Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Dah! Ndege ina speed jamani nilipanda AURIC AIR toka Njombe to Iringa ile naingia tu nasogea kwenye siti yangu ili nikae naambiwa "wa kushuka Iringa", nikadata nauliza wa kushuka Iringa mnamaanisha nini, yule kaka akasema tushafika Iringa, sikuonja hata siti ya ndege ikanibidi nishuke maana tuliisha fika Iringa, duh! ndege inakimbia jamani!
 

Hahahahaha#sina mbavu mie#
 
Ilikuwa mwaka 2002 toka Mza-Dsm, sikupata tabu yoyote, ila tu nilishindwa kula chakula cha "kizungu" Sandwich, tushazoea maharage na sangara. Hii mikate na majani kama mabichi ktkt ndio vitu gani, nikaona usiwe tabu, nikafunika kiboksi nikanywa soda.
 
Mie siku napanda Arusha to Dar za ardhini inaitwa ngorika ilivyokuwa inakimbia nilidhani tunaenda kwa ISRAELI kila akitaka ku overtake nafunga macho.

Chakula cha mombo kiliniondoa stress kwani sikutegemea kula wali nyama wa 2000 wenye nyama ya ukweli. Muda si mfupi tumeanza safari tumbo likaanza nilitamani wanishushe nimalizie kwa miguu nilipoambiwa utashushwa wami nilijikaza kisabuni
 
Bukoba - Mwanza.....vile vindege vidogo... hiyo siku kulikuwa na mvua sana asubuhi.. Wakati tunaingia kwenye ndege tukaambiwa tuzime simu zetu ila kuna watu nikawaona wanaendelea kutumia simu wakiwa ndani kabla hatujaondoka...ile tunaondoka tu airport kandege kakaanza kuyumba yumba mara pailot akarudia tangazo watu wote wazime simu...mimi simu yangu nilitoa na betri kabisaaaa..
 
Ombea usianzie kwenye ndege za jeshi,utajuta! But saiv naona kwaida tu kwenye ndege za aibiria na jeshi pia

Dah umenikumbusha ndugu yangu. Mwaka 2003 tupo Airport Tabora tunasubiri ndege ya jeshi ilipofika nikaona inatetema kwenye runway..iliposimama askari akachukua kitu kama chuma akaweka kwa mkiani ili ndege isitikisike nikasema leo kazi ipo basi hata kupanda nikawa muoga.
 
Mara ya kwanza kusafiri nilikuwa naenda Sehemu hivi kupitia Paris. Ila siku hiyo ndege ya Air France ikawa imeharibika na hivyo ikaja ndege ya Madagascar Airlines Boeng 747, mzinga wa pipa.

Uzuri ni kuwa nilipigwa shule nyumbani nzuri sana jinsi ya kufunga mkanda, kulaza kiti na kukirudisha, kufungua headphones na kuzitumia na wapi zipo tundu za kuchomeka.

Ila nakaa, pembeni kuna Dada wa Kiganda na Mudhungu wake, akawa anahangaika jinsi ya kufunga mkanda, bwana wake akamsaidia kufunga. Sijui siku hizi anajisikiaje akikumbuka ushamba huo wa siku ya kwanza.

Kasheshe ilikuwa wakati wa kula. Ila Mungu bariki nilishaambiwa kuwa kuna vikaratasi vya kufuta uso na asubuhi mnaletewa taulo za motomoto kufuta uso pia. Msosi kufika, maajabu matupu kwani nusu ya vyakula navifahamu na nusu sivifahamu. Mie na kundi langu lote tukawa tumekubaliana tutakula kila kitu na hatubakizi hata kama watakuwa CHURA wa Kifaransa maana hawa jamaa WALA VYURA hawakawii kumlisha mtu nyama zao.
Kila kitu kilienda safi ila ikawa kasheshe kuzila OLIVE ila nikajikaza nikazila. Kulikuwa na nyama nyeusi nyeusi, sikujali ni nini, nikazila bila huruma. Mwisho vikabaki vipaketi vitatu. Kimoja kukifungua ni Sukari, nikaibugia. Kingine kufungua ni jibini, nikaila bila huruma. Cha mwisho kufungua (nilikuwa nafahamu unafungua kwa kuvunja ncha iliyochomoza) ikawa kumbe maziwa ya kwenye kahawa ambayo nilishaimaliza mapema sana bila sukari wala maziwa. Basi nikaangalia kushoto kulia hakuna anayeangalia, nikabugia. Mwisho nikasema hata kama Mjinga fulani kaniona, sijali maana hatakuja kuniona tena. Mwisho sahani yote ikawa tupu na wakaja akina dada kuchukua makasha matupu.

Kuna jamaa alikuwa anawasumbua akina dada kuagiza pombe basi ilipofika saa 9 usiku, wakamuita na kumuonyesha Friji la Pombe lilipo na wakaenda kulala. Jamaa alipofika Paris, alikuwa anatambaa kutoka ndani ya ndege.
 
this is hilarious lol!!!
 
==> Hii nayo kiboko mkuu, ulibugia cream?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…