Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sure. Wamanga wanajua biasharaEmirates ndo Wana huduma nzuri
Sure. Emirates, Etihad, Qatar, Kuwait, Gulf Air na Oman Air wapo vzrSure. Wamanga wanajua biashara
😄😄😄Mie mara ya kwanza kupanda ndege nilitoka Dsm kwenda Mwanza. Process nzima hadi niingie kwenye ndege ilikuwa 'shughuli'. Nilikaa upande wa dirishani, tulipopita Ngorongoro crater eti sikuthubutu kuchungulia nje. Kisa? Niliogopa eti nikichungulia naegemea upande mmoja hivyo nikaona kama vile ndege italalia upande ule na kuanguka! Ama kweli ushamba ni kazi!
Hongera, hongera tenaMara ya kwanza nilikuwa natoka Dar kwenda Mwanza, wakati huo nina mimba ya 5 months lakini tumbo lilikuwa kubwa sana. Nimefika pale naulizwa una permit ya daktari kusafiri maana unaonekana mimba kubwa basi kwa kuogopa nitaachwa nisisafiri na sina doctor permit nikadanganya nina mimba ya miezi 3 ila ni triplets ( mapacha watatu ) nikapita na hongera nyingi.
Dubai Wana ukwasi ila hawaleti misaada Ikwiriri tuchimbe visima vya maji na Kujenga Madrassa, whyMkuu acha nuksi EK ndio usafiri wangu ingawa nilikuwa siipendi, mpaka ATC itakapoanza kuruka nje ya nchi. December nilipiga katrip Dubai na Boeing 747-300-ER, hili dude ni kubwa kasheshe mkifika Dubai inabidi lizunguke kidogo kabla ya kutua maana kuna traffic,basi hapo mara limekata kushoto mara limekata kulia unaona dunia chini inapanda na kushuka na ule mji ulivyokuwa mzuri unaona mistari ya taa tu!
vipi mkuu, ushafika Qatar?2022 inshallah naenda Qatar World Cup
Wana priorities zaoDubai Wana ukwasi ila hawaleti misaada Ikwiriri tuchimbe visima vya maji na Kujenga Madrassa, why
Pole sana. Wauza majenereta ndo wakati wao huutangu mtetezi wa wanyonge (fastjet) atolewe sina uhakika nitapanda tena ndege lini
🤣🤣🤣 Siyo serious bhna uanzingua mkuu dah nimecheka hakiMie mara ya kwanza kupanda ndege nilitoka Dsm kwenda Mwanza. Process nzima hadi niingie kwenye ndege ilikuwa 'shughuli'. Nilikaa upande wa dirishani, tulipopita Ngorongoro crater eti sikuthubutu kuchungulia nje. Kisa?
Niliogopa eti nikichungulia naegemea upande mmoja hivyo nikaona kama vile ndege italalia upande ule na kuanguka! Ama kweli ushamba ni kazi!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣tangu mtetezi wa wanyonge (fastjet) atolewe sina uhakika nitapanda tena ndege lini
Viroja vya siku ya kwanza kupanda ndege.....!!!!Ilikuwa 2012 ndo kwa mara ya kwanza napanda ndege niko kwenye FASTJET ya kutoka MWANZA kuja DAR, nilikuwa na mihemuko balaa, niliiwazia hii safari kwa muda wa wk 2, nakumbuka nilipiga picha kila sehemu nilipopata Aiport, nje ya ndege na ndani ya ndege mpaka leo zipo nimezihifadhi kwa ajili ya wanangu, wajukuu na vitukuu.
View attachment 245515
Kali zaidi tulipokuwa hewani ndani ya NDEGE nikamwita mhudumu nimwulize wapi TOILET, akanionyesha, nikaenda japo sikuwa na haja yoyote nikaishia kutema mate kwenye sink la chooni , kuflash, nikanawa mikono, nikasukutua mdomo na kutoka zangu.
View attachment 245577
Tulipotua pale JKNIA asubuhi saa 09:40 akili ndo ikazidi kupagawa baada ya kuyaona yale MADEGE mengine makubwa makubwa yanapaa na kutua, nikaashangaa kama dakika 15 hivi na kutoka zangu nje, pale nje sasa madereva TAX full kushupalia, wapi kaka, twende na hii, bei poa tu, kwenda kuuliza bei toka pale mpaka TEGETA sh ngapi eti naambiwa elfu 35, nikajisemea moyoni shwaiiiiinnn sana, wakati nimetoka Mwanza mpaka Dar nauli elfu 32 tena kwa NDEGE halafu kutoka hapa mpaka TEGETA elfu 35, nikaachana nao na kwenda kupanda zangu daladala kwa nauli ya sh 950 ila nyumbani niliingia 13hr shauri ya foleni.
View attachment 245578