Vipi Kama Tanzania Ingejiendesha Kwa Mfumo wa Majimbo?

Kwanini umefikiri hivyo mkuu?
Kwasasa NCHI NZIMA ni INAZUNGUMZA lugha moja.

Inahitaji tu RAIS kama NYERERE atakaysimamia VISION ya UCHUMI ya NCHI, KIMAGUFULI.

Ukitenga, nchi inageuka VIPANDE vipande, ULAJI kuzidi, UKABILA, na USHINDANI wa BINAFSI usio na MAANA yoyote.

Hakuna MSUKUMA atatoka kwao GEITA, kwenye DHAHABU akafanye kazi SINGIDA ambako.m mapato ni kidogo.

Mfano, halisi angalia INDIA, haiwezi kuwa sawa na CHINA.

Au angalia FEDERALISM ya Nigeria nchi tajiri mkubwa Mafuta, dhahabu na gesi alivyofeli.
 
Hii ni sera ya CHADEMA ipo kwenye ilani yao
 
Kwanini Comrade?

tatizo kubwa la nchi yetu ni utawala mbovu wa CCM unaozorotesha maendeleo pamoja na ukandamizaji wa haki za binaadamu. nje ya hapo moja ya silaha yetu kubwa ni umoja pamoja ya kuwa kuna changamoto ndogo ndogo.
Hio ishu ya majimbo inaweza kwenda kuchochea kutuvuruga. na kuanzisha matabaka baina yetu
 
Bado Sana, tunaweza kutoboa bila ishu za majimbo. Majimbo ili yafanye kazi vizuri inahitaji akili iliyopevuka Sana, Sisi watz bado Sana akili mgando na pia tumevurugwa...

Mambo Kwa ground ni tofauti Sana, wengi hatuna shule wala uelewa wa mambo mazito kama hayo. Itahitajika kufanya kampeni kubwa mno nch nzima ili kuwaelewesha watu kuhusu Hili jambo na Nina uhakika watu wataishia kupiga Hela Tu, watu wengi hawajui Tu but chini kabisa Kwa level ya mtu mmoja mmoja uelewa wetu wa mambo bado Sana, Ukitaka ufanikiwe kwenye Hilo jambo lazima watu wawe na uelewa wa pamoja kuanzia chini kabisa.

Jingine ni CCM, lazima Tu mfumo huo utaundwa kui favor CCM na kumbuka CCM ndio dola yenyewe so Hadi hapo tayari hiyo system ishakuwa compromised, Mfumo huo huo unahitaji watu waadilifu Sana ili kuweza kufanya kazi na Kingine watu wasichokijua ni kwamba Tanzania bado ina migawanyiko ya kikabila na kidini, hivi tunavyoishi sasa tunavumiliana Tu but kuna sehemu nyingi Tu zipo au zimeundwa kwasababu za kikabila au kidini....Kuna mikoa Leo hii utapigwa vita sababu ya dini au kabila lako na hata kwenye mifumo ya serikali pia n hivyo hivyo watu wanaishi kinafki Tu...

So tunatakiwa kuondoa tofauti zetu zile kubwa kubwa ndio twende huko Kwenye majimbo.
 

..sio kweli kwamba kila Msukuma wa Geita anataka kuwa ktk sekta ya madini. Wengine wanapenda kulima matikiti watahamia sehemu tofauti.

..kwanza, Dhahabu haitakuwepo miaka yote.

..pili, kuna maeneo mengi nchi hii yana dhahabu au madini mengine.

..tatu, sasa hivi kuna wananchi toka maeneo yalikogunduliwa madini wamesambaa maeneo mengine ya nchi na hawana interest na madini yaliyoko kwao.

..nne, hoja ya ukabila pia haina uzito. Sasa hivi wilaya zote za nchi hii zimegawanywa kikabila na hakuna tatizo lolote.
 
Majimbo gani hayana rasilimali?
 
Nimetolea dhahabu kama mfano.

Palipo na Mzoga ndipo wakusanyiko NZI.

Penye MASLAHI ndio.watu watahamia. Na ukabila utakuwa JUU, maana cha mtu mavi.

Kama.Mtwara wana gesi, maana yake watu wa Mtwara ndio kipaumbele chao cha kwanza.

Kuhamia kwingine haina maana kuwa kwwnu kukinoga usirudi.
 

..tangu gesi imegunduliwa watu wangapi wa kusini wamerudi kwao?

..je ugunduzi wa Tanzanite umepelekea wenyeji wa Mirerani wasichangamkie fursa maeneo mengine?

..sio sawa kuamini kwamba madini ndio fursa au utajiri pekee nchini kwetu.

..pia sio sawa kujifunga kifikra kwamba Mtanzania hapaswi kwenda maeneo mengine kutafuta fursa, na maisha.

..Mikoa tuliyonayo sasa hivi ni majimbo ya zamani yaliyogawanywa.

..Wilaya nyingi hapa nchini ni maeneo ambayo yako dominated na kabila moja la asili la pale.

..Mimi naamini ilimradi Watanzania wana HAKI ya kuishi popote nchini mwao, basi majimbo hayatakuwa na tatizo.
 
MKuu,

Umeibua hoja muhimu, hasa kuhusu uelewa wa wananchi, uadilifu wa taasisi, na changamoto za kiutendaji katika kuanzisha mfumo wa ugatuzi wa madaraka.

Hata hivyo, nadhani baadhi ya dhana zilizopo kwenye hoja yako ndizo hasa zinazopaswa kupingwa. Si lazima tusubiri Watanzania wawe “wamekomaa vya kutosha” ndipo tuanze kufanya mageuzi. Wakati mwingine, mifumo bora ndiyo huweka mazingira yanayowawezesha watu na taasisi kukomaa na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 
Matawi ya juu

Nawaelewa, lakini nadhani hapa tunapaswa kutenganisha mfumo na chama. Hoja ya majimbo si kwamba CCM au chama kingine kipewe majimbo, bali ni kujenga mfumo ambao unaweka mamlaka karibu na wananchi, unaoweka uwajibikaji wazi na unaoruhusu wananchi kuwawajibisha viongozi wao moja kwa moja.

Kama tatizo ni mfumo kutumiwa na chama fulani, basi mjadala wa msingi unapaswa kuwa namna ya kujenga taasisi na mifumo imara ambayo inafanya kazi kwa maslahi ya wananchi, bila kujali nani yuko madarakani.
 
Mkuu, nimekuelewa! na concern yako kuhusu umoja wa kitaifa ni ya msingi. Lakini nadhani tunachanganya mambo mawili tofauti, umoja wa nchi na namna ya kugawa madaraka.

Kuwa na mfumo wa majimbo hakumaanishi kila jimbo liwe nchi yake au kila eneo libaki na rasilimali zake. Unaweza kuwa na serikali kuu yenye vision ya kitaifa kwenye mambo kama sera ya uchumi, ulinzi, mambo ya nje, miundombinu mikubwa na mgawanyo wa rasilimali, huku majimbo yakiwa na mamlaka zaidi ya kusimamia huduma na maendeleo ya maeneo yao.

Na kuhusu mfano wa Nigeria, nadhani tunahitaji kuangalia kwa kina zaidi kabla ya kusema federalism yenyewe ndiyo imesababisha kushindwa. Mfumo unaweza kuwa mzuri au mbaya kulingana na taasisi, sheria, uwajibikaji na namna unavyotekelezwa.

Kwa upande wangu, hoja si kwamba Tanzania ivunjwe vipande vipande. Hoja ni kama tunaweza kujenga mfumo unaompa mwananchi wa Geita, Singida au Mtwara mamlaka zaidi ya kuona na kuwawajibisha viongozi wanaosimamia maendeleo yake, huku bado akiwa Mtanzania kwanza.

Kwa hiyo swali langu lingekuwa: Je, tatizo ni mfumo wa majimbo wenyewe, au ni hofu kwamba Tanzania haina taasisi imara za kuhakikisha mfumo huo hautumiki vibaya?
 
Huo mfumo mbona upo.

Serikali za vijiji ni serikali kamili.

Halmashauri ni serikali za maamuzi kupitia Madiwani ambao ni wateule wa wananchi.

Kuhusu wananchi kuwajibisha waliowachagua, sidhai maana hao ndio hawawezi hata kuwajibisha madiwani, wenyeviti serikali.za mitaa, Kamati za chakula mashuleni au bodi za shule mashuleni ambazo wao ndio waliowachagua.
 
Mikoa ambayo haujaitaja , umeiua au namna gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…