Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Mi bado kidogo kuachwa na ndege pale Adis Ababa
 
mgesa unapandaje Ethiopian Airlines ndege za MIPOPO na WACHINA +WAKINGA? Panda ndege za maana wewe! Wakolaa.
 
Mimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
[emoji28] [emoji28]
 
Nakumbuka tena kiroja kingine cha ushamba wangu wa kupanda ndege. Baada ya ile safari ya kwanza kabisa toka DSM to MZ niliendelea kusafiri kwa ndege mara kadhaa lakini ushamba haukwisha haraka. Siku moja nilikuwa natoka Ars kwenda Dsm. Nilikuwa nimekunywa maji mengi hivyo hapo katikati nikaenda washroom. Nilipomaliza kilichonipeleka nikataka kuflush choo. Nikatafuta kamba au handle ya kuvuta maji yatoke sikuona. Niliona buttons mbili au tatu hivi. Hee nikaogopa kubonyeza yoyote! Kisa? Eti niliogopa usikute button nitakayogusa isije kufungua mlango wa nyuma halafu nianguke nje!!!!!! Kweli ushamba mzigo!!!!
(Nina kisa kingine lakini acheni kwanza niwahi kazini. Hapa kazi tu!!!!!)
 
Hahahaaaaaa teh teh nimechekaa sana mpka mdogo wangu ananiuliza huko chumbani unacheka na nani na watu wote hawapo. Kusema kweli you made my day brooo
 
Usafiri mzuri,ila hauzoeleki hasa pale kwny mko hewani dege linatikisika uwiii huwa napata ganzii..mda wa kupaa pia
 
Mimi ilikuwa 2009 pale JNIA naelekea Ethiopia wakati niko kwenye escaletor ile nafika juu nikawa nimetulia tu kama gogo ilibakia almanusura nidondoke sikujua kuwa pale mwishoni una step ili kuiacha,anyway it was a lesson.
Escalator mpaka kesho ni ushamba wangu hata nizikute wapi huwa siwezi zitumia jmn loh,sijui nifanyeje,..nlitumia once tu nikaona siyawezi mhh ushamba mzigo
 
Naomba tushee experiences siku yako ya kwanza kupanda ndege ilikuwaje?
-inapoanza kukimbia kwenye run way
-inapo take off
-inapokuwa mawinguni
-inaposhika

Ulipokuwa ndani ulijishughulisha na nini?
Nina safari ya Angola, roho ina ninduda dunda hapa!
 
Mawingu nilibahatika kuya..... tangu udogoni.

Hadi napata akili imekuwa mazoea.

Na chombo cha majini (baharini) nilibahatika tangu udogoni.

Hadi napata akili imekuwa mazoea
 
Naomba tushee experiences siku yako ya kwanza kupanda ndege ilikuwaje?
-inapoanza kukimbia kwenye run way
-inapo take off
-inapokuwa mawinguni
-inaposhika

Ulipokuwa ndani ulijishughulisha na nini?
Nina safari ya Angola, roho ina ninduda dunda hapa!
Hapo Nmeona ni safari ya Angola..
Asante mkuu tumefahamu Unaenda nje ya nchi for the first time...
 
ninda chit-chat kuna uzi huu...tavunjika mbavu sana...pia utjifunza mengi sana...period
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…