Vipimo 3 vibovu wadada tunavyotumia kupima upendo na usiriasi wa mwanaume

Vipimo 3 vibovu wadada tunavyotumia kupima upendo na usiriasi wa mwanaume

Darcyy

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2021
Posts
2,432
Reaction score
9,758
(1) Kuomba pesa; Hiki ndiyo kipimo cha kwanza ambacho mabinti wengi wanakitumia, wanaamini mwanaume akikupa pesa basi anakupenda. Utasikia “Muombe pesa ujue kama yuko siriasi na wewe au la?”

Anaweza kukupa pesa kila siku na bado asiwe na mpango na wewe . Najua mwanaume mbahili anaboa, ila usimpime kwakua anakupa pesa, angalia namna anavyojali, kama angalau analipia chakula na nauli hana shida si lazima akupe pesa! Upendo wa kweli hautegemei pesa. Anaweza kutoa pesa, anapata mbunye na akakuacha anaenda kutafuta mwengine.

(2) Kumuambia mwanaume una mimba yake akakubali kulea; Hiki kimetengeneza single mother wengi, unakuta mwanaume alishakuambia umzalie, unamuambia kwanza unamimba ili kuona atafanyaje? Basi akiikubali unaona anakupenda unabeba kweli!

Dada iko hivi, mimba inakataliwa na miezi 6, anaweza kukubali mwanzo ili usitoe ila ukifikisha miezi 6 anajua hutoi anakuacha utalea mwenyewe anawaza kifikisha miaka 7 nakuja kuchukua mwanangu, hivyo hiki si kipimo kabisa.

Mwingine anaweza kukataa kwakua hajajipanga ila baadaye akafikiria na kuona mtoto Baraka akakubali, hivyo achana na kipimo hiki, kukubali au kukataa haina uhusiano na upendo. Au Ile unaona umekaa muda mrefu kwenye uchumba sugu ,basi unaona njia sahihi ni kubeba mimba Ili Huyo mwanaume akukubali mazima. Dada unapotea,acha kabisa mitego km hiyo, upelekea kumtesa mtoto mwisho wa siku.

(3) Mwanaume kujitambulisha kwenu au kukupeleka kwao; Hiki nacho ni cha hovyo kabisa, kuna wanaume ambao hawajali kujitambulisha hata kwa wanawake 20, wengine familia zao hata hazilali, Mama anapelekewa wanawake hata 10 na haulizi chochote tena unakuta anakuomba na pesa, hapo imekula kwako.

Epuka aibu ndogondogo za kutambulisha mwanaume halafu anakuacha, inakua uchumba sugu.

Tafuta kipimo kengine Cha kupimia upendo wa mwanaume, lakini si pesa, mimba Wala kutambulishwa kwao. Mwanaume akupendaye utaona tu upendo wake, hata ipite miezi 5, 6 Mpk 7. Hao wa hivyo vipimo wakimaliza tu shida zao ni ndukiiiii [emoji2091][emoji2091][emoji2091][emoji16], humuoni tena [emoji13][emoji57]
 
(1) Kuomba pesa; Hiki ndiyo kipimo cha kwanza ambacho mabinti wengi wanakitumia, wanaamini mwanaume akikupa pesa basi anakupenda. Utasikia “Muombe pesa ujue kama yuko siriasi na wewe au la?”
Kuomba omba pesa kwa wanawake wa ki-bongo ni tabia sio kigezo cha kupimia mapezi, wanawake wa namna gani akikusemesha maneno matano, matatu yana omba pesa au vitu kavu..........
 
Tukiwaomba papuchi wanajua haupo serious! Na sisi tukinyimwa tunajua Kuna mtu anapewa!.. hapo ndipo kinapoumanaga..[emoji23]

Ila hii dunia bila changamoto hatuendi!
Hii Dunia ngumu Sana [emoji28]... Hapo kwnye papuchi ni maamuzi ya m2 kutoa au kutotoa..... Ina mana na nyie hivyo ndo vipimo vyenu?? [emoji13]
 
Hili la kuomba hela wala si kipimo tena. Imekuwa desturi. Kina dada asilimia kubwa washachukulia mapenzi ni kitego uchumi, kiasi cha kuwa akiwa na mwanaume anataka kila tamanio alilokuwa nalo na hakuweza kulimudu litimizwe na mwanaume. Hii imeleta athari kubwa zaidi kwa wanaume kuchukulia kila mahusiano ni biashara kwa point ya kuwa nakupa hela unazoomba hivyo kuhalalisha kuwa na wanawake wengi zaidi kwa wakati mmoja as long as anaweza ku afford.
 
Kuomba omba pesa kwa wanawake wa ki-bongo ni tabia sio kigezo cha kupimia mapezi, wanawake wa namna gani akikusemesha maneno matano, matatu yana omba pesa au vitu kavu..........
Wengine wanapimia mkuu.. je, aone matumizi yapo???.. Kuna Ile anayekupenda hawezi kukunyima.
 
Mimi nimeshafeli ktk kipimo cha pesa.

Kabla sijakula mzigo nimepigwa kizinga cha Kodi miezi 6.

100k mara 6= 600,0000/.


Nimetumia mbinu zote za kibaharia nimle kabla sijalipia nimeshindwa.

Wanawake wanachojuwa wao pesa tu..
Ndy upendo.
 
Mimi nimeshafeli ktk kipimo cha pesa.

Kabla sijakula mzigo nimepigwa kizinga cha Kodi miezi 6.

100k mara 6= 600,0000/.


Nimetumia mbinu zote za kibaharia nimle kabla sijalipia nimeshindwa.

Wanawake wanachojuwa wao pesa tu..
Ndy upendo.
na kwanini ulikua unataka kula kwanza😅😅
 
Ndo tumeshambiwa 😁😁😁matan, ila no. 2 nilitumiaga ujanani,Reaction ya mtu ndo husema yote
 

Attachments

  • Screenshot_20220603-171205~2.png
    Screenshot_20220603-171205~2.png
    6.9 KB · Views: 27
Back
Top Bottom