Vipi Kama Tanzania Ingejiendesha Kwa Mfumo wa Majimbo?

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
8,461
Reaction score
19,779
Wasalaam,

Nimewaza jambo moja, Je Tanzania inaweza kujifunza kutoka kwenye mfumo wa majimbo wa nchi kama Marekani (federalism), na kuutengeneza kwa mazingira yetu?

Sisema tuige Marekani 100%. Lakini kuna principle moja ambayo nadhani inaweza kutumika.

Mamlaka zaidi, rasilimali zaidi na uwajibikaji zaidi viende karibu na wananchi.

Kwa sasa Tanzania ina Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa. Lakini fikiria kama badala ya kuwa na regions (mikoa) ambayo kwa kiasi kikubwa zinategemea maamuzi na bajeti kutoka juu, tungekuwa na majimbo yenye mamlaka makubwa zaidi ya kupanga na kuendesha maendeleo yao.

Kwa mfano, Tanzania inaweza kuwa na majimbo makubwa kama:

Northern State – Arusha, Kilimanjaro, Manyara

Lake State – Mwanza, Mara, Kagera, Geita

Central State – Dodoma, Singida, Tabora

Southern Highlands State – Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe

Southern State – Mtwara, Lindi, Ruvuma

Coastal State – Dar es Salaam, Pwani, Tanga

Western State – Kigoma, Katavi

Zanzibar ikiendelea kuwa na arrangement yake ndani ya Muungano.

Kila jimbo lingekuwa na serikali yake, bajeti yake, mipango yake ya maendeleo na priorities zake, huku Serikali ya Muungano ikibaki na mambo ya kitaifa kama ulinzi, mambo ya nje, fedha/currency na masuala mengine ya Muungano.

Hili ni wazo tu la mjadala.

Ningependa kusikia mawazo yenu,

Tanzania ikiwa na majimbo yenye autonomy kubwa, mnadhani maendeleo yataongezeka au tutatengeneza matatizo mapya?

Nawasilisha.✍️

Wasalaam,

Mla bata

München, Deutschland 🇩🇪.
 
Faida:
• Maendeleo ya haraka: Majimbo yatatumia rasilimali zao moja kwa moja (kama madini au kilimo) bila kusubiri maamuzi ya Dar es Salaam.
• Ukaribu wa viongozi: Madaraka yanawafikia wananchi kwa karibu, na maamuzi yanafanyika haraka.
Changamoto:
• Hatari ya ukabila na ukanda: Kuna uwezekano wa kupoteza umoja wa kitaifa na kuongezeka kwa ubaguzi wa kikanda.
• Pengo la kiuchumi: Majimbo yenye utajiri (kama Geita au Arusha) yatatajirika haraka, huku majimbo yasiyo na rasilimali yakibaki nyuma.
• Gharama kubwa: Uendeshaji wa serikali utakuwa ghali kwa sababu ya kuongezeka kwa magavana na mabunge ya majimbo.
Mimi bnafsi kwa Tanzania Bado kuwa na serikali ya majimbo
 
Ni sera nzuri ila kuna majimbo yatakufa kwa Njaa kali sana
Hapo ndipo tunahitaji mfumo wa kusawazisha rasilimali kupitia . 😄 Jimbo tajiri lisibebe kila kitu, na jimbo maskini lisiachwe life. Serikali Kuu iwe na mfuko wa kitaifa(Equalization fund) wa kusaidia majimbo yenye uwezo mdogo.
Na kumbuka, jimboni kuwa na autonomy si sawa na kujitenga na taifa. Tunazungumzia kugawa mamlaka, si kugawa Tanzania.
 
Kwa Nini un

Kwa Nini unadhan mpaka leo Kenya ukabira umewandama?
 
Faida:
• Maendeleo ya haraka: Majimbo yatatumia rasilimali zao moja kwa moja (kama madini au kilimo) bila kusubiri maamuzi ya Dar es Salaam.
• Ukaribu wa viongozi: Madaraka yanawafikia wananchi kwa karibu, na maamuzi yanafanyika haraka.
Changamoto:
• Hatari ya ukabila na ukanda: Kuna uwezekano wa kupoteza umoja wa kitaifa na kuongezeka kwa ubaguzi wa kikanda.
• Pengo la kiuchumi: Majimbo yenye utajiri (kama Geita au Arusha) yatatajirika haraka, huku majimbo yasiyo na rasilimali yakibaki nyuma.
• Gharama kubwa: Uendeshaji wa serikali utakuwa ghali kwa sababu ya kuongezeka kwa magavana na mabunge ya majimbo.
Mimi bnafsi kwa Tanzania Bado kuwa na serikali ya majimbo

Hoja zako zina mashiko mkuu. Lakini nadhani changamoto nyingi ulizotaja hazifanyi mfumo wa majimbo usiwezekane

Issue kama ya Ukabila/ukanda inaweza kuzuiwa na Katiba na taasisi za Muungano. Tofauti za kiuchumi zikadhibitiwa kwa mfumo wa kugawana mapato, na gharama za serikali zikadhibitiwa kwa kupunguza bureaucracy.
 
Embu kwanza panga hizo Kanda zako vizuri.

Pili kama lengo ni majimbo makubwa

Basi Kanda ya mashariki lazima
Ihusishe Morogoro, Pwani, Dar es salaam.

Kanda ya kaskazini ianzie Tanga, Kilimanjaro, Arusha na musoma

Kanda ya Kusini iwe Lindi, Mtwara, Ruvuma

Kanda ya kati
Iwe Dodoma, Manyara, Singida

Kanda ya magharibi iwe katavi, Tabora, Kigoma na kagera

Mafia uwe mkoa na iwe Kanda ya mashariki

Ukerewe iwe special administrative zone

Kanda ya ziwa iwe Mwanza, Simiyu, Geita
 
Hapo ndipo tunahitaji mfumo wa kusawazisha rasilimali kupitia . 😄 Jimbo tajiri lisibebe kila kitu, na jimbo maskini lisiachwe life. Serikali Kuu iwe na mfuko wa kitaifa(Equalization fund) wa kusaidia majimbo yenye uwezo mdogo.
Na kumbuka, jimboni kuwa na autonomy si sawa na kujitenga na taifa. Tunazungumzia kugawa mamlaka, si kugawa Tanzania.

1.hakuna jimbo masikini kati ya uliyoyataja.

2.kuna uhuru wa Watz kuishi na kufanya shughuli halali popote.

3.majimbo yatapewa mamlaka machache yatakayowawezesha kutoa huduma bora kwa wakaazi wake.

4.Tunaweza tusianzishe majimbo badala yake tukapeleka mamlaka zaidi kwa mikoa kutoa huduma za kijamii kwa wakazi wake.

5.Nafasi ya Mkuu wa mkoa ingefaa iwe ya kuchaguliwa kwa kura kuliko kuteuliwa na Rais.
 
..Kenya ukabila ulikuwepo tangu wakati kabla ya uhuru.

..kazi ya majimbo sio kuondoa changamoto za ukabila, au udini.

..majimbo yanapendekezwa kwa ajili ya kuboresha huduma kwa jamii, na kuchochea maendeleo.
👏🏽👏🏽👏🏽
 
Wazo lako ni baya . Unataka kuigawa Nchi vipande vipande.
Kiufupi wewe ni MTU mzima na umesoma lakini huijui history ya Nchi Yako, na hata hujui Nchi inahitaji nini kwa Sasa.
 
Na kama Mkuu wa Mkoa atachaguliwa na wananchi, basi uwajibikaji unakuwa wa moja kwa moja, anayeshindwa kuleta matokeo anaondolewa na wananchi, sio kama sasa kusubiri utashi wa anayemteua.

..ukisikiliza mahojiano ya Wakuu wa mikoa wa sasa hivi na vyombo vya habari utasikia mambo yafuatayo.

1.huwa wanapewa " maagizo " kuhusu mambo wanayotakiwa kuyatekeleza. Ni kama vision ya Raisi kuhusu mkoa husika.

2.wengi wanaeleza kwamba hulazimika kupitia kipindi cha mpito kulielewa eneoao la kazi, na jamii waliyoteuliwa kuiongoza.

3.wakati mwingine huhamishwa mara wanapokuwa wameshajifunza kuhusu mazingira mapya ya eneo wanaloongoza.

..mimi kwa kuzingatia yote hayo nimeona ni bora Mkuu wa Mkoa awe amechaguliwa na wananchi.

..Naamini kiongozi wa namna hiyo atakuwa na utayari zaidi kuwatumikia wananchi, na atakuwa loyal kwao badala kwa mamlaka ya Rais. Na wananchi wataweza kumdhibiti kuliko hawa wakuu wa mikoa wa sasa hivi.
 
Wazo lako ni baya . Unataka kuigawa Nchi vipande vipande.
Kiufupi wewe ni MTU mzima na umesoma lakini huijui history ya Nchi Yako, na hata hujui Nchi inahitaji nini kwa Sasa.
Ni tafakuri tu mkuu.
 
..hebu fafanua hoja yako.

..kwasababu hata mikoa imegawa nchi vipande vipande.
Huyo ni "muhafidhina" naelewa wasiwasi wake.

Wasalaam,

Nimewaza jambo moja, Je Tanzania inaweza kujifunza kutoka kwenye mfumo wa majimbo wa nchi kama Marekani (federalism), na kuutengeneza kwa mazingira yetu?

Sisema tuige Marekani 100%. Lakini kuna principle moja ambayo nadhani inaweza kutumika.

Mamlaka zaidi, rasilimali zaidi na uwajibikaji zaidi viende karibu na wananchi.

Kwa sasa Tanzania ina Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa. Lakini fikiria kama badala ya kuwa na regions (mikoa) ambayo kwa kiasi kikubwa zinategemea maamuzi na bajeti kutoka juu, tungekuwa na majimbo yenye mamlaka makubwa zaidi ya kupanga na kuendesha maendeleo yao.

Kwa mfano, Tanzania inaweza kuwa na majimbo makubwa kama:

Northern State – Arusha, Kilimanjaro, Manyara

Lake State – Mwanza, Mara, Kagera, Geita

Central State – Dodoma, Singida, Tabora

Southern Highlands State – Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe

Southern State – Mtwara, Lindi, Ruvuma

Coastal State – Dar es Salaam, Pwani, Tanga

Western State – Kigoma, Katavi

Zanzibar ikiendelea kuwa na arrangement yake ndani ya Muungano.

Kila jimbo lingekuwa na serikali yake, bajeti yake, mipango yake ya maendeleo na priorities zake, huku Serikali ya Muungano ikibaki na mambo ya kitaifa kama ulinzi, mambo ya nje, fedha/currency na masuala mengine ya Muungano.

Hili ni wazo tu la mjadala.

Ningependa kusikia mawazo yenu,

Tanzania ikiwa na majimbo yenye autonomy kubwa, mnadhani maendeleo yataongezeka au tutatengeneza matatizo mapya?

Nawasilisha.✍️

Wasalaam,

Mla bata

München, Deutschland 🇩🇪.
Itarudi nyuma kwa 200%.

Kutokana na background ya TZ, inatakiwa kuiga nchi zilizofanikiwa ambazo tunafanana background kama China, Vietnam, Malaysia.
 
Back
Top Bottom