princess ariana
JF-Expert Member
- Aug 19, 2016
- 9,245
- 18,347
Usijali mrembo, faza haus analeta vyombo vingine vi4 vya maana mbona ntakukatia tu tiketi one day.mimi ndo hata mlango wa airport sijauona nna miaka kadhaa sijaelekea ukonga[emoji23], ndege naziona angani tu!!!
na kwenye movie na media!!!
umasikini mbaya sana!!
Unapanda ndege ya shirika gani? Mi niliona kawaida ila ikiwa angani (mawinguni) kuna wakati inakuwa kama umepanda gari linalopita kwenye mashimo, hali hiyo kwenye denge wanaita turbulence. Inaogopesha kama ni mara yako ya kwanza.Naomba tushee experiences siku yako ya kwanza kupanda ndege ilikuwaje?
-inapoanza kukimbia kwenye run way
-inapo take off
-inapokuwa mawinguni
-inaposhika
Ulipokuwa ndani ulijishughulisha na nini?
Nina safari ya Angola, roho ina ninduda dunda hapa!
Usihuzunike kwa kutopanda ndege,Bombadia zipo utaondoa huo ushambamimi ndo hata mlango wa airport sijauona nna miaka kadhaa sijaelekea ukonga[emoji23], ndege naziona angani tu!!!
na kwenye movie na media!!!
umasikini mbaya sana!!
hahahahahhahMimi ilikuwa 2007 nilipata ride ya kwenda serengeti, nikapiga suti na scaf; kuingia kwenye ndege (hizi ndogo za watu 12) nakuta watu wamevaa simple sana kwa kuwa wanaenda bush; nilijisikia vibaya sana...
Hizi sound... braza[emoji3] [emoji3] [emoji3]Dah! ndege ina speed jamani nilipanda AURIC AIR toka Njombe to Iringa ile naingia tu nasogea kwenye siti yangu ili nikae naambiwa "wa kushuka Iringa",nikadata nauliza wa kushuka Iringa mnamaanisha nini,yule kaka akasema tushafika Iringa,sikuonja hata siti ya ndege ikanibidi nishuke maana tuliisha fika Iringa,duh! ndege inakimbia jamani!
Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka saa 12 asubuhi (ndege ndo inapaa) mimi nikajipa kama dakika 20 kutoka home Tabata mpaka Airport, nikidhani ni kama Mabasi ya Mkoani pale Ubungo stendi duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichokaje. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege.
**NEW DEVELOPMENT
Mwezi Juni 2015 nilipata safari ya kwenda CAMEROON (kwa hisani ya Watu wamarekani USAID) sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....
****MPYA ya 2016
Mwezi Januari nilienda NEW DELHI duuh pale airport hakuna sijui kutangaza wala nini ni KIMYA KIMYA tu ukisubiri matangazo utastukia ndege ishakuacha.
HAKIKA USHAMBA MZIGO!
Wewe hujawahi kupanda bado?Sasa unaturingishia kwamba umepanda sana ndege?Kweli ushamba mzigo.