusu kutafakari na kuelewa.
Wewe ndiye hujui, tuliza akili yako ufundishwe. Athari za mazingira kwa binadamu zinazosabanishwa na umeme wa hydro ni kubwa kuliko hiyo bei rahisi ya kunulia unit moja TANESCO. Soma athari za Guri Dam la Venezuela ambalo ndiyo kubwa kuliko yote katika South America au Three Gorges Dam ya China.
 
Back
Top Bottom