Madaraka ya rais ni makubwa iwepo check and balance rais awajibishwe kwa kutofuata katiba, jinai, Wizi na ufisadi hata akiwa madarakani.
Kazi za mahakama ziachwe zifanywe na mahakama kama kupatikana kwa Majaji, jaji mkuu, mwanasheria mkuu wa serikali!
Kuondoa utitili wa vyeo kama
Mkuu wa wilaya
Mkuu wa mkoa
Wabaki wakurugenzi
Wabaki wabunge
Wabaki madiwani na meya ndiye awe bosi wa wilaya na achaguliwe na wananchi
Wabunge wagombee wawili yaani mwanamke na mwanaume na lisiwe jimbo iwe kwa kila wilaya
Muda wa kuwa mbunge au waziri uwe mwisho miaka 10
Waziri mkuu na mawaziri wasiwe wabunge wawe wasomi na wapitishwe na bunge na mahakama kwa kufanyiwa vetting na kuangaliwa juu ya record zao za uko nyuma.
Sera ya Elimu iwekwe kwenye katiba hata aje kichaa gani watanzania waweze kusoma bure elimu ya msingi na sekondani na elimu yote i-base kwenye technical education.
Afya tuwe na Sera ya bima kwa watu wote iwe ni lazima kwa kila mtu utengenezwe mfumo wa kila raia kuwa na bima ya bei nafuu na tuwatambue masikini wote wanaoishi chini ya dollar moja kwa siku bima wapewe bure ndani ya katiba.
Ni hayo tu wengine watasema mengine!!