Kipimo cha Uaminifu kimeonekana Kama ndio kigumu zaidi kwa wanaume wengi,Sasa nimeona bora nitoe mbinu kadhaa hapa zilizonisaidia kukaa kwenye ndoa kwa miaka 10,bila kucheat,lengo ni kurudisha ile heshima ya mwanaume iliyopotea.
Wadau hizi ni mbinu ninazozitumia na zimefanya kazi 100%,najua hakuna "one size fits all" lkn hutakosa mawili matatu ya kukusaidia.
1.be transparent.
Kuna baadhi ya mambo unatakiwa kuweka wazi kwa mwenzi wako ie password zako zote kwny simu awe anazijua,rafiki yangu mmoja alikuwa ananishangaa Sana kwasabb mara nyingi akipiga simu yangu anapokea wife!akaniambia unapata wapi ujasiri wa kumwachia mkeo simu yako?..Kama unaweza kuuweka wazi mwili wako kwake unamfichaje simu,😲think big,Mr.
2. Celibacy
Wazee wa Zamani wanajua hii kitu,jifunze kukaa muda flani bila tendo,fanya kama mazoezi,anza na wiki nenda mwezi(ni muhimu kumshirikisha na mwenzi wako) hii itawasaidia kujenga uwezo wa kutawala hisia pindi unapopandisha njegezi😀
3. Fasting(kufunga)
Funga ni muhimu Sana tena Sana,Usisubiri ramadhani au kwaresma,weka utaratibu wako binafsi wa kufunga,funga inaondoa mahomoni ya ajabuajabu mwilini pia inaongeza uwezo wa kutawala matamanio.
4. Pornography
Kwenye list za addition duniani pornography inaongoza,kaa mbali na hii kitu,kuhamsha hisia kupitia watu wengine ni kosa la kiufundi,hata hii kasumba ya vibamia imetokea huko,unajilinganisha vp na mwanaume mwezio!oh G-d wash out this mess.
5. Marafiki wa kike
Wadau hii inategemea mtu na mtu,binafsi tangu nimeoa sijawahi huwa na urafiki na mtoto wa kike,rafiki yangu wa kike pekee ni mke wangu tu.
6.ulevi
Pombe inaharibu uwezo wa kufanya maamuzi sahihi,one of my brothers,siku moja alilewa almanusura abake mke wa mtu,pombe sio nzuri kabisa kwa mwanaume anayejitambua,tangu nimeoa sijawahi onja hata puff moja!
7. Mazingira hatarishi
Mahali ambapo Kuna bar na guest pembeni huwa ni hatari Sana,wapo wengi walioenda kucheki mechi za mpira wakaishia kucheza mechi zao😂
8. Uwe mtu wa sala
Bila kujali imani yako,sala ni muhimu Sana, wakati mwingine unaweza ukatumia kila mbinu na bado uka cheat,kwenye mazingira Kama hayo tunahitaji msaada wa M-ngu.
Kama Kuna mbinu yoyote unaijua ambayo unaweza kushare hapa,fanya hivyo utaziokoa ndoa nyingi Sana zinazoelekea kuvunjika.