Vipimo kumi vya Uanaume

Vipimo kumi vya Uanaume

Kabla sijakupinga naomba unijibu hil8 swali. Unatumia kigezo gani kusema hap sex imeendekezwa?

Kiukweli katika bandiko point namba 2 na hii namba 6 zinanitia shaka hiyo ndoa yenu imefikaje miaka 10 kwa mentality kama namba 6.
Kujua Kama unaendekeza au la ni suala binafsi ila some folks wanasema 2 times per wk is enough,boxer Mohammed ally aliwahi kusema "anakaa wiki 6 bila tendo Kama sehemu ya maandalizi ya pambano,hicho alichokuwa anafanya Mohammed ally ndio sex transmutation,ni vitu vinavyowezekana kabisa.
 
Kujua Kama unaendekeza au la ni suala binafsi ila some folks wanasema 2 times per wk is enough,boxer Mohammed ally aliwahi kusema "anakaa wiki 6 bila tendo Kama maandalizi ya pambano,hicho alichokuwa anafanya Mohammed ally ndio sex transmutation,ni vitu vinavyowezekana kabisa.
Kwa wanawake wa sasa wasio bikra haiwezekani. Watakusaliti
 
Umeandika vya msingi sana Mkuu, hasa namba 5 imenigusa zaidi na kiukweli mi napenda kujua mengi. Wakati wowote nitauliza lolote na napenda maelezo ya kina.
angalia hikinacho kwani wewe nimwanaume? toka kwenye uzi wetu chuchuwee
 
Mnahangaika tu !

Mwanamke akishafika safari yake utampa nini cha maana ili muendelee kusafiri pamoja!!?

Ukiona anakutii kwa kila kitu ujue bado hajafika safari yake!
 
Habari wanaharati wenzangu! Juzi tarehe 16/06/2024 ilikuwa ni siku ya Wababa duniani. Sasa tukiwa bado na lile vibe la kukumbukwa 😂🤣 sio vibaya ujipime hapa ili ujue kama wewe ni real au ndio wale feki waliojaa mitaani.

Uanaume ni zaidi ya kuwa na jina na jinsia ya kiume, ni zaidi ya kuwa na six-pack 🏋️. Uanaume sio machine, sio pesa, Uanaume ni spiritual and mental capacity.

Nimeandika uzi huu kwa ajili ya wanaume walio kwenye ndoa au wana familia, ila hata kama bado hujaoa si vibaya, unaweza kuokota mawili matatu yakakusaidia kesho.

Twende sasa kwenye vipimo kumi vya Uanaume:

1. Maono ya Muda Mrefu (Miaka 10, 20...)

Mwanaume ni mbeba maono. Bila maono, mwanaume anakuwa hana msimamo, badala ya kuzikimbiza ndoto zake ataishia kukimbiza wanawake💃🏃.

2. Uaminifu

Hapa namaanisha ule uwezo wa kukaa kwenye ndoa bila kumsaliti mkeo. Binafsi nipo kwenye ndoa miaka 10 na sijawahi kutoka nje ya ndoa. Hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya wanaume lakini inawezekana na huo ndio Uanaume!

3. Majukumu

Waliosema mwanaume ni majukumu hawakukosea kabisa. Mwanamke akikuzidi kipato usijilegeze, pambana mtoto wa kiume. Unaweza kufukuzwa kazi, biashara zikabuma na mkeo akakupiga tafu ni sawa lakini iwe kwa muda tu. Coming back ni moja ya mental toughness ya kiume. Mwanamke akijua wewe ni fighter, atakuheshimu tu hata kama anakuzidi kielimu.

4. Kupiga Mke Sio Uanaume

Rafiki yangu mmoja alimpiga mke wake akapelekwa polisi. Ile mke kusema tu ndio huyu hapa anayenipiga, dah! Jamaa alikula makofi heavy. Wazee wetu hawakukosea kusema mke hapigwi ngumi, anapigwa kwa upande wa kanga. Kama kuna kitu kilinisumbua ni pale mke anakuchokoza maksudi akijua huwezi kumpiga. Baadaye nilipata mbinu flani lakini sitaitaja hapa.

5. Information Genius

Wewe kama mwanaume unatakiwa ujue vitu vingi ili mkeo akikuuliza jambo uwe na majibu, uwe kama Google yake. Ile kusema hujui ni risk kwa sababu atakapo mpata wa kumjibu maswali yake jua umekwisha. Hata kama hujui jifanye mjuaji, wanawake wanapenda mwanaume mjuzi wa mambo sio mshamba mshamba.

6. Sex Transmutation

Wasomaji wa vitabu watakuwa wanaijua hii kitu. Mwanaume hutakiwi kuendekeza sana kile kitendo. Kuna wakati utakuwa mbali na mkeo, jifunze kuwa mvumilivu huo ndio Uanaume. Siku zote kumbuka kuwa "love is more than sex."

7. Uwezo wa Kubeba na Kuficha Mambo Mazito (Kifua)

Wanaume wenzangu, sio kila jambo unamwambia mkeo. Kuna mambo mengine unatakiwa kuyamaliza tu kimyakimya. Sayansi inatuambia kuwa mwanamke ni emotional being, ni kiumbe cha hisia. Ukivurugwa anavurugwa mara mbili yako! Mambo mengine mazito huna haja ya kumweleza. Kwa mfano, kama umefukuzwa kazi usiende kwa mkeo ukiwa kama umechanganyikiwa na kusema sijui tutaishije. Isee utaipoteza ndoa yako. Siku zote kuwa normal, unacho au huna, umepata au umekosa, be just normal huo ndio Uanaume. Acha kupayuka.

8. Uwezo wa Kutimiza Ulichoahidi

Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke anapenda kuahidiwa kitu lakini usipotimiza ahadi anakuwa disappointed sana na atakuona unastahili kupuuzwa. Always timiza ulichosema. Kama huna huo uwezo bora unyamaze kimya. Binafsi nashukuru nilimwahidi wife kumjengea day care nimetimiza 😄.

9. Mwanaume ni Founder

Neno "baba" maana yake ni mwanzilishi, mwasisi au kwa Kiingereza "founder." Hii inamaanisha mwanaume kama baba wa familia anatakiwa kuanzisha project za kifamilia ambazo zitasimamiwa na wanafamilia. Wahindi na Wajapani wanafanya sana hii kitu. Ni wakati wetu na sisi kuwa mafounder wa XYZ & Family Company. Uwezo tunao, tunahitaji uthubutu tu.

10. Uwezo wa Kutengeneza Utajiri wa Vizazi (Generational Wealth)

Ukitaka kupima uwezo wa wazee wetu angalia walichotuachia. Umaskini tulionao hautokani na makosa yetu, ni mnyororo mrefu wa vizazi vingi huko nyuma. Uanaume ni kutengeneza mifumo itakayosaidia kizazi chako kuishi vema hata ukiwa umeshatangulia mbele za haki. Wamarekani wanasema "one for the nation" yaani mafanikio ya taifa au hata familia yanamtegemea mtu mmoja ambaye atajitoa mhanga kwa ajili ya faida ya wengi.

Mwanaume "mtafute Mungu kama utakufa kesho na tafuta mali kama utaishi milele."

Wadau kipimo gani kwako ni mtihani? Hebu funguka hapa ili usaidike. Kama hayo yote yatakushinda basi walau kipimo cha kwanza mpaka cha nne uwe navyo.

Kwa leo ni hayo tu.
naona unakaribia kufa kwa msongo
 
Kujua Kama unaendekeza au la ni suala binafsi ila some folks wanasema 2 times per wk is enough,boxer Mohammed ally aliwahi kusema "anakaa wiki 6 bila tendo Kama sehemu ya maandalizi ya pambano,hicho alichokuwa anafanya Mohammed ally ndio sex transmutation,ni vitu vinavyowezekana kabisa.
Man You Are Mad. Yan puchi unalala nayo unaamka nayo uichape mara mbili kwa wiki? Sasa hauna tofauti na mimi ambaye sipo kwenye ndoa na nina uhakika wa kuchakata kila wiki mara 2+ ila naamua kuivungia kwa sababu ya kazi. Hapo sijaendekeza ila najua nikiwa kwenye ndoa naweza kila siku kama siyo kila baada ya siku ya siku mbili.(my own experience)
 
Umeandika vya msingi sana Mkuu, hasa namba 5 imenigusa zaidi na kiukweli mi napenda kujua mengi. Wakati wowote nitauliza lolote na napenda maelezo ya kina.
We Nifah, kama hujui halafu unajifanya unaelezea, utaonyesha ni kwa kiasi gani hujui..!!
 
We Nifah, kama hujui halafu unajifanya unaelezea, utaonyesha ni kwa kiasi gani hujui..!!
Nami sio ‘mwepesi’ pia, huwezi kunidanganya. Hadi nafikia kuuliza ni kwamba najua ila nataka kujua zaidi.
 
Daah, Ukiangalia mambo mengi yamekaa kumfurahisha zaidi mwanamke. Yaani unakomaa ili kumfanyia vitu vizuri mwanamke. Hata kwenye kumpiga mashine isipoenda vizuri unalaumiwa wewe
Ndio hivyo mkubali tu maana hata wanawake mambo mengi wanayoambiwa wafanye kwenye mahusiano au ndoa ni kwa ajili ya kuwafurahisha wanaume tu
 
Nikwambie tu wanawake wa sasa kama hauwaelewi vizuri, wewe wafanyie yote watakusamehe ila kosa au cheating kwao ni mwanaume kutokuwa na hela. Hii kitu hawatakusamehe.
 
Back
Top Bottom