Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

aiseee haya mambo ya ndege ni vema hata ku-google au kuchek kwenye YOUTUBE ili kujiridhika kabla mtu mzima hujaaibika ndegeni
 
Shukrani zimuendee PRINCE kwa kuwekeza kwenye FASTJET angalau na sisi tunakwea pipa kwa bei nafuu.
 
Hata kama utakuwa rubani huwezi kufikisha masaa laki moja

Wandugu Masanja....kuna pilot mmoja mkongwe sana alikuwa anaitwa Mazura huyu kafanya kazi muda mlefu sana toka miaka ya 60s enzi hizo kwenye mgodi wa Almas wa Williamson Diamnds Shinyanga...nae baadae miaka ya 80s kitu kama akaamia ATC.Kwa muda uliosemwa wa masaa yale yapatayo miaka 11...Kwa mtu kama Mzee Mazura yule anaweza kuwa nusu ya umri wake ameuendesha akiwa angani.Ndio kusema Mzee yule anaweza kuwa ametumia miaka 35 akiwa ni Pilot.Ni mmoja wa Mapilot wakongwe na wazuri sana Nchini Tanzania.

Kwa waliozaliwa Williamson ndege haikuwa kitu cha ushamba kwa walio wengi...manake siku nyingine mapilot mara kwa mara inasemekana walikuwa wanakusanya watoto mitaani na kwenda kuwapakia kwenye ndege na kuzunguka nao...maeneo kama Mwanza kisha kuwarudisha Willimson-Mwadui.
 
ungekuwa kikojozi ungekoma ubishi

Siziga hata Leo hii uki check inn counter pale Na ukapotea kwenye lounge ndege haiondoki!! Hadi wakupate! Maana upo close by Na confirmed unasafiri Na umesha book seat !! Ukiwa last counter!!!
 
Ndege ni kitu ambacho kwa kweli kila nikiwaza napata raha ya ajabu ikitokea ndo nasafiri na ndege yaani hata njaa sisikii kabisa, usingiz ndo sipati
 

Kama wale waliopanda ndege ya Malaysia,kama angetokea mmoja sidhani km ungetamani kupanda ndege tena;Japo utajipa moyo ILIKUWA NI AJALI,we acha kiherehere;mbona hata kupanda bus ni raha tu
 
Jamanii ata mimi sijawah naomba mnielekeze kuanzia airport nn kinatakiwa na kip haitakiwi mkanda unafungwaje namba za siti zimeandikwa wapi

Nenda kwenye maofisi ya mashirika ya ndege utajua taratibu;kwa ujumla maelekezo yote yanatoka ndani ya ndege ukipanda
 
Siziga hata Leo hii uki check inn counter pale Na ukapotea kwenye lounge ndege haiondoki!! Hadi wakupate! Maana upo close by Na confirmed unasafiri Na umesha book seat !! Ukiwa last counter!!!
Sio haiondoki. Utatafutwa kwa kutangaziwa kwenye spika mara 3. Usipoitikia/onekana wanaondoka.
 

Daah umetisha sana aisee huna mchezo na pesa
 
KWELI IMETOKEA
Mshikaji mmoja alikuwa anamzimia sana Bob Nester marley. Mshkaji anajihusisha na uchimbaji wa madini alikuwa ameahidi hata kama hana kiwanja nyumba gari ila akipata tu mkwanja lazima a fly kwenda kuzuru kaburi la mzee mzima. Mungu akambariki mwaka juzi kavuta bingo msela kakwea pipa hadi jameca.

Nakutia moyo wewe mwenye ndoto za kukwea pipa yote yanawezekana usikate tamaa angali bado unapumua. Mungu kwanza na mengine yanawezekana.
 
usiombe ukutane na mwanafunzi/bitoz ndo siku ya kwanza kupanda ndege (fastjet), niliwahi kiupanda na toz mmoja na kidemu chake pale KIA ndo wamefunga shule wanarudi Dar, yaani jamaa earphone masikioni, huku kamkumbatia demu wake, picha kila dakika hadi kero
 
Hivi kwa nini Madereva taxi pale JNIA fastjet ikitua wala hawaangaiki kuwauliza abiria kama wanachukua taxi? jamani bure mbaya sana iaseee!
 
bado cjawahi kupanda pipa sijui itakuweje ngoja nifatilie ushamba ntapata somo kidogo,
 
Jambo sana ndugu zangu.Kuna mtu anae jua gharama za kusafiri kwa fast jet from Dar to mwanza.Msaada please,
 
Jambo sana ndugu zangu.Kuna mtu anae jua gharama za kusafiri kwa fast jet from Dar to mwanza.Msaada please, hasanten
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…