Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Viroja: Siku ya kwanza kupanda ndege (ushamba mzigo)

Nope....
Kwa hizi ndege zetu za ndani ni kimoja...(kwa ambazo nimepanda mimi)

Nadhani Toilets zaidi ya Moja zipo kwenye ndege kubwa...
Nikipanda tena lazima niende sema kwenda ndege inatembea mmmh labda ikitua ndo nitakimbia chap.
Oh kumbe ni vidogo? Basi hapo hakuna kusindikizana.
 
Nikipanda tena lazima niende sema kwenda ndege inatembea mmmh labda ikitua ndo nitakimbia chap.
Oh kumbe ni vidogo? Basi hapo hakuna kusindikizana.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ni unaingia mwenyewe....

Mwenyewe ndege ikiwa inatembea hata kusimama siwezi...

Wale wanaoendaga Chooni ndege ikiwa juu wana moyo aisee...
 
Mbona kimo humu? Ni mengi yalitokea siku hiyo ila kubwa kuliko yote usiku sikulala, lakini pia niliwahi kuliko kiumbe yeyote yule ,si wanasemaja 2hr? Basi mimi 5hrs before nilikuwa pale.

Utamu wa ndege haujawahi mwacha mtu, na ukubwa huu ndege nimepanda mara kibao ila naona vioja haviishi.

Mwaka jana kuna sehem nilikuwa naenda basi niko airport kuelekea dar basi kuna msanii mmoja wa kile nae kalikuwa kanaelekea dar amefika pale alikuwa kananukia perfume kali balaa kalipopita kila mmoja airport alitamani ajuwe ni perfume gani kapaka.

Nikasema hapana hii chimbo ya hii perfume naijuwa nikampigia mwarabu huyu kaka anauzaga perfume za kupima akikuchanganyia perfume lazima ukubali.

Basi si ndo akaniambia huyu msamii wakati anaelekea airport alipitia dukani kwake akasetiwa ndo akaelekea airport.

Nikajisemea nextime airport nzima watanikoma😂😂😂

Juzi tu kakatokea ka safari ka chap dar,nikampigia mwarabu siku mbili kabla nikamuekeza kesho kutwa nipitie kwakwe anichanganyizie ya kupandia ndege😃😃😃 akanambia siku hiyo nikivaaa nisipake chochote,ile muda naenda nipitie kwake.

Nikafata maelekezo ,nikamwambia staki iwe kali lakini nataka airport nzima waulize niwaachie no. Mweeeeee alinichanganyizie perfume 4 chap nikaelekea airport. Siku hizi siwahi sana na mimi najichelewesha kidogo🤣
Kwanza nilianza kumkomesha alonipeleka, pili tumefika tu wale wakaka wanakuja kutupokea mizigo nilisikia " dada unanukua"

Kwenye line ya ukaguzi nilikuwa naona watu wanaangaika kuniuliza. Ndani kuna sehem kama 3 za ukaguzi wale wadada kila mtu aliniuliza napaka perfume gani, mmoja nilimwachia no ya mwarabu.

Yeyote alonisalimmia siku hiyo kwa kunikumbatia basi mwaka mzima hiyo nguo alokuwa anaivaa hatopakaga perfume.

Mimi ile nguo nilokuwa nimevalia siku ile hata niifue vip itachukuwa miaka mitano perfumu ile kuisha.

Tangu nijuwe kwa mwaramu. Ni mwenye wa kwenda kupimiwa vichupa, leo nanukia hivi ,kesho vile.
Niseme tu pilikapilika za kupanda ndege naona kwangu hazitoisha maana kila ninapopanda naona kama vile ni mara ya kwanza.

Kuna wakati nilikuwa nawaza nivae kisuti matata maana wale wadada wa air tanzania wengine hata hawapendezagi, ila kuna wengine zile uniform zinawakaa balaa.ila baadae nikawaza huu uzi wanaopanda ndege wanavaa simple sio unavaa suti kama vile unaenda mahakamani 😃😀😀

Ndege oyeeeeeee!!!
Namba ya Muarabu 😂
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ni unaingia mwenyewe....

Mwenyewe ndege ikiwa inatembea hata kusimama siwezi...

Wale wanaoendaga Chooni ndege ikiwa juu wana moyo aisee...
🤣🤣🤣🤣 unaogopa ukitembea itaanguka?

Hata na mimi siwezi nyanyuka , safari yenyewe lisaa limoja sijaenjoy hata seat yangu mara tumefika sasa nanyanyuka kwenda wapi? Pilikapilika za ndege dah!
 
Tusiowahi kupanda ndege tuna-comment wapi?
Au ndio tuanzishe nyuzi za kupanda nyungo.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Ni unaingia mwenyewe....

Mwenyewe ndege ikiwa inatembea hata kusimama siwezi...

Wale wanaoendaga Chooni ndege ikiwa juu wana moyo aisee...
mbona ndege ikitulia unatembea vizuri tu coz kuna wakati inafika hata huhisi kama upo ndani ya ndege inayokwenda kwa kasi...so unaenda ma kurudi salama kbs, we huoni cabin crew wanavgotembea confidently kbs.! punguza wogaa uende chooni😅
 
Mimi natamani nikipanda ndege niende hata huko bafuni/ chooni nikaone kulivyo ila cha ajabu sijawahi kwenda. Maana nikikaa tu muda kidogo nasikia matangazo ya kushuka ati tumefika.

Ati nimeisha kaa niamke wanione naenda huko naonaga kama sio ustaarabu najikuta siendi.
Hivi kukoje huko toilet kwenye ndege?
choo cha ndege ni kidogo tu saizi ya kuingia mwili mmoja wa mtu mzima...sema shimo lake ni tofauti na tulivyovizoea, baadhi ya ndege huwa hakuna maji kuna only toilet papers...mimi nlivyoingia chooni nilitaka kutoka nduki wakati wa kuflash, mana ulitoka mlio mkubwa sana mle ndani hlf hakuna maji yaliyokuja kuflash choo bt punde choo (shimo) kikawa safi...nikafikiria kwmb kuna presha maalum ndo inatumika kuflash choo cha ndege na sio maji.

siku nyengine ukipanda ndege kubwa jikaze ukajionee mwnyw.😃
 
mbona ndege ikitulia unatembea vizuri tu coz kuna wakati inafika hata huhisi kama upo ndani ya ndege inayokwenda kwa kasi...so unaenda ma kurudi salama kbs, we huoni cabin crew wanavgotembea confidently kbs.! punguza wogaa uende chooni[emoji28]
Hapana siendi...Choo chenyewe huwezi hata kujigeuza....Ukijaribu tu ni unajigusa na board[emoji23]
Cabin Crew ukute nao wanaogopa ila basi tu...

Naonaga tu ile ndege ikishafika juu...zile lights zikizima watu wanavyoanza Movement najiuliza wanawezaje aisee....Maana mimi ndiyo kitu nimeshindwa.
 
choo cha ndege ni kidogo tu saizi ya kuingia mwili mmoja wa mtu mzima...sema shimo lake ni tofauti na tulivyovizoea, baadhi ya ndege huwa hakuna maji kuna only toilet papers...mimi nlivyoingia chooni nilitaka kutoka nduki wakati wa kuflash, mana ulitoka mlio mkubwa sana mle ndani hlf hakuna maji yaliyokuja kuflash choo bt punde choo (shimo) kikawa safi...nikafikiria kwmb kuna presha maalum ndo inatumika kuflash choo cha ndege na sio maji.

siku nyengine ukipanda ndege kubwa jikaze ukajionee mwnyw.😃
Eee mbona haya makubwa sasa kama hakuna maji unajitawaza na nini jamani?
 
Mie mbona sitasahau..
Siku iyo nilijipodoa kama naenda harusini kufika airport parfume yangu ikawekwa kwenye dustibini niliumia sana.

Nilipoingia ndani sijui ni uoga nikaita air host aje kunifunga mkanda kasheshe wakati wa kushuka mkanda ukanishinda kufungua ikabidi jirani yng kk mmoja anisaidie..
Haha umenikumbusha, niliwahi kupanda na dada mmoja toka Jro to Jnia, alinisumbua balaa, hajui kufunga mkanda wala kufungua, maswali njia nzima...kaka tupo wapi...kaka tutafika saa ngapi, ..kaka wakati wa kushuka itakuwaje..kaka kaka kila mara nilichoka sana maswali
 
Mimi natamani nikipanda ndege niende hata huko bafuni/ chooni nikaone kulivyo ila cha ajabu sijawahi kwenda. Maana nikikaa tu muda kidogo nasikia matangazo ya kushuka ati tumefika.

Ati nimeisha kaa niamke wanione naenda huko naonaga kama sio ustaarabu najikuta siendi.
Hivi kukoje huko toilet kwenye ndege?
Hii ni kwasababu labda unapanda za safari fupi ndani ya saa 1 na madakika, ukipanda ya masaa mengi hutaogopa kwasababu baada ya masaa kadhaa utakuwa ukiona watu wakipishana kwenda uani.
Mimi pia nilizoea hizi safari za ndani so nilikuwa naona sio ustaarabu kuamka amka na kwenda uani, nilipoanza kusafiru safari ya masaa mengi uoga uliishia pale hasa niliposafiri kwa masaa 13 mfululizo
 
Choo ni kidogo...

Niliingia ndege ilitua Zanzibar kutokea KIA to Dar....Na mimi ni kama wewe..nikasema leo wacha nikavione....kwanza na Mlango ukataka kunizingua[emoji1787]

Mimi kwenda Chooni ndege inatembea hapana aisee...Naona itadondoka
Na ulivyo muoga sasa, huo mlango uliokuzingua ni precision?
Maana vimilango vyao vya hovyo sana
Makiwendo 😁
 
Natamani ningekutana na huu Uzi kabla ya June 2021. Ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda ndege. Nilipokuja kuusoma kwa mara ya kwanza, nafikiri mwanzoni mwa mwaka Jana(2022) kama siyo mwishoni mwa mwaka 2021, nilicheka sana. "Washamba" wanafanana. Kama ningeusoma kabla, ningepata maarifa ambayo yangesaidia kupunguza "ushamba"

Ilikuwa Alhamisi Usiku, 30/06/2021. Nilikuwa natoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam kwa ndege ya ATCL.

Alfajiri ya siku hiyo, nilipigiwa simu na mmoja wa watu wangu wa karibu lakini sikuipokea. Nilihisi kuwa pengine huenda kashafahamu kuwa siku hiyo napanda ndege. Sikutaka aniambie chochote kuhusiana na ndege, asije akanivunja moyo kusafiri kwa ndege. Nilikuja kumpigia baada ya kufika Dar es Salaam.

Nilifika mapema sana Airport. Ilibidi nikae kwa massa kadhaa kwenye mgahawa ulio pale Uwanjani, nafikiri unaitwa JAMBO CAFE, kusubiria muda wa kuripoti kuwadia.
Nikiwa hapo, nilianza kuingiwa na hofu, kiasi cha kuishiwa na hamu niliyokuwa nayo ya kupanda ndege. Nilitamani kuahirisha. Hata hivyo, nilijipa moyo, nikajisemea moyoni liwalo na liwe lakini ndege lazima nipande.

Nilitamani nikae kiti cha dirishani ili niwe ninachungulia mandhari ya ardhini nikiwa angani, na kwa bahati nzuri, ikawa hivyo. Nilikaa kiti cha dirishani, lakini siku "enjoy" kama nilivyokuwa nikitarajia. Nilitishwa na umbali tuliokuwepo angani.

Dakika chache baada ya ndege kuruka, nilipochungulia chini kupitia dirishani, taa za majengo zilionekana kwa mbaali. Sikuwa na hamu ya kuendelea kufanya hivyo. Niliamua kukafunga kabisa kale "kapazia" ka dirishani ili nisiendelee kupaona chini. Ule umbali ulikuwa unanitisha. Ila abiria wenzangu walikuwa na amani sana. Kuna waliokuwa wakichezea simu zao na wengine kompyuta pakato zao, na wengine walikuwa wakipiga stori kwa furaha kabisa. Mimi nilikaa kimya, kama vile sitaki kuongea, kumbe nilikuwa nimegubikwa na hofu.

Mkao na ukimya wangu, ulikuwa kama wa mtu anayetafakari jambo kwa kina . Lakini sikuwa natafakari, nilikuwa nimezama katika maombi, japo yalikuwa ni maombi ya kimya kimya. Niliomba safari nzima, kuanzia ndege iliporuka uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Hadi ilipotua Dar.

Wakati ndege inatua, nilifikiri huo ni uwanja mwingine huko Zanzibar, kwa hiyo baada ya kushusha au kupandisha abiria wengine, tungeendelea na safari hadi Dar. Lakini kumbe sivyo, tulikuwa tumewawasili jijini.


Tulipotangziwa kuwa hapo tulipo ni Uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam, kwangu ilikuwa ni furaha isiyo na kifani.
Sikutarajia ingetuchukua muda mfupi kiasi hicho. Tulitumia kama dakika kumi na mbili hivi angani. Mimi nilitarajia tungekaa angani kwa dakika kama 30 hivi.

Njiani baada ya kutoka Airport, nilikuwa nikitabasamu na wakati mwingine kucheka mwenyewe, kila nilipokumbuka heka heka za kuanzia maandalizi hadi nilipokuwa kwenye ndege.

Bora tu ilikuwa ni one way, pengine kesho yake ningetakiwa kupanda tena ndege, sijui ingekuwaje. Huenda ningekataa. Hata wiki mbili baadaye, bado sikuwa tayari. Hofu bado ilikuwepo.

Ilinichukua zaidi ya mwezi mmoja hiyo hali ya hofu kunitoka. Ilipoisha, shauku nayo ilirejea.

Kwa kweli, usafiri wa ndege ni mzuri sana!

Hongera zake mkuu Clasi! Uzi wake umekuwa burudani na "darasa" kwa wengi, Mimi nikiwa mmoja wao!!!
Mkuu mbona safari ya Zanzibar..dar ni fupi sana na ndege wala haipai juu sana?.kutoka Karume ukipaa dakika 10 hivi unaiona Dar, na kushuka ni ndani ya dk 15 hadi 20 hivi.

Kwa airbus toka Zanz to Dar ni dakiko 15 tu.

Naam kukaa dirishani raha sana
IMG-20230505-WA0001.jpg
 
Hii ni kwasababu labda unapanda za safari fupi ndani ya saa 1 na madakika, ujipanda ya masaa mengi hutaogopa kwasababu baada ya masaa kadhaa utakuwa ukiona watu wakipishana kwenda uani.
Mimi pia nilizoea hizi safari za ndani so nilikuwa naona sio ustaarabu kuamka amka na kwenda uani, nilipoanza kusafiru safari ya masaa mengi uoga uliishia pale hasa niliposafiri kwa masaa 13 mfululizo
Nasema hivi lazima niende nextime 😆
 
Back
Top Bottom