kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Niliomba rubani asimamishe ndege nikajisaidie.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iwekwe kwenye katibaNdege iwe Lazima kila mwananchi
Unanikumbusha...kuna mchungaji alikuja airport na suti ya wachungaji wa vijinini alikaguliwa hadi biblia watu walicheka sana alivyokuwa na wengeMbona kimo humu? Ni mengi yalitokea siku hiyo ila kubwa kuliko yote usiku sikulala, lakini pia niliwahi kuliko kiumbe yeyote yule ,si wanasemaja 2hr? Basi mimi 5hrs before nilikuwa pale.
Utamu wa ndege haujawahi mwacha mtu, na ukubwa huu ndege nimepanda mara kibao ila naona vioja haviishi.
Mwaka jana kuna sehem nilikuwa naenda basi niko airport kuelekea dar basi kuna msanii mmoja wa kile nae kalikuwa kanaelekea dar amefika pale alikuwa kananukia perfume kali balaa kalipopita kila mmoja airport alitamani ajuwe ni perfume gani kapaka.
Nikasema hapana hii chimbo ya hii perfume naijuwa nikampigia mwarabu huyu kaka anauzaga perfume za kupima akikuchanganyia perfume lazima ukubali.
Basi si ndo akaniambia huyu msamii wakati anaelekea airport alipitia dukani kwake akasetiwa ndo akaelekea airport.
Nikajisemea nextime airport nzima watanikoma[emoji23][emoji23][emoji23]
Juzi tu kakatokea ka safari ka chap dar,nikampigia mwarabu siku mbili kabla nikamuekeza kesho kutwa nipitie kwakwe anichanganyizie ya kupandia ndege[emoji2][emoji2][emoji2] akanambia siku hiyo nikivaaa nisipake chochote,ile muda naenda nipitie kwake.
Nikafata maelekezo ,nikamwambia staki iwe kali lakini nataka airport nzima waulize niwaachie no. Mweeeeee alinichanganyizie perfume 4 chap nikaelekea airport. Siku hizi siwahi sana na mimi najichelewesha kidogo[emoji1787]
Kwanza nilianza kumkomesha alonipeleka, pili tumefika tu wale wakaka wanakuja kutupokea mizigo nilisikia " dada unanukua"
Kwenye line ya ukaguzi nilikuwa naona watu wanaangaika kuniuliza. Ndani kuna sehem kama 3 za ukaguzi wale wadada kila mtu aliniuliza napaka perfume gani, mmoja nilimwachia no ya mwarabu.
Yeyote alonisalimmia siku hiyo kwa kunikumbatia basi mwaka mzima hiyo nguo alokuwa anaivaa hatopakaga perfume.
Mimi ile nguo nilokuwa nimevalia siku ile hata niifue vip itachukuwa miaka mitano perfumu ile kuisha.
Tangu nijuwe kwa mwaramu. Ni mwenye wa kwenda kupimiwa vichupa, leo nanukia hivi ,kesho vile.
Niseme tu pilikapilika za kupanda ndege naona kwangu hazitoisha maana kila ninapopanda naona kama vile ni mara ya kwanza.
Kuna wakati nilikuwa nawaza nivae kisuti matata maana wale wadada wa air tanzania wengine hata hawapendezagi, ila kuna wengine zile uniform zinawakaa balaa.ila baadae nikawaza huu uzi wanaopanda ndege wanavaa simple sio unavaa suti kama vile unaenda mahakamani [emoji2][emoji3][emoji3]
Ndege oyeeeeeee!!!
Ahaaaa Muwege mnatuchukulia hata tu video. Airport vioja haviishagi wewe waweza kuwa unapanda kwa mara ya 1000 ila wanaopanda kwa mara ya kwanza hawakosagi.Unanikumbusha...kuna mchungaji alikuja airport na suti ya wachungaji wa vijinini alikaguliwa hadi biblia watu walicheka sana alivyokuwa na wenge
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kuna mtu alipiga magoti Amsterdam wakati wanaunga ndege waende switz. Haya ni maneno waliokuwa karibu walimsikia akisema.
"Eh baba! ushukuriwe kwa kunifikisha huku juu mbinguni baba! duniani dhiki na shida nyingi baba! Mweh ndaga mwalafyale mweh"
Ndege inahamasisha kutafuta pess zaid
Nakumbuka ilikuwa Mwaka 2008 mwezi Juni nilikuwa naenda kikazi Lusaka, Zambia basi sijui hili wala lile kwenye tiketi iliandikwa saa ya ndege kuondoka saa 12 asubuhi (ndege ndo inapaa) mimi nikajipa kama dakika 20 kutoka home Tabata mpaka Airport, nikidhani ni kama Mabasi ya Mkoani pale Ubungo stendi duuh ile kufika nikaambiwa muda umeisha daah! Nilichokaje. But taratibu nikajifunza muda wa kufika airport, vitu visivyoruhusiwa kubeba kwenye ndege.
**NEW DEVELOPMENT
Mwezi Juni 2015 nilipata safari ya kwenda CAMEROON (kwa hisani ya Watu wamarekani USAID) sasa tukiwa huko tukalipwa posho kwa hela ya huko Central African Franc sasa nikazibana nije kubadilishia Bongo nafika bongo Bureau De Change zote hawabadilishi hizi pesa yaani nmepagawa sijui nikazitupe Coco maana....
****MPYA ya 2016
Mwezi Januari nilienda NEW DELHI duuh pale airport hakuna sijui kutangaza wala nini ni KIMYA KIMYA tu ukisubiri matangazo utastukia ndege ishakuacha.
View attachment 336440
HAKIKA USHAMBA MZIGO!
Usafiri wa ndege ndio usafiri salama kuliko wowoteNilisoma vizur ndio maana nikajibu labda ewew ndio usome upya.,...kwa kukusaidia nilimqoute aliesema kuhusu mkusanyiko wa mabati na injini ubungo akimaniisha mabasi,,,nikamuulize kwani ndege Ni mkusanyiko wa chuma Hadi awe na uhakika wa usalama kiasi hicho!!!!nachoamini hakuna usafir salama duniani Kama siku ya ajali imefika..kikubwa kumuomba mungu na kuwa waangalifu tu.
Wapi hii?Mje mpokee mabegi yenu 😁View attachment 2606460
Zichange uende New Zealand hamu itakuisha kmmkMimi natamani nikipanda ndege niende hata huko bafuni/ chooni nikaone kulivyo ila cha ajabu sijawahi kwenda. Maana nikikaa tu muda kidogo nasikia matangazo ya kushuka ati tumefika.
Ati nimeisha kaa niamke wanione naenda huko naonaga kama sio ustaarabu najikuta siendi.
Hivi kukoje huko toilet kwenye ndege?
Choo ni kidogo...Mimi natamani nikipanda ndege niende hata huko bafuni/ chooni nikaone kulivyo ila cha ajabu sijawahi kwenda. Maana nikikaa tu muda kidogo nasikia matangazo ya kushuka ati tumefika.
Ati nimeisha kaa niamke wanione naenda huko naonaga kama sio ustaarabu najikuta siendi.
Hivi kukoje huko toilet kwenye ndege?
Kuna vya ke na me?Choo ni kidogo...
Niliingia ndege ilitua Zanzibar kutokea KIA to Dar....Na mimi ni kama wewe..nikasema leo wacha nikavione....kwanza na Mlango ukataka kunizingua[emoji1787]
Mimi kwenda Chooni ndege inatembea hapana aisee...Naona itadondoka
Nope....Kuna vya ke na me?