Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha mkuu umetisha, dah maza anaita konda kwenye ndege! Dah nimecheka sanabaada ya gradu yangu chuo.Tukarudi mkoa na maza. Fastjet ndo imeanza.Nı mara yetu ya kwanza wote.
1. Mama anataka kukaa akakuta juu ya siti sehemu ya mizgo kuna mtu kashaweka wake.Akatia,"wee kondaa,we kondaa wéeh,hebu njoo kwanza"
2. Nikajaribu kwenda choóni japo sijabanwa alimradi tu nione pakoje
3.Facebuk page yangu iliomba poo. Mara checkin in at JKİ Airport. Mara nitupie picha alimradi kila mtu ajue.
4. Tulivofika madreva tax wakaanza kututukana eti "hamna lolote nyie mtakuwa fastjet tu" hapo kisa ni baada ya wao wanatugombania sie hatuna time tunaenda kwny daladala.
5. Jioni napokea simu toka kwa mjomba: "ah mjomba nimeamini ushamba mzigo wa mwiba".Nkamuuliza kwanini? Akasema,"leo sina raha. mama yako kutwa nzima anantambia kwny simu kisa kapanda ndege"
Mkuu mimi hii ndege ya chini nilipanda kipindi kile ngorika inafukuzana na buffalo, gari za kwanza asubuhi. Wacha kabisa! Nilipofika korogwe nilishuka mwenyeweMie siku napanda arusha to Dar za ardhini inaitwa ngorika ilivyokuwa inakimbia nilidhani tunaenda kwa ISRAELI kila akitaka ku overtake nafunga macho.
Chakula cha mombo kiliniondoa stress kwani sikutegemea kula wali nyama wa 2000 wenye nyama ya ukweli. Muda si mfupi tumeanza safari tumbo likaanza nilitamani wanishushe nimalizie kwa miguu nilipoambiwa utashushwa wami nilijikaza kisabuni
Mkuu mimi hii ndege ya chini nilipanda kipindi kile ngorika inafukuzana na buffalo, gari za kwanza asubuhi. Wacha kabisa! Nilipofika korogwe nilishuka mwenyewe
Hivi kwa nini airport KIA unacheck in kwanza alafu ndio unapita security check, kwa hiyo kama una liquid ya zaidi ya 100mls ndani ya begi usioingia nalo kwenye ndege inapita. Airport ya Dar tofauti. Kabla ya kucheck in lazima upitie security. Hapo mls 100 unaziacha hata kama zipo kwa check in bag. Kwa nini kuna hii tofauti?
We kiboko dohhh....umebugia jibini na sukari teh nimecheka sana!!Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.
Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.
Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.
Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.
Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
Mie siku napanda arusha to Dar za ardhini inaitwa ngorika ilivyokuwa inakimbia nilidhani tunaenda kwa ISRAELI kila akitaka ku overtake nafunga macho.
Chakula cha mombo kiliniondoa stress kwani sikutegemea kula wali nyama wa 2000 wenye nyama ya ukweli. Muda si mfupi tumeanza safari tumbo likaanza nilitamani wanishushe nimalizie kwa miguu nilipoambiwa utashushwa wami nilijikaza kisabuni
Hiyo ni Kama mm Pemba to Unguja 2007 ndo Mara ya kwanza achaga tu maana nilikuwa kituko kwa wataliii hewani kutangatanga c unajua kule bahari mkiruka tu kisiwa unajiona kiiiiiiileeeee knazd kilobyte ukubwa ue Na moyo babakoo la sivyo wazungu waliokuwapo nahisi nilikuwa center ya tourismMimi mwaka 2013 natoka Kia/dar,..sisahau ile ndege inaruka tu nilihisi km utumbo unageuka..ilinitoka tu Mungu wangu we..,jamaa pembeni kanipiga jicho hilo nikajifanya ile mungu wangu km nilisahau kitu airport kumbe mchechetu,huko juu ndo balaa maana sikuwahi na amani hd inashuka Dar ..dah ushamba bana.