Kwasasa NCHI NZIMA ni INAZUNGUMZA lugha moja.Kwanini umefikiri hivyo mkuu?
Mkuu TU implement mipango miji ya kisasa kwa Nchi yetuNi tafakuri tu mkuu.
Hii ni sera ya CHADEMA ipo kwenye ilani yaoWasalaam,
Nimewaza jambo moja, Je Tanzania inaweza kujifunza kutoka kwenye mfumo wa majimbo wa nchi kama Marekani (federalism), na kuutengeneza kwa mazingira yetu?
Sisema tuige Marekani 100%. Lakini kuna principle moja ambayo nadhani inaweza kutumika.
Mamlaka zaidi, rasilimali zaidi na uwajibikaji zaidi viende karibu na wananchi.
Kwa sasa Tanzania ina Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa. Lakini fikiria kama badala ya kuwa na regions (mikoa) ambayo kwa kiasi kikubwa zinategemea maamuzi na bajeti kutoka juu, tungekuwa na majimbo yenye mamlaka makubwa zaidi ya kupanga na kuendesha maendeleo yao.
Kwa mfano, Tanzania inaweza kuwa na majimbo makubwa kama:
Northern State – Arusha, Kilimanjaro, Manyara
Lake State – Mwanza, Mara, Kagera, Geita
Central State – Dodoma, Singida, Tabora
Southern Highlands State – Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe
Southern State – Mtwara, Lindi, Ruvuma
Coastal State – Dar es Salaam, Pwani, Tanga
Western State – Kigoma, Katavi
Zanzibar ikiendelea kuwa na arrangement yake ndani ya Muungano.
Kila jimbo lingekuwa na serikali yake, bajeti yake, mipango yake ya maendeleo na priorities zake, huku Serikali ya Muungano ikibaki na mambo ya kitaifa kama ulinzi, mambo ya nje, fedha/currency na masuala mengine ya Muungano.
Hili ni wazo tu la mjadala.
Ningependa kusikia mawazo yenu,
Tanzania ikiwa na majimbo yenye autonomy kubwa, mnadhani maendeleo yataongezeka au tutatengeneza matatizo mapya?
Nawasilisha.✍️
Wasalaam,
Mla bata
München, Deutschland 🇩🇪.
Kwanini Comrade?
Kwasasa NCHI NZIMA ni INAZUNGUMZA lugha moja.
Inahitaji tu RAIS kama NYERERE atakaysimamia VISION ya UCHUMI ya NCHI, KIMAGUFULI.
Ukitenga, nchi inageuka VIPANDE vipande, ULAJI kuzidi, UKABILA, na USHINDANI wa BINAFSI usio na MAANA yoyote.
Hakuna MSUKUMA atatoka kwao GEITA, kwenye DHAHABU akafanye kazi SINGIDA ambako.m mapato ni kidogo.
Mfano, halisi angalia INDIA, haiwezi kuwa sawa na CHINA.
Au angalia FEDERALISM ya Nigeria nchi tajiri mkubwa Mafuta, dhahabu na gesi alivyofeli.
Majimbo gani hayana rasilimali?Faida:
• Maendeleo ya haraka: Majimbo yatatumia rasilimali zao moja kwa moja (kama madini au kilimo) bila kusubiri maamuzi ya Dar es Salaam.
• Ukaribu wa viongozi: Madaraka yanawafikia wananchi kwa karibu, na maamuzi yanafanyika haraka.
Changamoto:
• Hatari ya ukabila na ukanda: Kuna uwezekano wa kupoteza umoja wa kitaifa na kuongezeka kwa ubaguzi wa kikanda.
• Pengo la kiuchumi: Majimbo yenye utajiri (kama Geita au Arusha) yatatajirika haraka, huku majimbo yasiyo na rasilimali yakibaki nyuma.
• Gharama kubwa: Uendeshaji wa serikali utakuwa ghali kwa sababu ya kuongezeka kwa magavana na mabunge ya majimbo.
Mimi bnafsi kwa Tanzania Bado kuwa na serikali ya majimbo
Nimetolea dhahabu kama mfano...sio kweli kwamba kila Msukuma wa Geita anataka kuwa ktk sekta ya madini. Wengine wanapenda kulima matikiti watahamia sehemu tofauti.
..kwanza, Dhahabu haitakuwepo miaka yote.
..pili, kuna maeneo mengi nchi hii yana dhahabu au madini mengine.
..tatu, sasa hivi kuna wananchi toka maeneo yalikogunduliwa madini wamesambaa maeneo mengine ya nchi na hawana interest na madini yaliyoko kwao.
..nne, hoja ya ukabila pia haina uzito. Sasa hivi wilaya zote za nchi hii zimegawanywa kikabila na hakuna tatizo lolote.
Nimetolea dhahabu kama mfano.
Palipo na Mzoga ndipo wakusanyiko NZI.
Penye MASLAHI ndio.watu watahamia. Na ukabila utakuwa JUU, maana cha mtu mavi.
Kama.Mtwara wana gesi, maana yake watu wa Mtwara ndio kipaumbele chao cha kwanza.
Kuhamia kwingine haina maana kuwa kwwnu kukinoga usirudi.
MKuu,Bado Sana, tunaweza kutoboa bila ishu za majimbo. Majimbo ili yafanye kazi vizuri inahitaji akili iliyopevuka Sana, Sisi watz bado Sana akili mgando na pia tumevurugwa...
Mambo Kwa ground ni tofauti Sana, wengi hatuna shule wala uelewa wa mambo mazito kama hayo. Itahitajika kufanya kampeni kubwa mno nch nzima ili kuwaelewesha watu kuhusu Hili jambo na Nina uhakika watu wataishia kupiga Hela Tu, watu wengi hawajui Tu but chini kabisa Kwa level ya mtu mmoja mmoja uelewa wetu wa mambo bado Sana, Ukitaka ufanikiwe kwenye Hilo jambo lazima watu wawe na uelewa wa pamoja kuanzia chini kabisa.
Jingine ni CCM, lazima Tu mfumo huo utaundwa kui favor CCM na kumbuka CCM ndio dola yenyewe so Hadi hapo tayari hiyo system ishakuwa compromised, Mfumo huo huo unahitaji watu waadilifu Sana ili kuweza kufanya kazi na Kingine watu wasichokijua ni kwamba Tanzania bado ina migawanyiko ya kikabila na kidini, hivi tunavyoishi sasa tunavumiliana Tu but kuna sehemu nyingi Tu zipo au zimeundwa kwasababu za kikabila au kidini....Kuna mikoa Leo hii utapigwa vita sababu ya dini au kabila lako na hata kwenye mifumo ya serikali pia n hivyo hivyo watu wanaishi kinafki Tu...
So tunatakiwa kuondoa tofauti zetu zile kubwa kubwa ndio twende huko Kwenye majimbo.
Matawi ya juutatizo kubwa la nchi yetu ni utawala mbovu wa CCM unaozorotesha maendeleo pamoja na ukandamizaji wa haki za binaadamu. nje ya hapo moja ya silaha yetu kubwa ni umoja pamoja ya kuwa kuna changamoto ndogo ndogo.
Hio ishu ya majimbo inaweza kwenda kuchochea kutuvuruga. na kuanzisha matabaka baina yetu
Mkuu, nimekuelewa! na concern yako kuhusu umoja wa kitaifa ni ya msingi. Lakini nadhani tunachanganya mambo mawili tofauti, umoja wa nchi na namna ya kugawa madaraka.Kwasasa NCHI NZIMA ni INAZUNGUMZA lugha moja.
Inahitaji tu RAIS kama NYERERE atakaysimamia VISION ya UCHUMI ya NCHI, KIMAGUFULI.
Ukitenga, nchi inageuka VIPANDE vipande, ULAJI kuzidi, UKABILA, na USHINDANI wa BINAFSI usio na MAANA yoyote.
Hakuna MSUKUMA atatoka kwao GEITA, kwenye DHAHABU akafanye kazi SINGIDA ambako.m mapato ni kidogo.
Mfano, halisi angalia INDIA, haiwezi kuwa sawa na CHINA.
Au angalia FEDERALISM ya Nigeria nchi tajiri mkubwa Mafuta, dhahabu na gesi alivyofeli.
Huo mfumo mbona upo.Mkuu, nimekuelewa! na concern yako kuhusu umoja wa kitaifa ni ya msingi. Lakini nadhani tunachanganya mambo mawili tofauti, umoja wa nchi na namna ya kugawa madaraka.
Kuwa na mfumo wa majimbo hakumaanishi kila jimbo liwe nchi yake au kila eneo libaki na rasilimali zake. Unaweza kuwa na serikali kuu yenye vision ya kitaifa kwenye mambo kama sera ya uchumi, ulinzi, mambo ya nje, miundombinu mikubwa na mgawanyo wa rasilimali, huku majimbo yakiwa na mamlaka zaidi ya kusimamia huduma na maendeleo ya maeneo yao.
Na kuhusu mfano wa Nigeria, nadhani tunahitaji kuangalia kwa kina zaidi kabla ya kusema federalism yenyewe ndiyo imesababisha kushindwa. Mfumo unaweza kuwa mzuri au mbaya kulingana na taasisi, sheria, uwajibikaji na namna unavyotekelezwa.
Kwa upande wangu, hoja si kwamba Tanzania ivunjwe vipande vipande. Hoja ni kama tunaweza kujenga mfumo unaompa mwananchi wa Geita, Singida au Mtwara mamlaka zaidi ya kuona na kuwawajibisha viongozi wanaosimamia maendeleo yake, huku bado akiwa Mtanzania kwanza.
Kwa hiyo swali langu lingekuwa: Je, tatizo ni mfumo wa majimbo wenyewe, au ni hofu kwamba Tanzania haina taasisi imara za kuhakikisha mfumo huo hautumiki vibaya?
Mikoa ambayo haujaitaja , umeiua au namna gani?Wasalaam,