Kwa kadri joto la kudai katiba mpya linavyozidi ndivyo ninavyojiuliza maswali mengi sana.
Maswali haya yanatokana na kwamba tulishuhudia jirani zetu Kenya walitunga katiba mpya kwa mbwembwe nyingi sana, kwa kuaminishwa kwamba wamepata muarobaini wa demokrasia.
Hata hivyo muda mfupi baadae walianza kuilalamikia hiyo katiba mpya kiasi cha kuibuka upya kwa vuguvugu linalodai mabadiliko mengine ya katiba ambayo hata raisi yuko upande wa walalamikaji.
Kwa uelewa wangu wa kawaida, kwa nchi zetu za kiafrika katiba nzuri ni ile inayompendelea mhusika kwenye maslahi yake.
Tuache kuzolewa na upepo wa wanasiasa naomba tutoe maoni huru kabla ya kuvaa jezi ya chama chochote ni kipengele kipi na kipi unadhani hakipaswi kuwepo kwenye katiba na kwa sababu zipi?
Mkuu umehitaji maoni huru bila kuvaa jezi wakati wewe umesheheni maoni lukuki ukiwa umevaa jezi.
Ya Kenya umeyapotosha kwa maslahi ya jezi ulilovaa.
Kwa kuyatambua mapungufu hayo ya dhahiri, itoshe sasa kukupa baadhi ya mapungufu ya wazi ya katiba iliyopo, ambayo yanaweka umuhimu na dharura ya katiba mpya hasa kwa mtanzania yule wa kawaida:
1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe.
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe.
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu.
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi.
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe.
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi.
7. Kuna utitiri wa vigogo wenye mapato yasiyoakisi tija, wala kuwa na ridhaa ya wananchi na wasiolipa kodi wanaopata uhalali kwenye katiba hii.
8. Kwa katiba hii polisi wanaweza mshikilia mtu kwa kumbambikizia kesi hata kwa miaka kadhaa. Mhanga akaja kuachiliwa bila ya wahusika kuwajibika kwa lolote. Hili likihalalishwa na katiba hii.
9. Nk.Nk.
Yako mengi ila umevaa jezi mkuu yaani hata kuandikia ni ukakasi mtupu!
Hata hivyo, kwenye mazingira haya hudhani kuwa mwananchi wa kawaida anaihitaji zaidi katiba mpya kuliko hata hao wanasiasa?
Kwamba, hudhani kuwa anayedhani hahitaji katiba mpya ni kwa sababu tu ya ujinga wake au kukosa elimu au kuwa na uelewa mdogo tu?
Au nasema uongo ndugu zangu?