Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Escalator mpaka kesho ni ushamba wangu hata nizikute wapi huwa siwezi zitumia jmn loh,sijui nifanyeje,..nlitumia once tu nikaona siyawezi mhh ushamba mzigo
Mimi nadhani inabidi ziboreshwe zaidi
 
Mi wala sikuwa na mcheche. Nadhani kwavile haikuwa ukubwani, hahahhhaaaa!!!. Ila kuna siku tunatoka site (mgodini), kuna jamaa yangu alikuja kwenye interview. Kwahiyo siku anaondoka na mimi ndiyo naenda likizo. Tukapanda wote kindege cha watu 12 toka site. Hichi kindege (huwa nakiita kibajaji) sometimes mkiwa hewani kinajiachia kama pangaboi limezimika vile. Lazima ung'ang'anie siti mazee. Basi jamaa yangu ilikuwa full kung'ang'ania siti. Akinicheki mi nimeuchapa usingizi mwanzo mwisho. Ile karibia tufika Dar akaniuliza ''we jamaa umewezaje kulala?''. Mi nikabaki nacheka.
Sasa ulimuonaje jamaa kama ameng'ang'ania siti wakati ulikua umelala.??!
 
DAR-SYDNEY masaa 23 hamu ya ndege iliniisha.
Halafu sijui kaanini, sehemu unazozichukulia kuwa ni karibu ukisikia majina yake ndio huwa mbali kuliko sehemu unazoweza kuona ni mbali ukisikia majina yake, mfano china au u. S. A
 
Halafu sijui kaanini, sehemu unazozichukulia kuwa ni karibu ukisikia majina yake ndio huwa mbali kuliko sehemu unazoweza kuona ni mbali ukisikia majina yake, mfano china au u. S. A
Acha kabisa ndugu, u r very right. Fikiria ndani ya nchi moja kwa ndege ni zaidi masaa 5 na nusu (SYDNEY to BRISBANE zote Australia). Halafu unakaa huko kijijini kwenu unajidanganya Tanzania ni nchi kubwa na tajiri sana. TEMBEA UKAONE watu wa shoka wanavyopiga kazi kujiletea maendeleo. .
 
Ukitaka kujua kuwa kila mtu humu JF kapanda ndege, hebu pita kwenye hii thread hususani pitia comments za mwanzo...!

😀
 
Ila Mwarabu kaamua kwa moyo mmoja kuwekeza kwenye biashara ya Ndege EMIRATES, Qatar na Etihad, Turkish & kidogo Royal Air Maroc . Sisi tutafika lini huko?
 
Ila Mwarabu kaamua kwa moyo mmoja kuwekeza kwenye biashara ya Ndege EMIRATES, Qatar na Etihad, Turkish & kidogo Royal Air Maroc . Sisi tutafika lini huko?
Sisi tujikite na kuwekeza kwenye viwanda, ndege ina changamoto sana. Pia tuwapige Promo wasanii wetu akiwemo Bilionea Manfongo.
 
Sijui kwa nn bado watu wanasafiri maelfu ya kilometa kwa barabara na kuna uwezo wa kukwea "mwewe" kutunza muda na kupunguza likeliness ya ajali.
Ajali ya ndege ni adimu ila ikitokea ni catastrophic
 
Raha ya kusafiri umbali mrefu uwe na washkaji zako 3 ena enjoy! Nchi nayo itamani sasa ni kwenda Russia na Israel
 
Ila wasukuma Hawataki ujinga wakiwa kwenye ndege. Wanapiga selfie mpaka juice wanayogaiwa
 
Dreamliner habari nyingine ile aisee. Yaani nilipandaga zile za Kenya Airways raha mpaka kumoyo. Kioo unaweza kuweka mpaka tinted!
 
Duuh kwl maish 2natofautia wkti nyny mnacfiana kpnd ndg kn mtnzani hjui ht kpnd Yuutong bac hlaf mnasma mzee kbana
 
Back
Top Bottom