Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)



Ndege inatua bila kutoa matairi? Ulishawahi kupanda ndege ıkatua bila kutoa matairi??
 
inatokea matairi yanagoma kutoka na mara nyingi hutokea mtiti ama ajali ya ndege kulipuka kwa moto kutokana na msuguano wa lami na bodi ya ndege kama fire wasipokuwa makini hali huwa ni mbaya sana
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
Aaaaaa!!!! mbavu zangu jamani. Wenzako mpaka mabasi ya mwendokasi yanatutia ushamba, sembuse pipa.
 
ATC mkianza msitusahau Katavi (uwanja wa ndege upo) MZee wetu alijitahid akatujengea japo ndege ndo haziji kwa wingi kama tulivotarajia
 
Heri KLM waanze safari za Bukoba maana tumechoka kelele za wasukuma kwenye fastjet
 
Watanzania tuamke jamani maana tumelala mno. Mtu akitoka sana kaenda China au Dubai kununua chupi & malapulapu mengine kuja kuuza kariakoo. Fungukeni nendeni mkafundishe kiswahili marekani hukooo
 
Watanzania tuamke jamani maana tumelala mno. Mtu akitoka sana kaenda China au Dubai kununua chupi & malapulapu mengine kuja kuuza kariakoo. Fungukeni nendeni mkafundishe kiswahili marekani hukooo
Wewe ndio uamke. Watu wameanza kwenda China kununua bidhaa juzi juzi, huko Marekani watu ndio walipoanzia safari.
 
Reactions: Qj_
Infact, wahaya wengi tuna uwezo hata wa kukodi ndege zitupeleke Bukoba direct mkituona huko fastjet ni ktk kuonyesha uzalendo na wala vumbi wa Mwanza /Musoma.
Cc. Rugemalira, Home boy.
 
mhmhmhmhmh ngoja nisubiri nikienda mbele nije nisimulie
 
Siku ya kwanza kupanda ndege kwa upande wangu, kila sehemu nilikuwa najipiga picha, nakumbuka nilijirekodi video huko kwenye mawingu... Haaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…