Vipimo kumi vya Uanaume

Vipimo kumi vya Uanaume

Tanzanian Dream

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
274
Reaction score
1,771
Habari wanaharati wenzangu! Juzi tarehe 16/06/2024 ilikuwa ni siku ya Wababa duniani. Sasa tukiwa bado na lile vibe la kukumbukwa 😂🤣 sio vibaya ujipime hapa ili ujue kama wewe ni real au ndio wale feki waliojaa mitaani.

Uanaume ni zaidi ya kuwa na jina na jinsia ya kiume, ni zaidi ya kuwa na six-pack 🏋️. Uanaume sio machine, sio pesa, Uanaume ni spiritual and mental capacity.

Nimeandika uzi huu kwa ajili ya wanaume walio kwenye ndoa au wana familia, ila hata kama bado hujaoa si vibaya, unaweza kuokota mawili matatu yakakusaidia kesho.

Twende sasa kwenye vipimo kumi vya Uanaume:

1. Maono ya Muda Mrefu (Miaka 10, 20...)

Mwanaume ni mbeba maono. Bila maono, mwanaume anakuwa hana msimamo, badala ya kuzikimbiza ndoto zake ataishia kukimbiza wanawake💃🏃.

2. Uaminifu

Hapa namaanisha ule uwezo wa kukaa kwenye ndoa bila kumsaliti mkeo. Binafsi nipo kwenye ndoa miaka 10 na sijawahi kutoka nje ya ndoa. Hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya wanaume lakini inawezekana na huo ndio Uanaume!

3. Majukumu

Waliosema mwanaume ni majukumu hawakukosea kabisa. Mwanamke akikuzidi kipato usijilegeze, pambana mtoto wa kiume. Unaweza kufukuzwa kazi, biashara zikabuma na mkeo akakupiga tafu ni sawa lakini iwe kwa muda tu. Coming back ni moja ya mental toughness ya kiume. Mwanamke akijua wewe ni fighter, atakuheshimu tu hata kama anakuzidi kielimu.

4. Kupiga Mke Sio Uanaume

Rafiki yangu mmoja alimpiga mke wake akapelekwa polisi. Ile mke kusema tu ndio huyu hapa anayenipiga, dah! Jamaa alikula makofi heavy. Wazee wetu hawakukosea kusema mke hapigwi ngumi, anapigwa kwa upande wa kanga. Kama kuna kitu kilinisumbua ni pale mke anakuchokoza maksudi akijua huwezi kumpiga. Baadaye nilipata mbinu flani lakini sitaitaja hapa.

5. Information Genius

Wewe kama mwanaume unatakiwa ujue vitu vingi ili mkeo akikuuliza jambo uwe na majibu, uwe kama Google yake. Ile kusema hujui ni risk kwa sababu atakapo mpata wa kumjibu maswali yake jua umekwisha. Hata kama hujui jifanye mjuaji, wanawake wanapenda mwanaume mjuzi wa mambo sio mshamba mshamba.

6. Sex Transmutation

Wasomaji wa vitabu watakuwa wanaijua hii kitu. Mwanaume hutakiwi kuendekeza sana kile kitendo. Kuna wakati utakuwa mbali na mkeo, jifunze kuwa mvumilivu huo ndio Uanaume. Siku zote kumbuka kuwa "love is more than sex."

7. Uwezo wa Kubeba na Kuficha Mambo Mazito (Kifua)

Wanaume wenzangu, sio kila jambo unamwambia mkeo. Kuna mambo mengine unatakiwa kuyamaliza tu kimyakimya. Sayansi inatuambia kuwa mwanamke ni emotional being, ni kiumbe cha hisia. Ukivurugwa anavurugwa mara mbili yako! Mambo mengine mazito huna haja ya kumweleza. Kwa mfano, kama umefukuzwa kazi usiende kwa mkeo ukiwa kama umechanganyikiwa na kusema sijui tutaishije. Isee utaipoteza ndoa yako. Siku zote kuwa normal, unacho au huna, umepata au umekosa, be just normal huo ndio Uanaume. Acha kupayuka.

8. Uwezo wa Kutimiza Ulichoahidi

Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke anapenda kuahidiwa kitu lakini usipotimiza ahadi anakuwa disappointed sana na atakuona unastahili kupuuzwa. Always timiza ulichosema. Kama huna huo uwezo bora unyamaze kimya. Binafsi nashukuru nilimwahidi wife kumjengea day care nimetimiza 😄.

9. Mwanaume ni Founder

Neno "baba" maana yake ni mwanzilishi, mwasisi au kwa Kiingereza "founder." Hii inamaanisha mwanaume kama baba wa familia anatakiwa kuanzisha project za kifamilia ambazo zitasimamiwa na wanafamilia. Wahindi na Wajapani wanafanya sana hii kitu. Ni wakati wetu na sisi kuwa mafounder wa XYZ & Family Company. Uwezo tunao, tunahitaji uthubutu tu.

10. Uwezo wa Kutengeneza Utajiri wa Vizazi (Generational Wealth)

Ukitaka kupima uwezo wa wazee wetu angalia walichotuachia. Umaskini tulionao hautokani na makosa yetu, ni mnyororo mrefu wa vizazi vingi huko nyuma. Uanaume ni kutengeneza mifumo itakayosaidia kizazi chako kuishi vema hata ukiwa umeshatangulia mbele za haki. Wamarekani wanasema "one for the nation" yaani mafanikio ya taifa au hata familia yanamtegemea mtu mmoja ambaye atajitoa mhanga kwa ajili ya faida ya wengi.

Mwanaume "mtafute Mungu kama utakufa kesho na tafuta mali kama utaishi milele."

Wadau kipimo gani kwako ni mtihani? Hebu funguka hapa ili usaidike. Kama hayo yote yatakushinda basi walau kipimo cha kwanza mpaka cha nne uwe navyo.

Kwa leo ni hayo tu.
 
Habari wanaharati wenzangu! Juzi tarehe 16/06/2024 ilikuwa ni siku ya wababa duniani,Sasa tukiwa bado na lile vibe la kukumbukwa😂🤣sio vibaya ujipime hapa ili ujue Kama wewe ni real au ndio wale feki waliojaa mitaani.
uanaume ni zaidi ya kuwa na jina na jinsia ya kiume,ni zaidi ya kuwa na six pack🏋️,Uanaume sio machine,sio pesa,Uanaume ni spiritual and mental capacity
nimeandika uzi huu kwaajili ya wanaume walio kwenye ndoa au wana familia ila hata Kama bado hujaoa si vibaya,unaweza kuokota mawili matatu yakakusaidia kesho.
Twende Sasa kwny vipimo kumi vya Uanaume............

1.Maono ya muda mrefu(miaka 10,20....)

Mwanaume ni mbeba maono,bila maono mwanaume anakuwa hana msimamo, badala ya kuzikimbiza ndoto zake ataishia kukimbiza wanawake💃....🏃

2.Uaminifu
Hapa namaanisha ule uwezo wa kukaa kwny ndoa bila kumsaliti mkeo,binafsi nipo kwny ndoa miaka 10 na sijawahi kutoka nje ya ndoa,hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya wanaume lkn inawezekana na huo ndio Uanaume!

3.Majukumu
Waliosema mwanaume ni majukumu hawakukosea kabisa,mwanamke akikuzidi kipato usijilegeze pambana mtoto wa kiume,unaweza kufukuzwa kazi,biashara zikabuma na mkeo akakupiga tafu ni sawa lkn iwe kwa muda tu,coming back ni moja ya mental toughness ya kiume,mwanamke akijua ww ni fighter,atakuheshimu tu hata Kama anakuzidi kielimu.

4.Kupiga mke sio Uanaume
Rafiki yangu mmoja alimpiga mke wake akapelekwa polisi ile mke kusema tu ndio huyu hapa anayenipiga,dah!jamaa alikula makofi heavy,wazee wetu hawakukosea kusema mke hapigwi ngumi anapigwa kwa upande wa kanga,Kama Kuna kitu kilinisumbua ni pale mke anakuchokoza maksudi akijua huwezi kumpiga....baadaye nilipata mbinu flani hv ila sitaitaja hapa.

5.information genious
Wewe kama mwanaume unatakiwa ujue vitu vingi ili mkeo akikuuliza Jambo uwe na majibu,uwe kama Google yake,ile kusema hujui ni risk kwasababu atakapo mpata wa kumjibu maswali yake jua umekwisha,hata Kama hujui jifanye mjuaji,wanawake wanapenda mwanaume mjuzi wa mambo sio mshambamshamba.

6. Sex transmutation
Wasomaji wa vitabu,watakuwa wanaijua hii kitu,mwanaume hutakiwi kuendekeza sana kile kitendo,Kuna wakati utakuwa mbali na mkeo,jifunze kuwa mvumilivu huo ndio Uanaume,siku zote kumbuka kuwa"love is more than sex"

7.Uwezo wa kubeba na kuficha mambo mazito(kifua)
Wanaume wenzangu sio kila Jambo unamwambia mkeo Kuna mambo mengine unatakiwa kuyamaliza tu kimyakimya,sayansi inatuambia kuwa mwanamke ni emotional being,ni kiumbe cha hisia,ukivurugwa anavurugwa mara mbili yako!mambo mengine mazito huna haja ya kumweleza,kwa mfano Kama umefukuzwa kazi usiende kwa mkeo ukiwa Kama umechanganyikiwa na kusema cjui tutaishije....isee utaipoteza ndoa yako,siku zote kuwa normal,unacho au huna,umepata au umekosa be just normal huo ndio Uanaume,acha kupayuka.

8.Uwezo wa kutimiza ulichohaidi
Ni ukweli usiopingika kuwa mwanawake anapenda kuhaidiwa kitu lkn usipotimiza ahadi anakuwa disappointed Sana!na atakuona unastahili kupuuzwa,always timiza ulichosema,Kama huna huo uwezo bora unyamaze kimya,binafsi nashukuru nilimwahidi wife kumjengea day care nimetimiza😄

9.Mwanaume ni founder
Neno baba"Father"maana yake ni mwanzilishi,mwasisi au kwa kingeleza"founder" hii inamaanisha mwanaume Kama baba wa familia anatakiwa kuanzisha project za kifamilia ambazo zitasimamiwa na wanafamilia(wahindi na wajapani wanafanya sana hii kitu) ni wkt wetu na sisi kuwa mafounder wa Xyz & familly company,uwezo tunao tunahitaji uthubutu tu.

10.Uwezo wa kutengeneza Utajiri wa vizazi(generational wealth)
Ukitaka kupima uwezo wa wazee wetu angalia walichotuachia,umaskini tulionao hautokani na makosa yetu ni mnyororo mrefu wa vizazi vingi huko nyuma,Uanaume ni kutengeneza mifumo itakayosaidia kizazi chako kuishi vema hata ukiwa umeshatangulia mbele za haki.
wamarekani wanasema "one for the nation" yaani mafanikio ya taifa au hata familia yanamtegemea mtu mmoja ambaye atajitoa mhanga kwa ajili ya faida ya wengi.
mwaunaume "mtafute M-ngu Kama utakufa kesho na tafuta mali Kama utaishi milele".........

Wadau kipimo gani kwako ni mtihani?hebu funguka hapa ili usaidike,Kama hayo yote yatakushinda basi walau kipimo cha kwanza mpk cha nne uwe navyo.

Kwa leo ni hayo tu
chai
 
Hujachepuka kwa muda wa miaka 10, kumgonga mkeo unagonga mara moja moja, Mjomba utakua na shida sehemu ila unatumia kigezo cha uanaume kuficha mapungufu/changamoto fulani.

Pita dna za watoto mapema utakuja kunishukuru
 
Back
Top Bottom