Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

cc: Tembele... ukitaka kubatasamu usiache pitia huu uzi
 
Last edited by a moderator:
Ha ha pale airport wanashuhudiaga vitimbi aisee kuanzia wasindikizaji mpaka wasafiri hususani wa fastjet
 
kuna siku nimeenda kumchukua mshua usiku nikakuta jamaa wamekuja na DCM mbili na matalumbeta wamekuja kumpokea ndugu yao kwi kwi kwi kwi kwi kwi mimi nilipata ushamba kwenye vile vitololi kumbe unatakiwa ukibonyeze ndio kitembee sasa mimi nilikomaa kusukuma hivyo hivyo hadi kwenye gari da niliteseka kinoma
 
Wale jamaa wanaokagua huwa wanafaidigi sana perfume za watu pia ukizubaa wanachomoa pesa kwenye wallet wakati umeweka kwenye kile kisinia
 
Hahaha mkuu umetisha, dah maza anaita konda kwenye ndege! Dah nimecheka sana
 
Mkuu mimi hii ndege ya chini nilipanda kipindi kile ngorika inafukuzana na buffalo, gari za kwanza asubuhi. Wacha kabisa! Nilipofika korogwe nilishuka mwenyewe
 
Mkuu mimi hii ndege ya chini nilipanda kipindi kile ngorika inafukuzana na buffalo, gari za kwanza asubuhi. Wacha kabisa! Nilipofika korogwe nilishuka mwenyewe

Shukuruni Mungu ajali hazikuwa nyingi kama sasa mngeshasahaulika.
 
Mara ya kwanza nilipanda KLM. Sikuthubutu kula hata kunywa maji kwani nilikuwa naogopa kwenda chooni. Kweli ushamba mzigo. Sikujua hata jinsi ya kupunguza fen baridi ilipozidi. Duh! Acha tu. Halafu safari ilikuwa ya kwenda London.
 
Hivi kwa nini airport KIA unacheck in kwanza alafu ndio unapita security check, kwa hiyo kama una liquid ya zaidi ya 100mls ndani ya begi usioingia nalo kwenye ndege inapita. Airport ya Dar tofauti. Kabla ya kucheck in lazima upitie security.

Hapo mls 100 unaziacha hata kama zipo kwa check in bag. Kwa nini kuna hii tofauti?
 
Mimi mwaka 2013 natoka Kia/dar,..sisahau ile ndege inaruka tu nilihisi km utumbo unageuka..ilinitoka tu Mungu wangu we..,jamaa pembeni kanipiga jicho hilo nikajifanya ile mungu wangu km nilisahau kitu airport kumbe mchechetu,huko juu ndo balaa maana sikuwahi na amani hd inashuka Dar ..dah ushamba bana.
 

Wa Dar wezi tu wanazichukua wao,inatakiwa vilokuwemo ndani Ya cargo vipite tu isipokuwa vya mkononi utakavyoingia navyo ndani,Dar wezi sana wanajifanya wa mjini.
 
We kiboko dohhh....umebugia jibini na sukari teh nimecheka sana!!
 
Ningekuwa na uwezo ningewapiga marufuku wale wafanyakazi wanaoelekeza jinsi ya kufanya in case of emergence..makes you feel like you are one step from death...hates vindege vidogo vya Dar-Mwanza visivyogawa pombe...gotta be intoxicated enough kutowaza kifo safari nzima

Can easily understand Denis Bergkamp
 
teh teh teh uwiiiii mbavu zangu mie mtoto wa marehemu!!!!

Mie nilikusanya vitambulisho vyote mpk vya drs la saba, birth certificate mpk death certificate za wazazi wng nikidhania ukifika kwenye mlango wa ndege unakaguliwa!!

Nikajisemea moyoni wakikataa hiki natoa hiki!!! mweeee ama kweli ushamba mzigo...
 
Mimi mara ya kwanza mwaka 2004 nlipanda precision air.

Sasa tylipokuwa angani nikaenda chooni. Nlivoingia nikaanza kujiuliza " hivi hiki choo ni cha kukaa au kuchuchumaa?". Duh! Akili zangu za uswazi zikanambia chuchumaa.. basi nikaparamia sinki na kushusha mzigo... duh.. noma kweli!

Return trip ndo nlifigure out kuwa ni cha kukaa.. hii sijawahi kumsimulia mtu yoyote... huwa nikikumbuka nacheka sana..
 

Nimeipenda sn hii aisee
 
Hiyo ni Kama mm Pemba to Unguja 2007 ndo Mara ya kwanza achaga tu maana nilikuwa kituko kwa wataliii hewani kutangatanga c unajua kule bahari mkiruka tu kisiwa unajiona kiiiiiiileeeee knazd kilobyte ukubwa ue Na moyo babakoo la sivyo wazungu waliokuwapo nahisi nilikuwa center ya tourism
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…