Vipimo kumi vya Uanaume

Vipimo kumi vya Uanaume

umeandika vema, ila kwa mtazamo wangu Baba ni yule anayesimama vema kwenye nafasi yake kama Kiongozi wa familia,
- Awe na uwezo wa kuona mbele(maono)
-Asiyeyumbishwa na jambo lolote(Msimamo)
- Mwenye kutimiza wajibu wake katika kutunza familia (muwajibikaji)

Bibilia inasema Baba mwema ni yule mwenye kuacha urithi kwa watoto wake
 
Nilikuwa napitia ukurasa wa Forbes kucheki list ya wanawake matajiri duniani,hiki ndicho nichokutana nacho.....isee namba hazidanganyi
Screenshot_20240619-115113.png

Kipimo no 9 na 10 vinahusika Sana hapa.kuanzisha family projects na uwezo wa kutengeneza Utajiri wa vizazi
Ukicheki hao matajiri kumi ni mmoja tu ndio hajarithi ila wengine tisa,wamerithi kutoka either kwa mume au kwa baba....wanaume M-ngu awape maisha marefu,tuzidi kutengeneza Utajiri utakaodumu vizazi na vizazi.
 
umeandika vema, ila kwa mtazamo wangu Baba ni yule anayesimama vema kwenye nafasi yake kama Kiongozi wa familia,
- Awe na uwezo wa kuona mbele(maono)
-Asiyeyumbishwa na jambo lolote(Msimamo)
- Mwenye kutimiza wajibu wake katika kutunza familia (muwajibikaji)

Bibilia inasema Baba mwema ni yule mwenye kuacha urithi kwa watoto wake
Umepita mulemule,hapo kwny urithi napo mtihani kweli,utakuta mtu ameacha watoto Saba na nyumba moja,hapo hajaacha urithi ameacha bomu💣soon litalipuka na familia itasambaratika.
 
Umepita mulemule,hapo kwny urithi napo mtihani kweli,utakuta mtu ameacha watoto Saba na nyumba moja,hapo hajaacha urithi ameacha bomu💣soon litalipuka na familia itasambaratika.
Na lazima tuelewe elimu sio urithi, unakuta mzazi amekazana "mwanangu sina cha kukirithisha bali nakurithisha Elimu soma kwa bidii" Elimu sio urithi
 
Katika hivyo 10 mimi nimepungukiwa kimoja tu UAMINIFU. Hapa ninapoandika Nina mimba nimeitunga nje yani wife ameshajua. Nilijitahidi Kwa uaminifu miaka yote ila niliteleza Kwa hili. Maneno yamezagaa mtaani hadi wife ameyapata.
 
Na lazima tuelewe elimu sio urithi, unakuta mzazi amekazana "mwanangu sina cha kukirithisha bali nakurithisha Elimu soma kwa bidii" Elimu sio urithi
Huo ni ujanja waliotumia wazee wetu kukwepa hili jukumu zito la kuacha urithi sio kwa watoto tu Bali na kwa wajukuu pia,Kuna wkt yule tajiri manji alisema "Utajiri alionao ni urithi kutoka kwa babu yake,urithi wa baba yake bado hajaugusa!mimi babu yangu hakuna alichoniachia zaidi ya kijitabu cha ujamaa,blacks tuna mwendo mrefu kwny hii kitu.
 
bora wewe babu umemkuta, mimi sijakuta hata kuku
 
Umeandika vya msingi sana Mkuu, hasa namba 5 imenigusa zaidi na kiukweli mi napenda kujua mengi. Wakati wowote nitauliza lolote na napenda maelezo ya kina.
Hongera zako. Kuna hawa wanawake wa uswazi hawa, ni pasua kichwa. Wanajua kila kitu. Ubaya ni kuwa asilimia kubwa ya wanavyojua ni ushauri kutoka kwa mashoga zao siku hizi kutoka social media.
 
Wasomaji wa vitabu watakuwa wanaijua hii kitu. Mwanaume hutakiwi kuendekeza sana kile kitendo. Kuna wakati utakuwa mbali na mkeo, jifunze kuwa mvumilivu huo ndio Uanaume. Siku zote kumbuka kuwa "love is more than sex."
Jambo hili kwa waliooa wanaelewa kwamba,lipo mikononi mwa mke wako
au uchepuke au usichepuke kutegemeana na huduma inayotolewa nyumbani. Niseme hivi japo huendi halitawafurahisha wanawake walio wengi
''Jukumu la kulinda raia na mali zao ni la polisi,baada ya polisi kuonesha kutotoshereza
yakaanzishwa makampuni ya ulinzi binafsi,enzi zile knight support etc'' na maisha yakaendelea.

Ukiwauliza watu wengi wanaochepuka sababu kubwa ya kwanza ni mke wake kuwa
mtoa hoja za kueleza alivyochoka na tendo hilo si chakula huwezi kufa kwa kulikosa
watu wanatafuta vi-knight suport kuepusha migogoro ya hapa na pale
japo kiukweli ni dhambi na haikubaliki.

Katika kusafiri kwangu,unakuta mtu mmesafiri,unashangaa usiku ule ule anatafuta
mwanamke wa kulala naye,unajiuliza ,je huyu hakutoka nyumbani leo?
kumbe unakuta pamoja na kutoka nyumbani,alishakaa miezi bila huduma
alikuwa anatafuta pa kutokea. Pande zote mbili zikijitambua tutavuka salama.
 
Katika hivyo 10 mimi nimepungukiwa kimoja tu UAMINIFU. Hapa ninapoandika Nina mimba nimeitunga nje yani wife ameshajua. Nilijitahidi Kwa uaminifu miaka yote ila niliteleza Kwa hili. Maneno yamezagaa mtaani hadi wife ameyapata.
Mr utakuwa unapitia wkt mgum,naomba M-ngu akuvushe hapo, sometimes tunajifunza kutokana na makosa ila pia nikupongeze kuvuka vipimo 9 sio mchezo pia.
 
Ukishindwa vyote,jitahidi ufuzu vile vinne vya mwanzo.
Hilo la nne ,kuna wanawake wanapenda kupigwa,amini usiamini.

Nakumbuka kuna sehemu nilikuwa naishi,jirani yangu alikuwa anapenda sana kumpiga mke wake,

Siku moja nikaenda kuamulia,nikamshauri mwamba tuondoke maeneo yale atulize hasira,tutarudi baadaye.

Yule mama alitoka akawa anatufuata akisema '' wewe unaingilia ugomvi wa watu unakuhusu nini.."

akaachia tusi moja matata sana, jamaa akasema unaona hiyo jeuri,wacha nimuonyeshe kazi .nilishangaa sana
 
Huo ni ujanja waliotumia wazee wetu kukwepa hili jukumu zito la kuacha urithi sio kwa watoto tu Bali na kwa wajukuu pia,Kuna wkt yule tajiri manji alisema "Utajiri alionao ni urithi kutoka kwa babu yake,urithi wa baba yake bado hajaugusa!mimi babu yangu hakuna alichoniachia zaidi ya kijitabu cha ujamaa,blacks tuna mwendo mrefu kwny hii kitu.
Kwenye mambo ya urithi nitapingana na wewe mpaka kesho. Nimebahatika kuishi hizi nchi za Scandinavia na nika-eperience mambo ya urithi kwa wenyeji.

Niseme tu karibu kila mtoto anaanza kivyake. Kwanza population kubwa ni wafanyakazi tu japo wana maisha mazuri na wanaweza kufanya chochote wanachotaka. Mtoto naye atasoma na kufanya kazi na kuwa na maisha mazuri bila kutegemea wazazi.

Labda utaweza kusema ni kwa sababu system yao ya maisha i.e seriakali zao ni nzuri, jambo ambalo nitakubali. Hivyo basi tunaweza kusema kabisa kuwa tatizo siyo kurithi bali ni uongozi mzuri. Huku kwetu wafanyakzi tunahangaika na biashara za pembeni na miradi kibao kwa sababu tu syetem na uongozi wetu siyo mzuri.
 
Kabla sijakupinga naomba unijibu hil8 swali. Unatumia kigezo gani kusema hap sex imeendekezwa?

Kiukweli katika bandiko point namba 2 na hii namba 6 zinanitia shaka hiyo ndoa yenu imefikaje miaka 10 kwa mentality kama namba 6.
Afadhal na wewe kama umeliona hilo. Huyu kijana wetu anaigizowa maisha. Kifupi mkewe ana akil sana kumzidi.
 
Back
Top Bottom