Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sikumbuki vizuri,ila nina zaidi ya masaa laki moja hewani
Hata kama utakuwa rubani huwezi kufikisha masaa laki moja
ungekuwa kikojozi ungekoma ubishi
mi naitamani sana KLM aisee mara nyingi huwa nalionaga pale KIA likitua na kupaa Nalitamani nilipande siku moja nikiwa naenda huko mbali sana sijui RUSSIA sijui wapi huko, yaani hapa najichanga tu nizushe trip ili mradi nikwee dude la KLM, wazungu wanafaidi sana aisee
Jamanii ata mimi sijawah naomba mnielekeze kuanzia airport nn kinatakiwa na kip haitakiwi mkanda unafungwaje namba za siti zimeandikwa wapi
Sio haiondoki. Utatafutwa kwa kutangaziwa kwenye spika mara 3. Usipoitikia/onekana wanaondoka.Siziga hata Leo hii uki check inn counter pale Na ukapotea kwenye lounge ndege haiondoki!! Hadi wakupate! Maana upo close by Na confirmed unasafiri Na umesha book seat !! Ukiwa last counter!!!
Ilikuwa 2012 ndo kwa mara ya kwanza napanda ndege niko kwenye FASTJET ya kutoka MWANZA kuja DAR, nilikuwa na mihemuko balaa, niliiwazia hii safari kwa muda wa wk 2, nakumbuka nilipiga picha kila sehemu nilipopata Aiport, nje ya ndege na ndani ya ndege mpaka leo zipo nimezihifadhi kwa ajili ya wanangu, wajukuu na vitukuu.
View attachment 245577
Kali zaidi tulipokuwa hewani ndani ya NDEGE nikamwita mhudumu nimwulize wapi TOILET, akanionyesha, nikaenda japo sikuwa na haja yoyote nikaishia kutema mate kwenye sink la chooni , kuflash, nikanawa mikono, nikasukutua mdomo na kutoka zangu.
View attachment 245578
Tulipotua pale JKNIA asubuhi saa 09:40 akili ndo ikazidi kupagawa baada ya kuyaona yale MADEGE mengine makubwa makubwa yanapaa na kutua, nikaashangaa kama dakika 15 hivi na kutoka zangu nje, pale nje sasa madereva TAX full kushupalia, wapi kaka, twende na hii, bei poa tu, kwenda kuuliza bei toka pale mpaka TEGETA sh ngapi eti naambiwa elfu 35, nikajisemea moyoni shwaiiiiinnn sana, wakati nimetoka Mwanza mpaka Dar nauli elfu 32 tena kwa NDEGE halafu kutoka hapa mpaka TEGETA elfu 35, nikaachana nao na kwenda kupanda zangu daladala kwa nauli ya sh 950 ila nyumbani niliingia 13hr shauri ya foleni.
View attachment 245515